CCM yafanya maamuzi mazito Kamati Kuu?

CCM yafanya maamuzi mazito Kamati Kuu?

kwanza mkuu FM ES tunashukuru kwa kutupa taarifa ambazo bado zinakuwa chunguni, yani bado motomoto. Na endelea na moyo huohuo, manake habari njema ni ile ipatikanayo mapema.

Kuhusu kutofautiana kimawazo kwa mada zitolewazo. Nadhani kutofautiana kulikuwepo, kupo na kutaendelea kuwepo. Hivyo mkuu sio kila mtu anayetofautiana nawe basi ana nia mbaya. Kumbuka uono wako wewe Mkuu sio sawa na uono wa Mfumwa. Tunaweza wote tunaangalia mbele, kumbe mmoja ana ona km 6, mwingine km 3. Hivyo tuendeleze forum yetu kwa hoja.

Nilitamani kusema kama ulivyosema, ndipo nikakumbuka usemi huu-I disapprove of what you say,but I will defend to the death your right to say it-Wana JF tukikumbushana kama hivi utaendelea kuwa juuuuuu.
----------------
Sema na watu upate kiatu
.
 
haya ndio maneno ya watu wastaarabu.(waungwana)
 
Hili linashangaza sana. Mimi nilifikiri baada ya kushinda uchaguzi na hasa ukizingatia sasa hivi ana matatizo makubwa ya kisiasa, JK angekuwa concilliatiry na kuwa-take on board watu serious kama akina Mkono. Kumbe bado anaendeleza yaleyale ya umtandao? Hivi hajui kwamba umaarufu wake hata katika chama chake umeshuka sana? He must be having a very mediocre team of advicers!

Mkuu Kitila,

I begg to differ, I mean a proven fisadi hata kama ana msimamo namna gani, hawezi kua kiongozi anayetufaa wananchi na atakayemchagua atakwua ni kama yeye yaani fisadi, ni huzuni kwa mtu makini kama wewe kushauri tushushe standards kwa sababu ya hela za ufisadi za kiongozi fisadi kama Mkono.

Kitila tunataka kusafisha taifa letu sio kurudidsha wale wale mafisadi waliokwisha tambuliwa na DR. Slaa, eti kisiasa wana msimamo na hela nyingi za ufisadi, wananchi kama mimi na wewe tunatakiwa kulilia hawa mafisadi wafikishwe kwenye sheria sio kupewa tena uongozi!
 
Nilitamani kusema kama ulivyosema, ndipo nikakumbuka usemi huu-I disapprove of what you say,but I will defend to the death your right to say it-Wana JF tukikumbushana kama hivi utaendelea kuwa juuuuuu.

thanks for your comment, na ni na support unacho sema au kwa kuliona hilo, ila wengine tukiandika hivi, wengine sijui ndio wenye chama au wanajiona kama nchi ni yao au wao wanauchungu saana na nchi kuliko wengine au ndio huluka ya mwanadamu basi wanadai unajifanya genius na blah blah zingine zisizo na maana. Keep it up Bro

haya ndio maneno ya watu wastaarabu.(waungwana)

Taarabu haziwezi kubadilisha msimamo wetu hata siku moja, kwanza tunajiamni sana ndio kwamba tunaingia kwa jina moja tu, halafu hatukubali ushauri njiwa wa kuwa eti mmoja wa mafisadi wa kwenye list ya Dr. Slaa sasa anafaaa kwa sababu ana msimamo huwa hatuna misimamo inayoyumba kiasi hicho kwamba eti one day huyu ni fisadi na ushahidi wazi, na kesho tena anafaaa kwa sababu ana msimamo baada ya kuchota hela zote zile kule BOT, hapana!

Sasa badala ya sisi kulilia afikishwe kwenye sheria, eti ndio kwanza tunalilia huyu fisadi apewe uongozi, eti kutokubaliana na haya mawazo kunatufanya tuimbiwe taarabu za Pemba, hapana msimamo wetu upo very clear kua kiongozi yoyote proven fisadi hafai period, na tutaendelea kuingia kwa jina moja tu na kusimama kidete kwenye hii misimamo yetu!

Ahsante Mkuu!
 
Kuhusu kikao hakijaisha ndio kwanza sasa hivi ninapoandika wanarudi kwenye kumalizia kikao.

Soon nitakuwa na dataz.....!
 
Okay wakuu, the dataz za kikao cha NEC ni kwamba;_

1. Jana NEC iliwapitisha wajumbe wote waliopitishwa na CC kugombea Jumuiya mbali mbali za CCM, lakini kulikuwa n utata mkubwa sana kutoka kwa wajumbe wengi wa NEC hasa wabunge, kuhusu kutolewa kwa jina la Mkono katika kugombea Wazazi na CC.

- Mvutano wa ishu hii ya Mkono, ulisababisha Mwenyekiti kuishia kuahirisha kikao bila makubaliano na kwamba lingejadiliwa tena leo, lakini leo asubuhi sana Mbunge Mkono, alimuandikia barua Mwenyekiti kumuomba kulitoa jina lake kabisa na kwamba lisijadiliwe tena na ameridhika na uamuzi wa kutolewa na CC.

2. Agenda nyingine ya jana ilikuwa ni ubadilishwaji wa system ya kura za maoni katika kugombea nafasi za CCM, hasa ubunge. Wajumbe wengi wametaka mawili either kuongezwa kwa wasimamizi yaani mabalozi wa nyumba kumi kusimamia uchaguzi huo, au wagombea wapewe nafasi ya kuzunguka jimbo zima mapema sana kabla ya uchaguzi kukaribia.

- Hili limepokelewa kama pendekezo na litafanyiwa kazi na kamati za CCM zinazohusika na kupatiwa majibu huko mbele.

3. Kamati maalum ya tathmini ya CCM, imetakiwa kufuatilia kwa makini hoja nzito sana kwamba inaonekana wabunge wengi wa CCM, hawana maeelewano mazuri na wajumbe wa NEC wa majimbo yao au mikoa yao, wajumbe wengi wametaka CCM kulitafutia kwa haraka ufumbuzi tatizo hilo.

- Wengi wa wajumbe wamedai kwamba kama hili halikutatuliwa mapema, litaleta mpasuko mkubwa sana kwenye uchaguzi ujao, na hata kusababisha wagombea wengi wenye uwezo kushindwa kwa mizengwe, na kuhamia upinzani, hili nalo limepokewa na kikao kama pendekezo na litafanyiwa kazi pia.

4. The more dataz ni kwamba wabunge wamemkumbusha tena mwenyekiti wa CCM, kuhusu ujumbe wao waliompa Waziri Mkuu ampelekee, kwenye kiako cha faragha majuzi, ambapo walimtaka amuondoe haraka sana katibu mkuu wa sasa wa CCM mzee Makamba, lakini hakukuwa na jibu la wazi kutoka kwa mwenyekiti, ndani ya kikao!

Now kikao kinaendelea, lakini tukizipata zaidi kwenye kumalizia basi tutaziweka dataz hapa kama kawaida.

Ahsanteni Wakuu!
 
Mkuu Kitila,

I begg to differ, I mean a proven fisadi hata kama ana msimamo namna gani, hawezi kua kiongozi anayetufaa wananchi na atakayemchagua atakwua ni kama yeye yaani fisadi, ni huzuni kwa mtu makini kama wewe kushauri tushushe standards kwa sababu ya hela za ufisadi za kiongozi fisadi kama Mkono.

Kitila tunataka kusafisha taifa letu sio kurudidsha wale wale mafisadi waliokwisha tambuliwa na DR. Slaa, eti kisiasa wana msimamo na hela nyingi za ufisadi, wananchi kama mimi na wewe tunatakiwa kulilia hawa mafisadi wafikishwe kwenye sheria sio kupewa tena uongozi!

Ndio maana mimi sina chama ndugu yangu...Kitila si CHADEMA?
Kazi ipo ndugu yangu..Na ndio maana mimi huwa sipendelei unazi wa vyama...Kwenye hili nashangazwa sana na mwana ccm kuwa against fisadi kuliko hata mwana mpinzani maarufu mwenye kupiga kelele za ufisadi kila kukicha.
Kazi nzuri mkuu FMES na kwa kweli umeipiga sana ccm tafu hapa jamvini, hilo siyo siri kabisa.
Wengine tusiokuwa na vyama kwasasa tunanufaika kwa sana.
 
Kazi nzuri mkuu FMES na kwa kweli umeipiga sana ccm tafu hapa jamvini, hilo siyo siri kabisa.
Wengine tusiokuwa na vyama kwasasa tunanufaika kwa sana.
Kamanda uoni kuwa huu ndio wakati muafaka wa kujiunga na CCM?
 
Mkuu Mushi,

Heshima mbele sana, mimi ni mwananchi mwenye uchungu na taifa langu ya vyama sio muhimu sana kwangu, ninaamini kama raia wa Tanzania ni haki yangu kulilia mabadiliko, ikiwa ni nia njema kwa taifa langu, yes mimi ni mwanachama hai na mkereketwa wa CCM, siwezi kuwazuia wale wote walioamua kufikiri tofauti,

Ninaamini CCM ina viongozi wachache wabovu, wanaohitaji kuondolewa sio kupewa nafasi zingine tena baada ya kuthibitishwa kwua ni wabovu, niaamini katiba yetu ina mapungufu sana inahitaji kurekebishwa kwa sababu ni ya chama kimoja haikuundwa kwa ajili ya siasa za vyama vingi,

Ninasema Tanzania ni taifa langu kama lilivyo lako, ninao uhuru wa kutoa mawazo yangu kama ilivyo kwa wengine wote, kazi ya kusafisha uovu ndani ya uongozi wa taifa letu sio ya mchezo, lakini pole pole inaonekana tunakaribia kufika wkenye ukweli wa ishu.

Ahsante Ndugu yangu
 
Mkuu Mushi,

Heshima mbele sana, mimi ni mwananchi mwenye uchungu na taifa langu ya vyama sio muhimu sana kwangu, ninaamini kama raia wa Tanzania ni haki yangu kulilia mabadiliko, ikiwa ni nia njema wka taifa langu, yes mimi ni mwanachama hai na mkereketwa wa CCM, siwezi kuwazuia wale wote waliaoamua kufikiri tofauti

Ninaamini CCM ina viongozi wachache wabovu, wanaohitaji kuondolewa sio kupewa nafasi zingine tena baada ya kuthibitishwa kwua ni wabovu, niaamini katiba yetu ina mapungufu sana inahitaji kurekebishwa kwa sababu ni ya chama kimoja haikuundwa kwa ajili ya siasa za vyama vingi,

Ninasema Tanzania ni taifa langu kama lilivyo lako, ninao uhuru wa kutoa mawazo yangu kama ilivyo kwa wengine wote, kazi ya kusafisha uovu ndani ya uongozi wa taifa letu sio ya mchezo, lakini pole pole inaonekana tunakaribia kufika wkenye ukweli wa ishu.

Ahsante Ndugu yangu

Safi sana Mkuu lakini CCM ina viongozi wengi wabovu sio wachache ndiyo maana bado kuna matatizo makubwa sana katika kupambana na mafisadi na kuipitia upya mikataba ya uchimbaji wa dhahabu. Kwa mfano angali Meremeta ambayo ililipwa shilingi bilioni 155 wengi ndani ya CCM wameamini kwamba suala hilo linahusu usalama wa Taifa kitu ambachi si kweli bali ni wizi mtupu na cha kushangaza ndani ya CCM inaelekea suala hilo limeshawekwa pembeni.

Angalia mafisadi ambao bado wamekumbatiwa na wanapeta ndani ya chama akina Lowassa, Karamagi, Msabaha, Rostam, Mramba, Chenge, Mkapa na wengineo wengi tu. Kama kweli viongozi mafisadi wangekuwa wachache basi walio wengi wangesimama kidete kuwafukuza wale wote ambao ni mafisadi ili kukisafisha chama na kukirudishia hadhi yake machoni kwa Watanzania, lakini wengi alio ndani ya CCM wanaogopa kuwagusa hao maana wanajua nao wenyewe wana ufisadi wao. Ndiyo maana nasema walio viongozi wengi ndani ya CCM ni mafisadi na hii ndiyo sababu kubwa ya CCM kupoteza credibility yake miongoni mwa Watanzania walio wengi.
 
Kama kweli viongozi mafisadi wangekuwa wachache basi walio wengi wangesimama kidete kuwafukuza wale wote ambao ni mafisadi ili kukisafisha chama na kukirudishia hadhi yake machoni kwa Watanzania, lakini wengi alio ndani ya CCM wanaogopa kuwagusa hao maana wanajua nao wenyewe wana ufisadi wao. Ndiyo maana nasema walio viongozi wengi ndani ya CCM ni mafisadi na hii ndiyo sababu kubwa ya CCM kupoteza credibility yake miongoni mwa Watanzania walio wengi.

Mkuu Bubu,

Heshima mbele bro, hapa unachanganya ishu nyingi sana katika hoja moja, kwa mfano hapa JF tuko wananchi wangapi? Hivi kweli wote tuna msimamo sawa? Unasema kuwa wingi wa wananchi ni lazima uendane na msimamo? Sasa how do you define wananchi millioni 40 wanaoichagua CCM kushika power for the last 45 years?
 
Nadhani majority ya viongozi wa CCM ni mafisadi na ndio maana inakuwa ngumu kukisafisha chama.
 
Sichanganyi issue yoyote. Msimamo wangu ni kwamba ndani ya CCM viongozi wengi ni mafisadi ndiyo maana masuala mengi yaliyogubikwa na ufisadi bado yanaiyumbisha nchi. Masuala hayo ni kama suala la Meremeta kulipwa shilingi 155 billioni kutoka BOT ambalo viongozi wa CCM wanataka kulifanya ni la usalama wa Taifa ili lisijadiliwe na Watanzania, mikataba ya madini ambayo haina maslahi kwa Watanzania pamoja na kuwa Kikwete katika kampeni zake 2005 aliahidi kuiangalia upya mikataba hiyo huu ni mwaka wa tatu sasa ambapo hajafanya lolote. Suala la fisadi Mkapa kujiuzia Kiwira katika mazingira ya kutatanisha tena kwa bei poa kabisa na kisha kuishinikiza TANESCO kusaini mkataba na kampuni yake hiyo wa shilingi 326 billioni hili bado linapigwa danadana.

By the way hii CCM ya kuanzia Mwinyi mpaka Kikwete ina tofauti kubwa na CCM iliyopita wakati wa Nyerere. Kikwete aliahidi ahadi nyingi sana wakati wa kamoeni zake ambazo zilimfanya aingie madarakani kwa ushindi wa kishindo lakini hadi hii leo hakuna hata moja aliyoitekeleza. Kwa kifupi tunaweza kusema aliudanganya umma wa Watanzania umchague akichagua fika hana mpango wa kutimiza hata moja ya ahadi zake. Utakaaje madarakani miaka mitatu ushindwe kutimiza hata moja ya ahadi zako wakati wa kampeni? Kwa mantiki hayo basi kuchaguliwa kwa CCM hasa miaka ya karibuni kuanzia Mkapa ni ukosefu wa mawasiliano kupitia magazeti, radio na TV huko vijijini ambako Watanzania wengi ndiko wanaoishi. Wengi wanajua chama cha kukichagua ni CCM tu na wakishasikia neno 'wapinzani' basi wanawahusisha na machafuko. Hivyo kamwe hatuwezi kusema kuchaguliwa kwa CCM kunaonyesha sera nzuri zozote.

Kama kweli CCM viongozi wabovu na mafisadi wangekuwa wachache basi masuala haya yangepewa kipaumbele na walio wengi ndani ya chama hicho ili yajadiliwe bila woga wala kificho ili yapatiwe ufumbuzi na kama kuna sheria zilipindwa basi wahusika wote wachukuliwe sheria zinazostahili, lakini mpaka leo viongozi mafisadi na wabovu ambao ni wengi ndani ya CCM wanataka kuyazima haya yote kimya kimya.

Sichanganyi issue yoyote. Msimamo wangu ni kwamba ndani ya CCM viongozi wengi ni mafisadi ndiyo maana masuala mengi yaliyogubikwa na ufisadi bado yanaiyumbisha nchi. Masuala hayo ni kama suala la Meremeta kulipwa shilingi 155 billioni kutoka BOT ambalo viongozi wa CCM wanataka kulifanya ni la usalama wa Taifa ili lisijadiliwe na Watanzania, mikataba ya madini ambayo haina maslahi kwa Watanzania pamoja na kuwa Kikwete katika kampeni zake 2005 aliahidi kuiangalia upya mikataba hiyo huu ni mwaka wa tatu sasa ambapo hajafanya lolote. Suala la fisadi Mkapa kujiuzia Kiwira katika mazingira ya kutatanisha tena kwa bei poa kabisa na kisha kuishinikiza TANESCO kusaini mkataba na kampuni yake hiyo wa shilingi 326 billioni hili bado linapigwa danadana.

By the way hii CCM ya kuanzia Mwinyi mpaka Kikwete ina tofauti kubwa na CCM iliyopita wakati wa Nyerere. Kikwete aliahidi ahadi nyingi sana wakati wa kamoeni zake ambazo zilimfanya aingie madarakani kwa ushindi wa kishindo lakini hadi hii leo hakuna hata moja aliyoitekeleza. Kwa kifupi tunaweza kusema aliudanganya umma wa Watanzania umchague akichagua fika hana mpango wa kutimiza hata moja ya ahadi zake. Utakaaje madarakani miaka mitatu ushindwe kutimiza hata moja ya ahadi zako wakati wa kampeni?

Kama kweli CCM viongozi wabovu na mafisadi wangekuwa wachache basi masuala haya yangepewa kipaumbele na walio wengi ndani ya chama hicho ili yajadiliwe bila woga wala kificho ili yapatiwe ufumbuzi na kama kuna sheria zilipindwa basi wahusika wote wachukuliwe sheria zinazostahili, lakini mpaka leo viongozi mafisadi na wabovu ambao ni wengi ndani ya CCM wanataka kuyazima haya yote kimya kimya.

CCM ina viongozi wachache mafisadi, lakini ingekwua na wengi basi Lowassa angekwua bado ni waziri mkuu, Kikwete ana mapungufu ya uongozi ambayo hayana uhusiano wowote na CCM kama chama, mapungufu ya Mwalimu kiuongozi hayakuwa na anything to do na chama in general,

Sio kweli kwamba viongozi wengi wa CCM wanahusika na EPA, sasa kama nia ni kuleta mabadiliko nafikrii ni uamuzi wa Upinzani na Tanzania kufikiri hoja ya kukubalika wka wananchi, kwa sababu sio siri kwamba hii ya CCM nzima kua chama cha mafisadi kama unavyodai siku zote it does not work with wananchi,

Upinzani mtafute another startegies za kuwashawishi wananchi waamue tofauti, lakini kama ndio hoja hii tu basi CCM itatawala milele, maana wananchi sio wajinga kiasi hicho cha kutojkujua kua ni viongozi wachache sana ndani ya CCM ni mafisadi, wengi sio na CCM kama chama sio cha mafisadi, ila kina wananchama wachache tu wanaohitaji kusafishwa, ndio maana kazi inayoendelea ya kuwasafisha mafisadi imeaanza kuleta matunda ingawa sio kwa speed ambayo tungeitaka hapa JF.
 
Nadhani majority ya viongozi wa CCM ni mafisadi na ndio maana inakuwa ngumu kukisafisha chama.

Nafikiri zaidi ya asilimia 95 kuanzia viongozi wa vijiji mpaka kwa JK ni mafisadi. Wanachotofautiana ni kiwango cha kuiba.

Katika viongozi walipo madarakani ni wachache sana ambao unaweza kusema bila kubabaika kwamba ni waadilifu.

Kuna ufisadi wa aina nyingi sana Tanzania. Mwingine umebarikiwa na sheria lakini bado ni morally wrong.
 
CCM ina viongozi wachache mafisadi, lakini ingekwua na wengi basi Lowassa angekwua bado ni waziri mkuu, Kikwete ana mapungufu ya uongozi ambayo hayana uhusiano wowote na CCM kama chama, mapungufu ya Mwalimu kiuongozi hayakuwa na anything to do na chama in general,

Sio kweli kwamba viongozi wengi wa CCM wanahusika na EPA, sasa kama nia ni kuleta mabadiliko nafikrii ni uamuzi wa Upinzani na Tanzania kufikiri hoja ya kukubalika wka wananchi, kwa sababu sio siri kwamba hii ya CCM nzima kua chama cha mafisadi kama unavyodai siku zote it does not work with wananchi,

Upinzani mtafute another startegies za kuwashawishi wananchi waamue tofauti, lakini kama ndio hoja hii tu basi CCM itatawala milele, maana wananchi sio wajinga kiasi hicho cha kutojkujua kua ni viongozi wachache sana ndani ya CCM ni mafisadi, wengi sio na CCM kama chama sio cha mafisadi, ila kina wananchama wachache tu wanaohitaji kusafishwa, ndio maana kazi inayoendelea ya kuwasafisha mafisadi imeaanza kuleta matunda ingawa sio kwa speed ambayo tungeitaka hapa JF.

Kushindwa kwa CCM siyo tu katika kupambana na ufisadi bali pia kuhakikisha rasilimali zetu zinanyanyua viwango vya maisha ya Watanzania walio wengi. Botswana inapata 50% ya mapato ya dhahabu yake wakati sisi tunapata 3% tu na pamoja na fisadi Mkapa kung'ang'ania kuifanya siri mikataba hiyo hakuna hata mmoja ndani ya CCM aliyesimama kidete ili kutetea maslahi ya Tanzania kuhusiana na rasilimali zetu mbali mbali. Kwanini tunashindwa kuhakikisha mikataba tunayosaini ya rasilimali zetu ina maslahi kwa Watanzania badala ya wageni?

Naam Lowassa, Karamagi, Msabaha na Chenge si mawaziri tena lakini bado wanapeta ndani ya CCM na bungeni kwa kukingiwa kifua na CCM. Kama kweli CCM ingekuwa inataka kujisafisha basi hawa wote ilibidi wafukuzwe chama. Haitoshi kuwavua uwaziri wakati bado wanahudhuria vikao vyote vya juu na kufanya maamuzi ndani ya CCM na hali kadhalika ndani ya serikali maana CCM ni chama tawala na mamuzi yake hayaishii CCM tu. Hata Mwalimu leo hii angekuwa hai hii CCM angeikana kata kata na alishaanza kuikosoa kabla ya kufariki kwake.

Wananchi wanaamka taratibu na mfano mzuri ni Tarime. Pamoja na vitisho vya CCM na kuwatumia polisi na FFU kuwapiga wananchi wanaopinga CCM na hata kuwakamata baadhi ya viongozi wa CHADEMA ikiwemo mgombea aliyeshinda uchaguzi huo bado CCM haikupata kitu. Kwa hiyo Watanzania wanafungua machi kidogo kidogo na kama CCM haitaona umuhimu wa kubadilika na kuweka maslahi ya Watanzania mbele badala ya yale ya mafisadi na wageni basi si ajabu itabaki katika vitabu vya history katika muda si mrefu ujao. Sasa hivi wamebaki na sera za kuwatenganisha Watanzania kwa kudai CAHDEMA ni chama cha wachaga wakati hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha hilo.

Mimi si mwanachama wa chama chochote cha upinzani bali ni mtetezi wa maslahi ya Watanzania. Hivyo kama CCM ikiamua kubadilika leo hii na kuweka mbele maslahi ya nchi badala ya mafisadi na wageni sitaona aibu yoyote kusimama mbele ya kadamnasi kuipigia makofi CCM na viongozi wake, lakini mpaka hapo watakapoamua kuyaweka maslahi ya Tanzania mbele nitaendelea kuikosoa CCM kwa makosa mengi inayoyafanya katika kuendesha Tanzania ambayo yanaifanya nchi yetu isipige hatua zozote za kimaendeleo pamoja na kuwa tuna utajiri mkubwa wa rasilimali na pia kuwakumbatia mafisadi ndani ya chama hicho.
 
Katika Uongozi wa nchi yoyote iwe hata ya kidikteta, mafisadi huwa ni watu wachache sana.. Kabla hata ya Utawala wa Roma nguvu ya dola siku zote huwa inashikwa na watu wachache sana..Hivyo sii kweli CCM kuna viongozi wengi Mafisadi, ila hao wachache ndani ya CCM wana nguvu ya juu (internal) ktk Uongozi wa chama..

Nakumbuka hata China ktk mageuzi ya Uchumi wao ilibidi wawakamate na kuwatia hatiani viongozi wa juu wanne tu ktk Utawala alouacha MaoTse Tung..
Na leo hii tunaona mabadiliko makubwa yakiendeshwa na chama kile kile kilichokuwa kikitukanwa dunia nzima..

Tatizo kubwa la kijiwe hiki ni pale tunaposhindwa kutofautisha issue kati ya Ubovu wa Policies and procedures tunatakiwa kukilaumu chama sio uongozi.. Na pale kuna Uongozi mbaya ktk utekelezaji wa Policies nzuri tunakilaumu chama badala ya viongozi..
Pia kuna upande mwingine ambao Policies ni mbovu na viongozi wa juu wabovu vile vile.. jambo ambalo yawezekana ndio wengi wetu wamekuwa wakijaribu kukizungumzia chama CCM... Kwa hiyo hata kama kuna baadhi viongozi wazuri ndani ya chama lakini kwa sababu ya Policies za chama ni mbovu wakiongozwa na viongoizi wabovu inakuwa vigumu watu kutenganisha..

CCM kama chama wanatakiwa kukaa kitako na kutafuta mapungufu yao badala ya kuendelea kujenga ahadi hewa kwa wananchi..Kwa miaka 48 ya Utawala wake, miaka hii michache chini ya 20 imekuwa ikipoteza popularity na sasa hivi imefikia hadi vijijini wananchi kutoweka imani zao juu ya chama hiki....
yawezekana mabadiliko yaliyofanyika ndani ya chama yanaweza kuleta sura mpya, lakini mara nyingi ni vizuri kwanza utafute mapungufu yako kabla hujafanya mabadiliko...
The wound could be deeper than expected!
 
Jamani PUNDIT amechafua hali ya hewa, lakini kapata majibu yake leo. Muda wake umekwisha........
 
Mkandara,

Wakati wa mwalimu nitasema labda policies ndio zilikuwa mbovu pamoja na capacity ndogo ya watendaji. Lakini kilichopo sasa ni culture ya ufisadi ambao imeenea kwenye jamii zetu zote na huko CCM imekomaa.

Kama yalivyo mabadiliko kwenye culture yoyote, zinaweza kutumika nguvu kwa kuwanasa wale vinara wachache na kutoa onyo kali au through kuelemisha jamii mpaka waone umuhimu.

Njia iliyorahisi na haraka ni kutumia bakora.

Hata hao wanaosema wanapinga ufisadi, ukiwafuatilia kidogo tu unakutana na harufu kali ya ufisadi.
 
Back
Top Bottom