CCM yafanya maamuzi mazito Kamati Kuu?

CCM yafanya maamuzi mazito Kamati Kuu?

Mkuu FMES hapa chumbani kuna habari za kutisha zina miminika juu ya tukio hili .Nataka kwenda pale Nyerere square nianze kuona nje ya ofisi za CCM kutakuwa na hali gani .Mkono tena ? Why ?Wacha nithibitishe hizi kwanza .

Sawa sawa, nitaku-beep soon narudi kulala tena maana mawasiliano magumu sana na chumba cha mkutano.
 
Mkuu,
Hapa mfano wa Yesu ni JK na .... na ... na Mimi na .... na ....


Heshima mbele Mkulu,

Umesema vyema,JK yesu na wewe sijui nani........


Sawa,kama hivyo ndivyo,sijui kama unajua kwamba Mungu ni Dictator mamraka yake hayana Ubiya hana wakumwogopa wala kumashauri kwenye maamuzi
Mungu akitaka ufe utakufa tu,ufungwe utafungwa,upate ridhiki yako utapata(wazee wa EAC).
sasa huyu wako wewe hata swala la EPA linamshinda
 
Well hii taarifa ya CCM , naona kuna ambao imewafurahisha sana, inaonyesha CCM wanaweza wakacheza trick au wakafanya jambo amablo watanzania wapenzi wa CCM wakalifurahia, quotes zote hapo juu zinapelekea

1. Kuwasifu CCM!!!
2. Kuwa alert CCM wasifanye makosa
3. Zinaonyesha ni za wapenzi wa CCM waliochoka na mwenendo wa CCM
4. Mpaka wengine wanamsaidia Kikwete amweke katibu nani!!!!

Hii inanipa picha kuwa CCM kuondoka madarakani ni kazi sana, maana wale wapinzani nao pia ni washabiki wa CCM, yaani ni kama Yanga anacheza na Arsenal huku kuna wachezaji wa Yanga ambao ni arsenal damu!!

Hii hali inatisha, inabidi tukae chini na kujiuliza CCM tangu mwaka miaka ya 60 mpaka leo imefanya nini au ndio kuwa excited na habari za UVCCM?

Kazi hipo, kuna somo kali inabidi litembee hapa

CCM inabidi iondoke madarakani kwa namna yeyote ile!!!! mpo!!!!!

Kama dataz ni hizi za kichama!! nina wasiwasi haya tupo!

what are you exciting for??

We have proved by any means CCM 'hawatatutoa' lets build our strategy how to remove them from power!!

Kesho Kikwete akisema anajiuzulu nafasi yake kuchukuliwa na fulani mnayempenda mtaandamana mtaani kuisifia CCM, kama Mkapa alivyomwachia madaraka Kikwete amekaa pembeni ametulia-anakula nchi na kiwira yake, ndivyo mtakavyofurahi eti kusikia Kiwete amejiuzulu, atakaa pembeni na kula nchi, hao mnaowaona wazuri SIO WAZURI WANGEKUWA WAZURI TU, KAMA WANGEONDOKA CCM, KAMA NYERERE ALIVYOSHAURI, angalau mrema alijaribu

sijaona mwanamapinduzi ktk post hizo hapo juu nimeona washabiki wa CCM waliojificha ndani ya mwamvuli wa wanamapinduzi! ambao wako tayari kutuaminisha kuwa hawaipendi CCM huku wa vinywa na matendo wakiipenda CCM. Sina maana hawatakiwi washabiki a CCM humu la, swala ni kuwa kama mshabiki wa CCM, bado una ndoto kuwa iko siku CCM watafanya mabadiliko naomba, nikuonee huruma sana, CCm ndio waliotufikisha hapa tulipo tukiwa nchi ya pili kwa umaskini duniani, lakini inayoongoza kwa mali asili!

Sorry ,my style of writing this kind of critics is ''message sent' huwa sina utaalamu wa kumuelewesha mtu anayebisha au kupinga nilichoandika


Someni tena post zenu, muwaleze watu kuwa maana yenu ni nini? FMES kweli hulali kisa CCM

haraka haraka naona ktk kundi hilo hapo juu kuna waliokuwa CCM walihama, lakini wana kadamu ka CCM, na wako tayari kurudi wakisikia kitu cha kuwafurahisha HATA KAMA NI KIINI MACHO!!! HATA KAMA HAKILENGI KUWASAIDIA WATANZANIA WOTE!!
''don't mind criticism. If it is untrue, disregard it; if unfair, keep from irritation; if it is ignorant, smile; if it is justified it is not criticism, learn from it''.


waberoya

heshima kwako mwanamapinduzi waberoya,

naamini ni haki yako ya kimsingi kutoa tafsiri ya mchango wa memba hapa na matukio ya kisiasa yanatokea katika taifa letu. na katika haki yako hiyo unayohaki pia ya kuamua nani ni mwana mapinduzi au la.

aidha naamini ni haki yangu ya msingi kutoa tafsiri ya matukio ya kisiasa na mchango wa memba humu jamvini bila kujaribu kwa makusudi kabisa kumkwaza mtoa hoja. sasa tafsiri yangu ni kwamba umeniita kinyume cha mwana mapinduzi ambayo kwangu mimi ni msaliti! sina pingamizi kwa wewe kuniona msaliti kwa mtazamo wako lakini napinga vikali kama tafsiri yako ni kumaanisha mimi ni msaliti kwa taifa langu. japokuwa mimi si mwanachama au shabiki wa chama chochote cha siasa naamini kabisa kuwa mwanachama wa ccm si usaliti aslani wala si kukosa uana mapinduzi.

nakutakia mafanikio katika harakati za mapinduzi.

hayo ni maoni yangu tu na kama wewe samahani kama nimetumia lugha nzito.
 
The more dataz ni kwamba:-

1. CC imepitisha majina 3 ya wagombea uenyekiti wa UV-CCM toka Zanzibar, nao ni Yusuf Hamadi Masauni, Suleiman Haji, na Adila Vuai.

2. Mvutano mkubwa ulizuka katika kuamua nini cha kufanya na uchaguzi wa makamu wa mwenyekiti wa UV-CCM, ambapo katiba inasema wazi kwamba hapa ni lazima atoke bara,

- Baada ya mvutano mkali sana, ikaamuliwa majina ya waliokuwa wakigombea uenyekiti yachujwe na wachaguliwe kutoka kundi hilo kupata mgombea umakamu, kwa hiyo CC imewapitisha wagombea:- Beno Malisa, Hassan Bashe, na Bi Z. Kawawa.

3. Kwa upande wa Mwenyekiti wa Wazazi, leo jina la Mkono limetenguliwa, na kupitishwa majina matatu nao ni Bulembo, Mhina, na Mama Nyawazo.

4. Umoja wa kina mama, huko yameachwa majina yale yale matatu, yaani Mama Janet Kahama, Mama Sophia Simba, na Mama Masunga.

Kikao kinaendelea bado na tutaoa more dataz zitakapopatikana tu, ingawa sasa hivi ninapoandika ndio inajadiliwa agenda ya yaliyojiri Tarime, yaani Makamba na Msekwa on the hot seat.

So far hay ndio maamuzi muhimu yaliyofanyika, lakini baadaye tutakwua na more breakdown ya exactly yaliyojiri ndani ya kikao cha jana na leo.

Ahsante Wakuu!

Hii ya kumtoa Mkono ni kwamba anaogopa a Strong figure kwenye CC., maana wengine watakuwa vibaraka tu.
 
Nakubaliana na dataz hizi za Mkuu FMES......

Nakubalina kuwa wao kama wana ccm kuna ambao ni kweli wamechoshwa na ufisadi.

Lakini mimi binafsi sina chama kwasasa...Ila nikiambiwa nitowe mchango wangu kwenye hili...Basi nitasema ni kama kuchanga karata upya tu...Ila karata ni zile zile...Kwenye ulambaji ndio muhimu kwani wakati wa uchangaji ni lazima kuna upangaji..Hilo hatukwepi kwasababu lazima kuna agenda kwenye reshuffle...Tuombe Mungu wazalendo walambe dume...Hata hivyo kusema eti kutakuwa na mabadilko constructive wakati timu ni ile ile ni jambo gumu kidogo.

Tutegemee nini kutokana na hilo?

Je huo uchaguzi wa uvccm ndio uliosababisha Mh Rais akashindwa kufanya la maana kuhusiana na ufisadi kama vile EPA nk?
Sitaki kuamini hivyo.

Hata hivyo FMES nawatakia kila la kheri kwani njia mliyoichaguwa ni nyie mtakayoipita na muhakikishe ni constructive na si politics as usual.

Kuna wakati wananchi walikuwa excited kama wakati wa issue ya Lowassa kujiuzulu na kuundwa kwa baraza jipya?

Kama ni upotezaji wa muda basi sisi watanzania tuko mbele sana..Yani njia sahihi zinaweza kuonekana lakini viongozi bado wanapenda kutufanyia majaribio ili kuona reaction yetu.

Haya wanayofanya ccm kama haikuwa politics basi wangetakiwa kufanya loong time ago.

Tulishaanzisha hadi threads hapa za kuwataka wafanye mabadiliko...Lakini individualism inapewa sana kipaumbele..Angalia ni mambo mangapi tungeyaepuka kama wangefanya haya kitambo...Sasa hivi ni kinda late....Na siyo tu ni late...Bali sidhani kama kuchangwa upya kwa karata ni mwisho wa kupata garasha especially kama kuna kupangia.
 
Kwa hiyo huko CCM huyo Yesu Kristo ni nani anayefananishwa nae? Ingawa naweza kuikubali katika muktadha wa "Msafara wa mamba, na kenge wamo", sijawahi kuona wala kusikia kuwa mamba wameonekana kwenye msafara wa kenge! Na kwa kiingereza kuna nyingine: "Birds of a feather flock together".

Mkuu Kithuku, Heshima mbele;
Watu kama JK na Pinda ni watu safi ambao ninaweza kusema kuwa ni "wale wanaokula na wenye dhamb" lakini wao ni watu safi.
Wengine walio safi nitasema baadaye.
 
AH! Tunasubiri, na sasa sijaelewa hii inamaanisha nini!
 
Mkuu Kithuku, Heshima mbele;
Watu kama JK na Pinda ni watu safi ambao ninaweza kusema kuwa ni "wale wanaokula na wenye dhamb" lakini wao ni watu safi.
Wengine walio safi nitasema baadaye.

Ndio hapo usemi wote kuwa issue hii ni sawa tu na kuchanga karata upya...Karata ni zile zile na chaguo la Mungu ni lile lile...Mungu na awaepushe watanzania na manabii wa uongo.
Amen.
 
Hii ya kumtoa Mkono ni kwamba anaogopa a Strong figure kwenye CC., maana wengine watakuwa vibaraka tu.

Hivi mkono si alikuwemo kwenye list ya mafisadi ya Dr. Slaa, au? Halafu si alisema anaenda mahakamani kumshitaki Dr. Slaa kwa sababu ya ile list hivi alijaishia wapi?
 
Hivi mkono si alikuwemo kwenye list ya mafisadi ya Dr. Slaa, au? Halafu si alisema anaenda mahakamani kumshitaki Dr. Slaa kwa sababu ya ile list hivi alijaishia wapi?

No kweli kuwa Mkono alikuwemo, ila kutoka mwanzo yeye alisema hatokwenda mahakamani
 
The more dataz ni kwamba:-

1. CC imepitisha majina 3 ya wagombea uenyekiti wa UV-CCM toka Zanzibar, nao ni Yusuf Hamadi Masauni, Suleiman Haji, na Adila Vuai.

2. Mvutano mkubwa ulizuka katika kuamua nini cha kufanya na uchaguzi wa makamu wa mwenyekiti wa UV-CCM, ambapo katiba inasema wazi kwamba hapa ni lazima atoke bara,

- Baada ya mvutano mkali sana, ikaamuliwa majina ya waliokuwa wakigombea uenyekiti yachujwe na wachaguliwe kutoka kundi hilo kupata mgombea umakamu, kwa hiyo CC imewapitisha wagombea:- Beno Malisa, Hassan Bashe, na Bi Z. Kawawa.

3. Kwa upande wa Mwenyekiti wa Wazazi, leo jina la Mkono limetenguliwa, na kupitishwa majina matatu nao ni Bulembo, Mhina, na Mama Nyawazo.

4. Umoja wa kina mama, huko yameachwa majina yale yale matatu, yaani Mama Janet Kahama, Mama Sophia Simba, na Mama Masunga.

Kikao kinaendelea bado na tutaoa more dataz zitakapopatikana tu, ingawa sasa hivi ninapoandika ndio inajadiliwa agenda ya yaliyojiri Tarime, yaani Makamba na Msekwa on the hot seat.

So far hay ndio maamuzi muhimu yaliyofanyika, lakini baadaye tutakwua na more breakdown ya exactly yaliyojiri ndani ya kikao cha jana na leo.

Ahsante Wakuu!

Mkuu FMES pia nadhani ulisema hapo awali kuwa waliamuwa kuwateuwa wagombea kutoka Zanzibar kutokana na mgogoro wa kina Beno Malissa...Sasa Beno ndiyo bado mgombea Umakamu...Je si kutatuwa na tatizo hapo?
Kama sijaelewa naomba unieleweshe mkuu.....Kwasababu Nape na yeye si angewekwa kwenye huo uteuzi wa Umakamu?
Kwasababu nadhani kama kulikuwa na mgogoro kwenye uenyekiti...Umakamu nao inaweza kuwa the same maana kuwapa hao wazenji ni kanyaboya tu...Kazi za Bara watazifanya wenye utaalam na bara...This time makamu.
I stand corrected.
 
Mkuu Kithuku, Heshima mbele;
Watu kama JK na Pinda ni watu safi ambao ninaweza kusema kuwa ni "wale wanaokula na wenye dhamb" lakini wao ni watu safi.
Wengine walio safi nitasema baadaye.

Utakuwaje mtu safi kama umetumia pesa za mafisadi akina Jeetu, Subhash, Manji na wengineo wengi kuingia madarakani? Pesa hizo zilitumika kutoa hongo kwa wajumbe wa CCM waliopiga kura kumchagua mgombe Urais 2005. Hakuna usafi hata kidogo na hizo pesa walizomkusanyia wahindi na mafisadi wengine. Subhash ndiye alikuwa anakusanya kwa wahindi wenzie na kuzikabidhi kwa waliomo ndani ya mtandao ili zitumike kama hongo. Kuna usafi kweli hapo?
 
Ndio hapo usemi wote kuwa issue hii ni sawa tu na kuchanga karata upya...Karata ni zile zile na chaguo la Mungu ni lile lile...Mungu na awaepushe watanzania na manabii wa uongo.
Amen.

Mkuu Jo... Mushi, heshima yako.
ulichoomba unakiamini au ni kwavile umeona na kusikia wengine wakiomba?
Unapoomba unamuomba Mungu yupi?

Nyongeza ya watu safi: Msekwa, Makamba, ... wengine nitaongeza baadaye.
 
Mkuu Jo... Mushi, heshima yako.
ulichoomba unakiamini au ni kwavile umeona na kusikia wengine wakiomba?
Unapoomba unamuomba Mungu yupi?

Nyongeza ya watu safi: Msekwa, Makamba, ... wengine nitaongeza baadaye.

Mkuu wewe si mchungaji?
Mmesahahu kuwa mlisema ni chaguo la Mungu?
Ndio maana sishangazwi na usafi unaouona...Maana inawezekana kuwa kiongozi wa dini si lazima uwe safi.
Mimi sipingani na maoni yako kama member wa JF...Ila maoni yako kama mchungaji kwasababu mliwaambia waumini wenu maneno kama haya na matokeo yake ni haya...Sasa Mungu wenu nyie mlio na macho ya kuuona usafi wa viongozi hao uliowataja hapo juu ni Mungu yupi huyo?

NB:Kama unakumbuka nilishawahi kukuuliza huko nyuma...Je wewe ni mchungaji wa mbuzi ama kondoo?
 
Mkuu Jo... Mushi, heshima yako.
ulichoomba unakiamini au ni kwavile umeona na kusikia wengine wakiomba?
Unapoomba unamuomba Mungu yupi?

Nyongeza ya watu safi: Msekwa, Makamba, ... wengine nitaongeza baadaye.

Huyu Makamba anayeshinda kwa Manji kila siku akiomba Michuzi? Si Makamba huyu huyu aliyedai mkataba wa jengo la UV-CCM haujasainiwa kumbe alikuwa ni muongo. Si Makamba huyu huyu ambaye baadhi ya watendaji wa CCM katika mikoa mbali mbali hawataki kusikia jina lake au kuiona sura yake? Na huyo Msekwa si ndiye aliyetaka kuuza ardhi kwenye mbuga za wanyama kwa wageni si ndiye huyu huyu aliyepewa nafasi ya umakamu CCM katika mazingira ya kutatanisha pamoja na kuwa hakuwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo? Acha tabia ya kutaka kutetea visivyostahili kutetea. Inaelekea na wewe kwa namna moja au nyongine unafaidika na ufisadi ndiyo maana unatetea watu ambao uongozi umewashinda.
 
Hata hivyo FMES nawatakia kila la kheri kwani njia mliyoichaguwa ni nyie mtakayoipita na muhakikishe ni constructive na si politics as usual.

Mkuu Mushi,

Heshima mbele, kwa maoni yangu ni kwamba kilichotendeka hapa na haya maamuzi ni a response ya rais kwa ajili ya uchaguzi wa 2010, hasa kwa kuzingatia matokeo ya Tarime ambayo pamoja na makosa mengi ya CCM, lile la Vijana lililosababisha yule kiongozi kujitoa UV-CCM na kujiunga na Chadema the last minute, linaaminika sana ndani ya uongozi wa CCM kwamba lilikuwa moja ya sababu kubwa ya kushindwa kwa CCM. Kampeni chafu za huu uchaguzi wa Vijana, zilikuwa zinatishia sana kumeguka wka CCM.

Rais pia anajaribu kuhakikisha CCM haimeguki, ndio maana ya kupewa nafasi kwa mafisadi kwenye nafasi ya kugombea nafasi ya makamu wa mwenyekiti, ambayo tayari ameshizuia na kumpigia ndogo ndogo anayemtaka.

Hapa mshindi ni Kubenea, ambaye aliyasema haya yote, na waliokuwepo kwenye kikao wamejionea wenyewe jinsi Muungwana alivyolalamika sana kwa wazee huko CC kumuunga mkono hoja ya kuwazuia wagombea wa Bara ambapo alilia sana kuhusu kuhusishwa kwa mtoto wake na hizo kampeni chafu, kwamba "... Ridhiwani amekuwa akizunguka sana mikoani kwenye hizi kampeni...", mshindi hapa ni Kubenea.

Walisohindwa hapa ni kwanza ni Mkuchika ambaye ameachwa in the air na this a slap in his face, na sasa analalamika sana huko pembeni kwamba amepandishwa mkenge. Sasa not only that tu ni kwamba kitendo chake cha kwua at odd na waandishi wa habari kimempunguzia uwezo wa kuchukua nafasi ya bosi wake, Makamba ambaye habari zake ziko wazi kabisa kwamba he is on the wway out kama sio tayari. Wajumbe wengi waliojadili na muungwana kwa siri wamelikataa jina la Mkuchika kwa sababu ya standing yake na waandishi kwamba hawezi kuidsaidia CCM na hiyo reralition yake na media.

Mwingine aliyeshindwa hapa ni Makamba wabunge karibu nusu wa CCM wamemtumia ujumbe jana rais kwamba ni lazima aondolewe soon au sasa kwa sababu hawako tayari kusimama naye wkenye kugombea ubunge kwenye uchaguzi unaokuja, hasa baada ya Tarime. Kinana ndiye aliyetgemewa kushika nafasi hiyo, lakini inasadikiwa kwamba Kinana ana agenda moja kwanza kabla ya zote, nayo ni kuwafuta uanachama CCM mafisadi wote as soon as akiingia tu!

Sisi wananchama wa CCM, inategemea upo kundi gani, lakini kwa wale tuliko kundi la kupiga ufissadi kama linavyojulikana yaani la "wapiganaji" huu ni ushindi mkubwa sana kwa sababu, uchaguzi wa Tarime ndio umeweka wazi umuhimu wa nafasi yetu ndani ya CCM, na ni uchaguzi huo hasa ambao tuliogomea kabisa na kutokwenda huko ndio in a big part umeleta matokeo haya ya sasa ya CC.

Halafu Nape ni another hero wa this thing kwa sababu can you imagine bila Nape kuleta ule mtafaruku, Nchimbi si leo angekwua anakunywa mvinyo kwa kuku tu! again Nape won hapa, tena big time, sasa anajiweka kwenye nafasi nzuri sana kwenye kugombea nafasi yoyote kwenye chama, ingawa tayari jina lake linatajwa kwenye nafasi moja nzito sana.

Rome haikujengwa kwa siku moja, na haya ni maoni yangu reading this situation na ninaweza nikawa wrong pia, na soon tukizipata dataz za mwisho kikao tutaziweka hapa.

Ahsante Wakuu!
 
Mkuu,
Hapa mfano wa Yesu ni JK na .... na ... na Mimi na .... na ....

Hizi ni kufuru na kejeli juu ya M/Mungu na Masihi wake..

Nafikiri inabidi mkemewe sasa, naona inakuwa too much..Msilete mifano ambayo inatukwaza tafadhali
 
Mzee ES heshima mbele mkuu maana umeweza kubreak hii kitu kwenye mtiririko unaotakiwa na kuweka issue nzima kwenye mstari.

Ahsante mkuu na kama kawaida kwenye breaking news tu uko mbele mkuu.
 
Field Marshall ES
Field Marshall ES has no status.
JF Senior & Premium Member Join Date: Thu Apr 2006
Posts: 7,194
Rep Power: 37

Thanks: 7,180
Thanked 6,011 Times in 2,503 Posts
Credits: 672,395

Re: ...CC Ikulu Dar Mafisadi Chini!

NIONAPO JINA HAPO JUU NAKUWA INT KUSOMA ALICHOTOA HUYU BWANA MAMBO YAKE NI MAZITO LABDA KWA UFUPI KIJANA USIKATE TAMAA NDUGU TUKO NNYUMA YAKO
 
Mpaka dakika hii kichwa kinanizunguka. Kama mliwahi kusikia usanii Tanzania, ndio huu na CCM imeonyesha kuwa si tu ni chama cha kisanii bali kinaongozwa na wasanii waliobobea. Nimejizuia kuchangia nione huu mchezo wa kuigiza utaishia wapi lakini naona imekuwa kama ngoma mduara. Hakuna kusimama katikati kwenye vita tulioyo nayo - one is either with them or against them.

Inanikumbusha Nduli Idi Amin alivyokuwa mjanja kwani kila alipohisi kuwa kuna matatizo ya kiutawala yanamnyemelea, alizua mambo kama ya kuvamiwa na nchi jirani na hivyo kujipa muda wa kushughulikia wabaya wake wa ndani. Baada ya CCM kuona wananchi wanaaza kushtuka kama walivyoonyesha wana Tarime, wamekaa chini na kusuka hizi tunazoletewa kama eti mara MAFISADI wapigwa chini (sic)

Ukweli ni kwamba kundi lote la mafisadi liko pale pale na linalofanywa ni changa la macho na danganya toto. Wadanganyika kama watoto wa mitaani, wanaitikia ngoma ya mdundiko kama kawaida yao wakati EPA, Richmond, IPTL, Meremeta, Tangold, Kiwira n.k. ziko pale pale. Sana sana sasa wanachofanya mafisadi wakiongozwa na kamanda wao JK ni "regrouping" kwa ari, kasi na nguvu mpya.

Mama Kilango yu wapi, Mwakyembe yu wapi, Kimaro yu wapi, Nape yu wapi na wengine wengi tu. Nguvu ya mafisadi ipo kwenye umoja wao na thubutu uonekane msaliti, hutapewa nafasi ya kupumua. Juzi tu favorite wa jumuiya ya Wazazi, fisadi Mkono kapotea njia na kulivalia njuga swala la Buhemba, je kuna mtu anashangaa na kutoswa kwake ?

Mkuu FMES, nakupa heko kwa kumwaga dataz na naomba uendelee lakini naomba uwe mwangalifu - unaweza kutumiwa na wajanja bila kujua. JF inaweza ikajikuta inapambana na vivuli tu vya maovu nchini kwa kulishwa ubwabwa na makanyagio huku minofu ikiendelea kutafunwa kwenye vikao eti vya siri vya walafi. Sisemi kuwa unayotuletea sio kweli ila tutapoteza dira kama tutaamini kuwa hapa kuna nia ya dhati ya kupambana na UFISADI.
 
Back
Top Bottom