CCM yafanya maamuzi mazito Kamati Kuu?

CCM yafanya maamuzi mazito Kamati Kuu?

Uchaguzi wa wazinzibari kugombea uenyekiti badala ya watu wa bara na wagombea kutoka bara waliomba uenyekiti kupewa nafasi ya umakamu uenyekiti kwa gia ya kuwaadhibu mafisadi inaweza isifanikiwe. Kwa nini nasema hivyo.....

Tunajua sehemu kubwa ya umoja wa vijana ipo Tanzania bara, kwa maana hiyo hawa wagombea kutoka bara(tunaohisi wanakuwa backed na mafisadi) kwa kiasi kikubwa wana influence kubwa kwa wajumbe na viongozi wengi upande wa bara. Kwa maana ya kupewa nafasi ya kugombea umakamu mwenyekiti iwapo mmojawapo atashinda anaweza still akawa na influence na nguvu kubwa kuliko mwenyekiti (mgeni kutoka znz) kwa sababu ya mtandao wa viongozi wa chini waliojijengea. Hii itamaanisha nguvu ya mwenyekiti itakuwa limited na still mafisadi watakuwa still na influence kubwa kulinda mambo yao.

Dawa ilikuwa kukata kila jina kama kweli sababu ilikuwa ni kuwa wanakuwa backed na mafisadi kwa hiyo mwenyekiti wa CCM akahisi kuwa nia ya kusafisha chama haitatimia. Otherwise muono safari bado ni ndefu kwa CCM kama kweli inataka kujisafisha.
 
ukitaki kulinganisha linganisha vilivyo katika kundi moja yaani ccm, kwa hiyo katika kuona kwangu kati ya hao waliopitishwa kwa ajili ya mwenyekiti wa wazazi, na muona huyo ni bora kuliko hao wengine. licha ya ufisadi wake. alternatively naomba unipe uzuri wa hao waliopitishwa, bulembo, nyawazwa etc labda unaweza kubadili au ku-support msimamo wako

Huyu ni mmoja wa watu wanaowakilisha watanzania wengi sana,
You wrote this in your sense??...unajua fisadi ila ana uafadhali....

damn!!!!

waberoya
 
Huyu ni mmoja wa watu wanaowakilisha watanzania wengi sana,
You wrote this in your sense??...unajua fisadi ila ana uafadhali....

damn!!!!

waberoya

Ndudgu yangu Wareboya....hao mafisadi waliowekwa wawe wasaidizi ndio watakuliza kabisa, halafu mtu aseme sisiemu imewashinda mafisadi, what the.....Tanzania sio na nchi gani?

nakumbuka msemo huu wa kitoto...AIM HIGHER YOUR FAILURE WILL BE SUCCESS
 
Huyu ni mmoja wa watu wanaowakilisha watanzania wengi sana,
You wrote this in your sense??...unajua fisadi ila ana uafadhali....

damn!!!!

waberoya

Basis zangu nimezitaja, lakini kama wewe unaona tofauti andika hizo zako, nami naweza kukubaliana na wewe au la, badala ya kutumia neno damn!!!, na hapo ninalinganisha na hao waliopitishwa. Bulembo, nyawazwa, na Mhina. Kama katika moja wao anaweza kusima kwenye CC , na kuongelea mambo ya kitaifa bila woga na kufinyanga finga maneno.
Sorry sitatumia neno kwamba ulicho andika hapo ulikuwa uko kwenye sense zako au la?
 
Samahani sana August kwa kutumia neno damn!,nimegundua halikuwa zuri pale..sorry ila bado siamini kuwa kuna usafi wowote CCM. August tuwaze kuiondoa CCM, hakuna cha uafadhali humo wala justification yeyote.

Kwa kifupi, katika zama hizi za vyama vingi , kiongozi yeyote wa CCM anayejiona msafi ni mnafiki na mwongo.Kubaki CCM ni kutaka kula, marupurupu na vijisenti fulani.Hamna mwenye uchungu wa taifa, ndio maana hatujawa na akina Morgan Tsavangirai bado.

Kubaki ndani ya system ya CCM , huku ukisema wewe ni msafi , hali ukijua huwezi kufanya lolote lile, ama sivyo watakukolimba , chifupa n.k....Nape naye yumo humo humo.

Sina maana wahame chama!!! wakijitokeza wawili watatu, waseme tunajivua uanachama wa CCM kwa ni hatujaridhika na jinsi inavyopafom, nchi itataharuki, wananchi wataamka!, nchi itatikisika, lakini watakuwa mashujaa, HAWAPO HAO!!!! tunalala tunaamka tunapiga kelele -UVCCM!!!!!

Hivyo basi usalama pekee ni kuwa mbali na CCM na kurusha makombora ya mbali.Wengi wana CCM, tumewaona wanapiga kelele, na jamii inawatambua , sasa wako kimya, kesho tena wataamka na kupiga kelele.jamii itawaona mashujaa, miaka inaenda , nothing has been done 3 years now, tunaimba CCM na JK, hao mashujaa wako humohumo!!!!

August ni lini unafikiri utatuaminisha kuwa hao waliochaguliwa wanaweza kuleta mabadiliko , kuliko aliyotegemewa kufanya Kikwete aliyechaguliwa kwa 80%????

Kwa nini tusikae chini na kuona kuwa Rais ndiye tatizo?? hivi unapoua nyoka unaangalia mkia??
Kichwa ndio tatizo, kichwa kikielekea kulia mwili wote unafuata hata kama kuna kiungo kilema, kitavutwa tu

Mtu anakaa chini na kuona mabadiliko ya UVCCM ,na kuwa katibu makamba akiondoka basi ndio nchi imeendelea!!!-Kwa namna hii kwa nini magazeti ya udaku yasiwatajirishe akina Shigongo?

Ukishaona jamii inafurahia habari fulani, ambayo imetengenezwa na watawala, ujue jamii hii imechoka, imeonewa imenyanyaswa au imekata tamaa ya kuwa ni jinsi gani watakavyowaondoa watawala, au imekosa mbinu sahihi ya kuwaondoa watawala.Hivyo basi taarifa, habari yeyote ile inayohusu mabadiliko kutoka kwa watawala inawafurahisha, kwani wameshindwa kufanya makubwa.

Sina lengo la kukosoa taarifa wala dataz kama hizi, ila tunapopata dataz hizi, zisitulemaze na kupumzika au kuhema kwa mapumzika, la tujue kuwa kazi iliyopo ni kumuondoa rais, kwa gharama yeyote hata ikilazimu kizazi hiki kuangamia.

let our motto be 'Leave state house JK', akilala, akiamka, akute wimbo huu, akijifanya kufanya anayoyafanya sasa, akute wimbo ni huu huu, kuwa ondoka Kikwete. Akiona tunakuwa excited na matendo yake butu anafurahi na kesho analeta lingine, 2010 hiyi mnampeleka ikulu kama kawa.

Mungu iokoe Tanzania

waberoya
 
Ladslaus Modest,Mpita Njia,

..hivi uhusiano wa Kinana na wale Waarabu wa Loliondo uko vipi?

..halafu inasemekana Kinana ndiyo kiungo kati ya kampeni za CCM za Uraisi na pesa chafu za mafisadi.

Mkuu Joka, ni kweli kuwa Kinana naye ana sehemu yake ya kashfa. Kwa hakika, ukichunguza kila mtu ana sehemu ya kashfa. Kama tukichukulia methali ya samaki akiuoza mmoj... hapo tutakuwa na watu wachache sana wanaofaa kutoka CCM.
Lakini ukimuweka Kinana kwenye mizani, ukipima mabaya na mazuri yake, na uwezo wake wa kurekebisha mambo kwenye matatizo, mimi namuona kuwa mtu ambaye anaweza kutusaidia kutuvusha katika hali hii iliyotuzingira hivi sasa.
Nchi imebanwa na mafisadi kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba Kikwete, kama ulivyomuelezea kuwa anachoangalia yeye ni kuwa na madaraka, anashindwa kabisa kuwadhibiti. Naamini kuwa Kinana ana uwezo na ujasiri wa kuwadhibiti hao. Pia Kinana ni mmoja wa viongozi wachache ninaowafahamu ambao wanaelewa kwa undani maana ya CONSTRUCTIVE CRITICISM. Hawa wengine, kila wanapokoselewa wanaona kuwa hawapedwi
 
Uchaguzi wa wazinzibari kugombea uenyekiti badala ya watu wa bara na wagombea kutoka bara waliomba uenyekiti kupewa nafasi ya umakamu uenyekiti kwa gia ya kuwaadhibu mafisadi inaweza isifanikiwe. Kwa nini nasema hivyo.....

Tunajua sehemu kubwa ya umoja wa vijana ipo Tanzania bara, kwa maana hiyo hawa wagombea kutoka bara(tunaohisi wanakuwa backed na mafisadi) kwa kiasi kikubwa wana influence kubwa kwa wajumbe na viongozi wengi upande wa bara. Kwa maana ya kupewa nafasi ya kugombea umakamu mwenyekiti iwapo mmojawapo atashinda anaweza still akawa na influence na nguvu kubwa kuliko mwenyekiti (mgeni kutoka znz) kwa sababu ya mtandao wa viongozi wa chini waliojijengea. Hii itamaanisha nguvu ya mwenyekiti itakuwa limited na still mafisadi watakuwa still na influence kubwa kulinda mambo yao.

Dawa ilikuwa kukata kila jina kama kweli sababu ilikuwa ni kuwa wanakuwa backed na mafisadi kwa hiyo mwenyekiti wa CCM akahisi kuwa nia ya kusafisha chama haitatimia. Otherwise muono safari bado ni ndefu kwa CCM kama kweli inataka kujisafisha.

Mkuu hapa tupo kwenye wavelength moja. Haiwezekani wawagundue kuwa ni mawakala wa mafisadi halafu wawaondoe kwenye uenyekiti na kuwaweka kwenye makamu mwenyekiti. kama kweli walibaini dhambi yao ya ufisadi walitakuwa kupigwa kibuti moja kwa moja
 
Mpita Njia na Deny_All,

Mmejuaje kwamba CCM wamewaengua hao wagombea kwa sababu ni mafisadi ?

Kina Makamba, Kingunge na party stalwarts wengine wametoka kumsulubisha Nape majuzi hapa kwa madai yake kwamba kuna ufisadi ndani ya UV_CCM. Sasa unadhani kina Makamba hao hao wataenda tena kwenye Central Committee kukubali kwamba kuna ufisadi UV_CCM? Yani wam vindicate Nape ?

Hao wagombea waliofanya ufisadi hao, walifanya ufisadi wakati wana nafasi gani ndani ya UV_CCM ?

Na kama ulivyosema Mpita Njia, kama kweli wameondolewa kwa sababu ya "dhambi yao ya ufisadi" watawapitishaje kwa vyeo vingine vya umakamu?

Tupime vitu kwanza kabla ya kuviamini kwa vile tu mtu fulani kaleta habari zake hapa.
 
Nchi imebanwa na mafisadi kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba Kikwete, kama ulivyomuelezea kuwa anachoangalia yeye ni kuwa na madaraka, anashindwa kabisa kuwadhibiti. Naamini kuwa Kinana ana uwezo na ujasiri wa kuwadhibiti hao. Pia Kinana ni mmoja wa viongozi wachache ninaowafahamu ambao wanaelewa kwa undani maana ya CONSTRUCTIVE CRITICISM. Hawa wengine, kila wanapokoselewa wanaona kuwa hawapedwi

Mkuu Mpitanjia,

Heshima mbele, hapa tupo ukurasa mmoja, na anyways leo is another day tumerudi pale pale kwenye mapambano, against mafisadi. Hatua moja mbele, hatua mbili nyuma ndio siasa za bongo, lakini one day tutakua kama USA na Europe yaai hatua zote mbele!

Jana tumeshinda goli moja against mafisadi, so far tumeshinda magoli mawili kumtoa Lowassa, Msabaha, Karamagi, lilikuwa goli moja, na this one kuondolewa wagombea wa bara goli la pili,

Mafisadi nao wameshinda magoli mawili kwanza ufissadi wao na pili kulifungia Mwanahalisi, so far tuko 2-2, aliyeleta habari ni mimi Mkulu FMES wazee wa radio station ya sauti ya umeme na leo is another day tunasonga mbele na bongo yetu, CCM na viongozi wake tumewachagua sisi wananchi wa Tanzania na bado wana miaka miwili zaidi until then ni watawala wa haki kisheria, hawakujiweka

Na dalili zinaonyesha wazi kwamba watachaguliwa tena, tena kwa kishindo, WHY? Kwa sababu wengi wetu tuna hasira za humu forum tu kwenye internent, lakini sio political Community organizers wala wapiga kura, the best politics we know ni kushindana na waleta habari humu JF that is all, sisi tunaendelea kupigana kwenye battle ground, yaani ground zero na we have to pay the bills pia! Tutaendelea kuzileta habari kama zilivyo wakitaka wateme au wameze shauri yao!

Peace and out!.......... Next!!!!!
 
Mkuu FMES
Mimi ni mchanga sana hapa jamvini JF.Katika mambo yaliyonivutia saaana na kujiunga ni issue unazomwaga hapa.Ni data za nguvu na mvuto.Na siku zote niko interested na thread ambazo huwa unachangia.Heshima mbele sana mkuu and keep onnnnnnnnnnnnn!
 
Mkuu Heshima mbele sana, lakini nakuomba uwe muangalifu sana maana haya maneno uliyoyasema yanaweza kukuletea matatizo makubwa sana, kuwa unaniabudu, unaniogopa, au mimi ni Mungu,

please jaribu kuwasifia zaidi hao ndugu zetu huko upande wa pili kuwa ni magenius, bwa! ha! ha! ha! ha! ha!

Mkuu Icognito, respect bro na tupo ukurasa mmoja uzuri ni kwamba Tanzania ni taifa letu, taifa la mababu zetu, taifa la nyanya zetu, na ni taifa la watoto wetu, kwa hiyo kwetu hapa ni kupigania taifa letu, letu sisi wenyewe, mkuu tupo ukurasa mmoja hapo na respect!

Sasa hivi ninazitafuta dataz za mkutano wa mafisadi juzi usiku, kilichofanyika under acting chairman Nchimbi, baada ya kikao cha kwanza juzi cha CC, ninazo nusu lakini bado sijazithibitisha ukweli wake kwa 100%, nikimazliza kuzi-verify nitazimwaga hapa kama kawa, tena kwa mwendo wa mdundo, stay tuned! Sasa naingia kibaruani later wakuu!

Ubarikiwe Mkuu Icognito, na wembe wetu ni ule ule! Kumkoma nyani mpaka giladi!
 
Sababu tosha ya kulifagilia mbali hili genge la wezi na wasanii kabla taifa halijaangamia zaidi.

Kama tutalifagilia mbali hili genge la wezi na wasanii, je! ni genge lipi la waaminifu ambalo laweza kuingia badala yao? na kama hilo genge la waaminifu likiingia tuna uhakika gani kama halibadilika, kama ambvyo tumeona na kusikia yaliyo tokea Zambia, Liberia, Kenya N.K .........
 
Kama ni kweli, Kinana ni Mtu safi atatusaidia sana CCM.

But c Kinana huyuhuyu aliyetaifisha zile mashine za kufua nguo ambazo zilitolewa kwa ajili ya Hospitali ya mkoa wa Arusha (Mt Meru) akawafungulia ndugu zake Dry cleaner pale Arusha?
 
But c Kinana huyuhuyu aliyetaifisha zile mashine za kufua nguo ambazo zilitolewa kwa ajili ya Hospitali ya mkoa wa Arusha (Mt Meru) akawafungulia ndugu zake Dry cleaner pale Arusha?

Pamoja na kuwa sina uhakika na tuhuma ulizozianisha, lakini ninakuhakikishia kuwa ukimchunguza kwa kina Kinana, utakumbana na kashfa nyingine zaidi ya hizo. lakini, katika wale waliooza, ukitafuta mwenye nafuu kidogo, Kinana anakuwa juu
 
Na dalili zinaonyesha wazi kwamba watachaguliwa tena, tena kwa kishindo, WHY? Kwa sababu wengi wetu tuna hasira za humu forum tu kwenye internent, lakini sio political Community organizers wala wapiga kura, the best politics we know ni kushindana na waleta habari humu JF that is all, sisi tunaendelea kupigana kwenye battle ground, yaani ground zero na we have to pay the bills

Field Marshall,
Kwa hali ilivyo katika nyakati zetu hizi,hali ya uelewa wa umma,hali ya kuishi katika mfumo wa Chama kimoja kwa miaka 30,hali ya kuwa na katiba isiyokidhi maslahi ya taifa kwa enzi hizi na umaskini uliokithiri mimi naungana na wewe kuwa tuanpiga kelele tu.dalili za hawa watawala kuchaguliwa tena kwa kishindo zipo hiyo 2010 na zitaendelea kuwepo kwa karne hii yote.Madhara ya Nyerere ni makubwa kuliko yote ni kututawala kwa fimbo ya Ujamaa,kuhodhi fikra ma kuwafanya watu wengine wakiishi bila kujitambua,na umma ukabaki na fikra zilizodumaa.

Bila kuondoa huu ugonjwa wa fikra zilizodumazwa kwa kubadili mfumo mzima wa utawala ,kuunda katiba mpya na kuzindua akili za umma zilizolala na kudumaa tutakuwa na CCM hadi mwisho wa karne ya 21,na siyo hivi karibuni.Wengine tutakuwa tumeshakufa na Mungu pekee ndiye anayejua huko mbele watabadika lini hawa Watanzania wa leo.Tuendelee kupiga kelele humu nadani ya forum sisi wenyewe,huko nje mmmmhh kazi ni kubwa!
 
Kwanza Kamati kuu si NEC kama unavyobainisha kwenye heading. Lakini, mbona ni kawaida kwa vikao hivyo kufanyika hapo? Hata vinapofanyika Dodoma, huwa vinafanyika kwenye ukumbi wa Tamisemi-hii ni ofisi ya serikali pia.
Nadhani hoja yako inalingana na ya Zitto juzi Bungeni wakati alipombana Pinda kwa ninia anahusisha ziara zake na shughuli za chama

Hata kama wamezoea kufanya katika ofisi za serikali!does it mean for all long they got no place for their meetings!this is too much!There must be separation between party and government activities.State house is no more a mere place for every one to go there and play meaningless games.It must be respected!Even they are used to do it still expiriencine in doing illegal acts doesnt justfy them!
 
Kinana anayepigiwa chepuo ni yupi?.Kinana ninayemfahamu ni fisadi kama mafisadi wengine.Huyu Kinana alidivert msaada wa mashine za kufulia nguo za wagonjwa Mt Meru Hospital akazipeleka kwenye kampuni yake Falcon drycleaner.Miradi yote ya Kinana kaajiri wasomali wenzake wasiojua hata kiswahili.
Kinana anajulikana kwa kufanikisha deal la Loliondo,alilidhalisha jeshi letu wakati huo akiwa waziri wa ulinzi kutumia magari kusafirisha wanyama kwa faida yake binafsi.
Kinana anahusika kwa kiasi kikubwa kuwapatia uraia wakimbizi wa kisomali walioko katika kijiji cha Chogo Handeni.
 
Back
Top Bottom