CCM yafanya maamuzi mazito Kamati Kuu?

CCM yafanya maamuzi mazito Kamati Kuu?

inwezekana yumo kwenye tuhuma, lakini ni mtu mwenye msimamo kwenye mambo abayo, hayaendani na utashi wa mwenyekiti eg kukemea OIC, sasa hao wengine sifikiri watakuwa na uwezo huo etc.

Labda uweke record yake kwa taifa amewahi kutufanyia nini hasa cha kumfanya awe tofauti na wengine mafisadi waliotajwa na Dr. Slaaa? au?
 
Mkuu,

Nina issues na hizi dataz.

Moja, kwani Umoja wa Vijana, kama ilivyo katika vyombo, vikao, na ngazi zingine za CCM, hawana utaratibu wa kuwa na viongozi tofauti kutoka bara na visiwani ? Itawezekanaje Rais ajiamulie kushauri eti wagombea wote watoke Zanzibar ?

Mbili, Kikwete amewezaje kutamka CCM kuna rushwa ? Hiyo kwake ni kukubali machafu ya chama tawala, na akitoa madai hayo anaweza kubanwa achukue hatua kwa kutumia ushahidi ambao atadaiwa, maana rushwa ni kosa la jinai. Kikwete atawezaje kweli kutangaza CCM kuna rushwa ?

Tatu,
umetuambia kwamba CCM watasikiliza rufani ya Nape. Lakini hapo hapo umetoka kutuambia kwamba CCM wameshaamua, wameshapitisha kwamba ni Wazenji tu ndio watakaogombea. Hapo unaona pamekaa sawa kweli ?

Nne, Kikwete hawezi kumuongelea mtoto wake kwenye kikao cha Central Committee. Hususan kumuhusisha na rushwa. Ni kitu bizarre!!!

Tano, kuna thread ilianzishwa kabla inasema imekuwaje kikao cha CCM kimefanyika Ikulu. Wewe ukakimbia kutafuta "dataz" kali zaidi lakini zilipofika zikaonekana kama dead on arrival kwa sababu zilidai kikao kimefanyika Dodoma, hadi Wakuu kina Masatu walipokushtua. Ulichanganya vipi data hapo?

Unaona matatizo ya "dataz" zako ?

Sasa anza mashambulizi lakini I hope unaelewa kwa nini wengine huwa tunakataa kuzimeza nzima nzima.

Soma HAPA.Ubishi mwingine ni for the sake ya kubisha tu.Could you be gentleman enough na kukiri kuwa ulichemka ku-criticize kabla hujawa na data za kutosha?Simpe rule ya criticism iko hivi:usikosoe kitu ambcho wewe mwenyewe huna data za kutosha kuhusu unachokikosoa.
 
The dataz za mwisho wa kikao:-

1. Ni kwamba hakuna zaidi kilichosemwa, kulikuwa na mashambulizi ya hapa na pale husu EPA lakini yalikwepwa kiaina aina.

2. Wabunge wote wa CCM, wametaka kifanyike kikao cha dharura cha wabunge wa CCM, kitafanyika kati ya kesho na keshokutwa chini ya mwenyekiti Pinda, Agenda ya Makamba.

3. Mwishoni pia Kulizuka tena mvutano mkubwa kuhusiana na uchaguzi wa UV-CCM, mkoa wa Dar, ambako mtoto wa Spika anaelekea kukubalika zaidi kuwa mwenyekiti wake mpya, lakini tayari mafisadi wameshapitisha mcehzo wao.

Wakuu heshima mbele, hapa tumefika mwisho wa wa dataz kuhusu kikako hiki, sasa labda kati ya leo na kesho na kuendelea tunaweza kupata some more ya yaliyojiri, lakini kwa sasa this is it.

Shukrani kwa wakulu wote, na JF mbele zaidi yaani one step ahead!
 
Soma HAPA.Ubishi mwingine ni for the sake ya kubisha tu.Could you be gentleman enough na kukiri kuwa ulichemka ku-criticize kabla hujawa na data za kutosha?

Simpe rule ya criticism iko hivi:usikosoe kitu ambcho wewe mwenyewe huna data za kutosha kuhusu unachokikosoa.

Mkuu Mlalahoi,

Heshima mbele bro, usiwe unapotea sana mkuu.
 
Mmeacha kuzungumzia kushindwa kwake kuliongoza Taifa kwenye suala la wizi wa fedha za EPA mmebakia kuimba nyimbo za CCM. Hivi mnafikiri ni bahati mbaya kwa NEC kukutana siku moja baada ya suala la EPA na kuja na maamuzi mazito?

a. Kule kulikoibiwa fedha kwa mabilioni hakuna mtu aliyetimuliwa, kuitishiwa kikao wala nini
b. Kule ambako hakuna wizi wowote ule wala kughushi watu ndio inadaiwa hata kupoteza kazi watapoteza.

Tukisema Ibara 15:1 Iko kazini watu wanasema tunaionea CCM.

MM,

I am with you on this, jamaa wa CCM wanawachanganya watu tu na kuondoa attention kutoka katika issue zinazohitaji immediate attention kama EPA na kutuletea hizi spin za UVCCM.

Tunawaangalia tu walivyoishiwa nyimbo.
 
Maamuzi hayo inasemekana ni mazito sana....At least humo ndani ya ccm...Lakini nadhani bado haija ainishwa wazi kwamba ni kivipi uzito huo wa hayo maamuzi utawapa tabu mafisadi na haki kutendeka.
 
Mkuu BAK, heshima mbele.
Haya unayoandika na kuzungumza una weza kututhibitishia?
"Mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni"

Haya yanasemwa na watu ndani ya CCM ambao walishiriki katika kumchagua mgombea wa CCM. Pesa nyingi sana zilikusanywa toka kwa mafisadi mbali mbali ili kutumika kuwahonga wajumbe ili wampigie kura huyo unayemuona wewe ni safi. Hili siyo siri na muda si mrefu kwa jinsi mambo yanavyoenda ndani ya nchi yetu litaanikwa hadharani. Hastahili kupewa haki yoyote ile, wakati mwingine kiongozi wa nchi inapofikia mahala ukaona uongozi wako unailekeza nchi mahali pabaya ni bora uyaweke mbele maslahi ya nchi yako badala ya kwako mwenyewe na kuamua kuachia ngazi.

Mpaka leo kashindwa kutwambia ni akina nani waliohusika na wizi wa pesa za EPA. Kiasi kilichoibiwa na kila mmoja, kiasi kilichorudishwa na kila mmoja. Kama kuna unmovable assets zilizokamatwa ziko wapi na zina thamani gani lakini wakati huo huo amekuwa na speed ya haraka mno kuwasamehe mafisadi wa EPA, wakati suala la EPA bado lina utata mkubwa miongoni mwa Watanzania wengi, lakini kasoro zote za utendaji wa Kikwete huzioni bali uko tayari kumpigia debe kama ni safi!!!! Hadi hii leo Kiwira kuuzwa kwa Mkapa bado ni kitendawili hadi hii leo mikataba ya uchimbaji wa madini haijanyiwa marekebisho yoyote ili Watanzania tunufaike na rasilimali zetu badala ya mafisadi na wageni. Hebu tumia akili yako uliyopewa na mungu kutafakari mambo kwa kina badala ya kukurupuka na kutoa sifa zisizostahili.
 
Rome haikujengwa kwa siku moja, na haya ni maoni yangu reading this situation na ninaweza nikawa wrong pia, na soon tukizipata dataz za mwisho kikao tutaziweka hapa.

Ahsante Wakuu!

Kaka Tatizo ni kuwa CCM haijengi bali INABOMOA kilichojengwa na TANU....

Tanzanianjema
 
Soma HAPA.Ubishi mwingine ni for the sake ya kubisha tu.Could you be gentleman enough na kukiri kuwa ulichemka ku-criticize kabla hujawa na data za kutosha?Simpe rule ya criticism iko hivi:usikosoe kitu ambcho wewe mwenyewe huna data za kutosha kuhusu unachokikosoa.

Mlalahoi,

Hujaelewa. Au huwa huelewi.

Moja, Nionyeshe ni wapi kwenye hilo gazeti waliposema, kama alivyodai mleta dataz, na kama nilivyopinga, kwamba Rais Kikwete ndio amejiamulia kuengua majina ya Watanzania Bara.

Mbili, Nionyeshe ni wapi kwenye hilo gazeti waliposema, kama alivyodai mleta dataz, na kama nilivyopinga, kwamba Kikwete ametamka kwamba UV - CCM kulijaa rushwa.

Tatu,
Nionyeshe ni wapi kwenye hilo gazeti waliposema, kama alivyodai mleta dataz, na kama nilivyo question, kwamba Nape ametupwa nje ya kinyang'anyiro lakini hapo hapo wamepitisha rufaa yake ya kutaka kuwa ndani ya kinyang'anyiro.

Nne, Nionyeshe ni wapi kwenye hilo gazeti waliposema, kama alivyodai mleta dataz, na kama nilivyopinga, kwamba Kikwete amemuhusisha mtoto wake na rushwa ndani ya CCM.

Tano, Nionyeshe ni wapi kwenye hilo gazeti waliposema, kama alivyo indicate mleta dataz, na kama nilivyopinga, kwamba mkutano ulikuwa Dodoma na sio Ikulu, Magogoni.

Nionyeshe sehemu moja niliyokosea katika issues tano nilizo zi raise. Moja tu, please!

Kuna vitu vinginge ukisikia tu unajua ni uongo on its face. Kikwete atam lambast vipi mtoto wake kwa rushwa ndani ya kikao cha Central Committee bwana ? Think about it man. Yani am vindicate Kubenea kwamba kuna fissures ndani ya familia ya Kikwete?

Nionyeshe nilipokosea, na ukishindwa kunionyesha usilalamike nikikwambia kwamba wewe huna sophistication ya kuchambua ninavyovichambua.
 
Labda uweke record yake kwa taifa amewahi kutufanyia nini hasa cha kumfanya awe tofauti na wengine mafisadi waliotajwa na Dr. Slaaa? au?

ukitaki kulinganisha linganisha vilivyo katika kundi moja yaani ccm, kwa hiyo katika kuona kwangu kati ya hao waliopitishwa kwa ajili ya mwenyekiti wa wazazi, na muona huyo ni bora kuliko hao wengine. licha ya ufisadi wake. alternatively naomba unipe uzuri wa hao waliopitishwa, bulembo, nyawazwa etc labda unaweza kubadili au ku-support msimamo wako
 
Kaka Tatizo ni kuwa CCM haijengi bali INABOMOA kilichojengwa na TANU....

Ndugu yangu Tanzanianjema,

Vipi ndugu yangu salama huko? Leo natafuta kisusio baba yangu na mbege kidogo! Lakini wewe ni ndugu yangu!
 
ukitaki kulinganisha linganisha vilivyo katika kundi moja yaani ccm, kwa hiyo katika kuona kwangu kati ya hao waliopitishwa kwa ajili ya mwenyekiti wa wazazi, na muona huyo ni bora kuliko hao wengine. licha ya ufisadi wake.

Sawa sawa, hakuna ugomvi kaka hapa tunajadili siasa tu ndugu yangu,

kama unasema licha ya ufisadi wake Mkono ndiye anayefaa, unataka niseme nini tena si umemaliza mkuu the genius wetu JF? au? Bwa ! ha!ha! ah! ah! ah!hasira hasara kaka!
 
Field Marshall Es,
Mkuu pamoja na kwamba mimi sio ktk kundi la wafuasi wa chama CCM, ningependa unifahamishe kidogo kuhusiana na hawa vijana waliochaguliwa toka Zanzibar... je, hawa wamechaguliwa kutokana na sifa zipi za uongozi au ndio ktk kuwavuruga tu Mafisadi..

Sijui kama umewahi kufikiria hili wakati ukimpongeza mkulu, lakini Mwenyekiti wenu siku zote ameonyesha dalili mbaya sana ktk uteuzi wake..mara nyingi huteua watu ili kumkomesha mtu mwingine, yaani kuna husda zilizojengwa hivyo kuondoa mzizi wa fitna hutafuta mganga nani kumwondoa mchawi..ndio maana baraza lake la kwanza la mawaziri lilikuwa Hovyoo, tazama Makamba na baadhi za teuzi zake ktk wizara nyeti kote wamejaa watu ambao kusema kweli hawakuwa na uwezo ktk utendaji kazi ila uwezo ktk kuweka vijembe na kufagia njia za mafisadi..

Sasa ikiwa changes haziwezi kutokea ndani ya uongozi wa serikali, zikafuatia ndani ya chama itakuwa vigumu sana kufanya mabadiliko yoyote ya ndani Washington yetu..sura zile bado zipo ndani na zinaendesha nchi!
Kusema kweli picha nzima inanipa kuwa chaguzi hizi hazikulenga uwezo wa watu hao kuongoza ila kuangamiza watu fulani...
 
una jua ndugu yangu mimi mambo ya sifa sinayo wether nipo genius au nafahamiana na watu na hapa najizui kutaja majina sababu itakuwa ni kutaka hizo sifa amazo hazina maana na pia najizui kusema wewe unajuana saana na fulani na fulani maana itakuwa ni kukukashifu ,( hayo ni ya kwangu) na kila binadamu ana uzuri/na ubaya wake , hivyo nakuomba kwa ustaarabu tu especially ukinijibu mimi mambo yanayo reflect hayo usiya weke, maana nakuheshima kama ulivyo, kama weakness unazo ni zako, nikikucheka au kukununia haitasaidia, kwa hiyo mimi nitachukua yalio mazuri yako, na mapungufu yako nitayaacha kama yalivyo, na ikibidi kukushauri nitafanya hivyo kwa ustaarabu tu either kwa uwazi or kwa chati/pembeni kwa sababu na wewe ni binadamu hivyo unahitaji misaada/michango ya wengine kuboresha ulicho nacho.
 
kwanza mkuu FM ES tunashukuru kwa kutupa taarifa ambazo bado zinakuwa chunguni, yani bado motomoto. Na endelea na moyo huohuo, manake habari njema ni ile ipatikanayo mapema.

Kuhusu kutofautiana kimawazo kwa mada zitolewazo. Nadhani kutofautiana kulikuwepo, kupo na kutaendelea kuwepo. Hivyo mkuu sio kila mtu anayetofautiana nawe basi ana nia mbaya. Kumbuka uono wako wewe Mkuu sio sawa na uono wa Mfumwa. Tunaweza wote tunaangalia mbele, kumbe mmoja ana ona km 6, mwingine km 3. Hivyo tuendeleze forum yetu kwa hoja.
 
Mkuu sina uhakika unasema nini, maana mimi siku zote ninatiumiza wajibu wangu hapa kama mwanachama, yaani kukata ishus, hayo ya nia mbaya umeyatoa wapi? Na unatokea wapi nayo? Hii topic iko sawa wala kwangu haina noma sasa sielewi unatkea wapi? au ndio ile eti ya kutaka kunikosesha raha, hivi kweli unaamini unainkosesha raha mimi hapa au wewe mwenyewe na wasomaji wengine? Bwa! ha! ha! ah! ah!

Mkuu najaribu kupitisha white zenfandel kidogo, cheeers!
 
una jua ndugu yangu mimi mambo ya sifa sinayo wether nipo genius au nafahamiana na watu na hapa najizui kutaja majina sababu itakuwa ni kutaka hizo sifa amazo hazina maana na pia najizui kusema wewe unajuana saana na fulani na fulani maana itakuwa ni kukukashifu ,( hayo ni ya kwangu) na kila binadamu ana uzuri/na ubaya wake , hivyo nakuomba kwa ustaarabu tu especially ukinijibu mimi mambo yanayo reflect hayo usiya weke, maana nakuheshima kama ulivyo, kama weakness unazo ni zako, nikikucheka au kukununia haitasaidia, kwa hiyo mimi nitachukua yalio mazuri yako, na mapungufu yako nitayaacha kama yalivyo, na ikibidi kukushauri nitafanya hivyo kwa ustaarabu tu either kwa uwazi or kwa chati/pembeni kwa sababu na wewe ni binadamu hivyo unahitaji misaada/michango ya wengine kuboresha ulicho nacho.

Hapana mkuu nimeamua ku-support chaguo lako la Mkono kuwa mwenyekiti wa Wazazi, punguza jazba huu ni mjadala wa siasa tu! Bwa! ha! ha kwani nakatazwa kucheka? Bwa!ha!ha !ha ha! a!h
 
Field Marshall Es,
Mkuu pamoja na kwamba mimi sio ktk kundi la wafuasi wa chama CCM, ningependa unifahamishe kidogo kuhusiana na hawa vijana waliochaguliwa toka Zanzibar... je, hawa wamechaguliwa kutokana na sifa zipi za uongozi au ndio ktk kuwavuruga tu Mafisadi..

Sijui kama umewahi kufikiria hili wakati ukimpongeza mkulu, lakini Mwenyekiti wenu siku zote ameonyesha dalili mbaya sana ktk uteuzi wake..mara nyingi huteua watu ili kumkomesha mtu mwingine, yaani kuna husda zilizojengwa hivyo kuondoa mzizi wa fitna hutafuta mganga nani kumwondoa mchawi..ndio maana baraza lake la kwanza la mawaziri lilikuwa Hovyoo, tazama Makamba na baadhi za teuzi zake ktk wizara nyeti kote wamejaa watu ambao kusema kweli hawakuwa na uwezo ktk utendaji kazi ila uwezo ktk kuweka vijembe na kufagia njia za mafisadi..

Sasa ikiwa changes haziwezi kutokea ndani ya uongozi wa serikali, zikafuatia ndani ya chama itakuwa vigumu sana kufanya mabadiliko yoyote ya ndani Washington yetu..sura zile bado zipo ndani na zinaendesha nchi!
Kusema kweli picha nzima inanipa kuwa chaguzi hizi hazikulenga uwezo wa watu hao kuongoza ila kuangamiza watu fulani...

Mkuu Bob,

Heshima mbele sana, ninakubaliana kabisa na analysis yako kwa 100%. kwa leo nimechoka sana na furaha ndugu yangu naomba kupumzika kidogo, nifurahie huu ushindi, na kesho is another day!.
 
OMG.jpg

...............................
 
Back
Top Bottom