Tetesi: CCM yalizwa na CHADEMA uchaguzi mdogo Uyui Tabora

Tetesi: CCM yalizwa na CHADEMA uchaguzi mdogo Uyui Tabora

Hivi hii teknolojia ya kutengeneza picha kama hivi (kuonyesha watu wengi hivi) inapatikana wapi?

Endapo kama ungekuwa ni mzalendo halisi, ungehudhuria mikutano ya vyama ili uone na siyo kupokea maneno ya kujazwa katika kichwa chako ndipo ungejua kama picha zimetengenezwa au ni uhalisia.

Acha maneno ya vijiwe vya kahawa pale chini ya mti mbele ya Shina la Wakereketwa.
 
cocochanel nakusalimia habari za muda huu??
wewe vijiji 12 kati ya 83 unapagawa kihivyo kweli
Uyui wilaya hii tabora huko ndio ngome za CCM. Si unajua maeneo mengi ya vijijini kwenye umasikini sana ndio CCM huwa inashinda uchaguzi? Inavyoonekana wananchi wamechoka Na hiki chama miaka zaidi ya 50 bado watu wana umasikini uliokithiri.
mbona umepotea unahabari ulikuwa unadanganywa? CCM imeshinda tena vibaya pole sana. mchezo huu hauhitaji hasira
 
Tunaombeni matokeo tafadhalini, .... Tunapenda kujua namna alivyoangukia pua
 
Uyui wilaya hii tabora huko ndio ngome za CCM. Si unajua maeneo mengi ya vijijini kwenye umasikini sana ndio CCM huwa inashinda uchaguzi? Inavyoonekana wananchi wamechoka Na hiki chama miaka zaidi ya 50 bado watu wana umasikini uliokithiri.

Kuwa ngome ya CCM hakuna tabu, wamepata mtihani sasa wa kujibadili kwa walipo pungua, wasipotumia akili wanalo mbeleni.

Kabla ya kusema ni masikini, jiulize wananchi wanajaribu kufanyaje walipo kupata kipato kujiendeleza? Je hawana mashamba, hawatafuti kazi, hawalimi yaani wanataka nini? Au unataka serikali iwe inawapatia pesa za matumizi kila wiki au mwezi? Wana viongozi na wanaotaka kupata vyeo huko vijijini kazi ni wao kufanya yanayotakiwa mengi na hao wananchi watakipenda tu chama tawala bila hata kusita. Mengi yapo, tabu viongozi na wapenda vyeo hawana ule ujuzi na hawajiendelezi kujua ya kufanya kukarisha wafuasi kupenda wawaongoze...wengi matumbo mbele na kufikiria mbele sekunde moja au kuwa nyuma dk 5, badala ya kuwa mbele dk 5.

Hao waliochaguliwa nao wana kazi kubwa kwa sababu sasa wapo kwenye mizani ya wananchi, wakipwaya wanalo mbeleni.. njia kuelekea 2020 sio mbaya kupima wengine wakoje katika uongozi na ahadi zao kama watatekeleza na kubadili wananchi wanachotaka kukiona. Kwa hiyo usishangilie kivileeeeee.... kazi mnayo Mr. Chadema. Kawapeni maarifa ya kujipaisha hata mbeleni wapigiwe kura na wengi. Sio mnaishi mitandaoni


Duh!!! nakuandikia gazeti kama vile utanilipa... nasepa bye
 
TUNAOMBENI MATOKEO YA UYUIIIIIIIIII.......

Mbona mmepotea ghafla??????
 
WANYAMWEZI WENZANGU NAO WAMEPELEKA UJUMBE LUMUMBA. TABORA YA LEO SIO YA MWAKA 77.
Matokeo Uchaguzi Mdogo wa Vijiji na Vitongoji wilaya ya Uyui mkoani Tabora 23/4/2017.

CCM Ya pigwa na chadema

1.KITONGOJI CHA NYANGALAMILA CCM 85, CDM 156[emoji818]
2.KITONGOJI CHA NDONO MILUMBANI CCM 15,CDM 32[emoji818]
3.KIJIJI CHA ITOBELA CCM 298, CDM 232
4.KITONGOJI CHA KINAMAGI MIHONGONI CCM 31, CDM 49[emoji818]
5.KIJIJI CHA NDOBA CCM 67, CDM 123[emoji818]
6.KIJIJI CHA MSIMBA CCM 269, CDM 288[emoji818]
7.KITONGIJI CHA ITINKA CCM 8 CDM 22[emoji818]
8.KITONGIJI CHA IBADI CCM 22, CDM 26[emoji818]
9.KITONGIJI CHA NYANGALAMILE-SHITAGE CCM 45, CDM 117[emoji818]
10.KITONGOJI CHA BUKALA CCM 21 CDM 167[emoji818]
11. KITONGOJI CHA SESELA CCM 47, CDM 21
12.KITONGOJI CHA KABUMBULI CCM 81, CDM 5.
13.KITINGOJI CHA IMALAUDUKI CCM 90, CDM 230[emoji818]
14.KITONGOJI CHA IPUMLO CCM 45, CDM 72[emoji818]
15.KITONGOJI CHA UGOWOLA "B" CCM 85, CDM 158.[emoji818]
16.KIJIJI CHA NZUBUKA CCM 195, CDM 502[emoji818]

======

[HASHTAG]#Updates[/HASHTAG] ya [HASHTAG]#Matokeo[/HASHTAG] ya #Uchaguzi_Mdogo wa Vijiji na Vitongoji wilaya ya Uyui mpaka sasa ni kama ifuatavyo...

1.KITONGOJI CHA NYANGALAMILA CCM 85, CDM 156[emoji818]

2.KITONGOJI CHA NDONO MILUMBANI CCM 51,CDM 32

3.KIJIJI CHA ITOBELA CCM 298, CDM 232

4.KITONGOJI CHA KINAMAGI MIHONGONI CCM 31, CDM 49[emoji818]

5.KIJIJI CHA NDOBA CCM 167, CDM 123

6.KIJIJI CHA MSIMBA CCM 269, CDM 288[emoji818]

7.KITONGIJI CHA ITINKA CCM 80, CDM 22

8.KITONGIJI CHA IBADI CCM 22, CDM 26[emoji818]

9.KITONGIJI CHA NYANGALAMILE-SHITAGE CCM 45, CDM 117[emoji818]

10.KITONGOJI CHA BUKALA CCM 217, CDM 167

11. KITONGOJI CHA SESELA CCM 47, CDM 21

12.KITONGOJI CHA KABUMBULI CCM 81, CDM 5.

13.KITINGOJI CHA IMALAUDUKI CCM 90, CDM 23.

14.KITONGOJI CHA IPUMLO CCM 45, CDM 72[emoji818]

15.KITONGOJI CHA UGOWOLA "B" CCM 85, CDM 158.[emoji818]

16.KIJIJI CHA NZUBUKA CCM 195, CDM 155.

17.KITONGOJI. HA MITUNDU - KIZENGI CCM 25, CDM 26[emoji818]

18.KITONGIJI CHA SAIDING CCM 73, CDM 47

19.KITONGOJI CHA MWASUSU CCM 81, CDM 57

20.KIJIJI CHA SONGAMBELE CCM 307, CDM 240

21. KITONGOJI CHA MWAKALOMO CCM 21, CDM 30[emoji818]

22.KITONGOJI CHA 04-MKALYA CCM 90, CDM 61

Tutaendelea kuwaletea matokeo ya kura......

Tunaendelea kuamini [HASHTAG]#watanzania[/HASHTAG] wa leo na #wana_Uyui wa leo si wa Jana hivyo wanaendelea kuungana na kushikamana.

Aluta continua.......

General kaduma.
Katibu chadema kanda ya Magharibi
Mkuu kuna kilaza mmoja katupotosha kuwa ccm ndiyo iliyoshinda
 
Safi sana!

Waendelee tu na viburi na dharau zao wakizani Bombardier na treni ya umeme ndio kila kitu.
Hizo bomberdier mkulima wa karanga debe tatu na gunia 2 za makopa huku kwetu idongalyosi ananufaika nazo kitu gani?
 
Upotoshaji hauwasaidii chochote
Wilaya ya Uyui ilikuwa na Vijiji 15 vyenye Uchaguzi na Vitongoji 58
CCM imeshinda Vijiji 14 kati ya 15
CCM imeshinda Vitongoji 51
Chadema 7
Binafsi nilisimamia Kata ya Ibelamilundi iliyokuwa na vitongoji 6ambavyo vyote vile kwenda CCM

Hahahaha mkuu hutaki wapumue? Waacheni kidogo wajitekenye na kucheka wenyewe.
 
huu upupu unaoendelea utawaliza ccm 2020
wananchi wanaona kinachoendelea
tunaona ugumu wa pesa ilhali kina bashite wao wanauzia magazeti kazi hawafanyi,
tunaona tetenas na dawa nyingine muhimu hakuna mahospitalini
tunaasikia pia matusi ya viongozi wetu wakishika vipaza sauti
tunaona pia wanavyotumia hela zetu kugawa kama njugu bila kufwata sheria
tunaona wimbi la watanzania kukosa ajira
tunaona pia vijana wetu wanaondolewa vyuoni ati ni vilaza
tunaona pia hakuna boom vyuoni
tunaona pia kuwa serikali haina ajira na huku mitaani pia tunaona jinsi mabiashara yanavyofungwa kwa kukosekana mizunguko ya uchumi ...........

pia tunana natunaona watu wanavyotekwa humu na tunaona kina cuf na kina nape na kina nanihii walivyoshikiwa mabunduki

tunwaona majibu mtayapata mubashara kabisaaaaaaaaaaaa
huu ni mwanzo endeleeni kusema wanaolalamika ni wapiga dili wakati wapiga dili ni ccm tuliowapa dhamana ya kutuongozea nchi lakini wao wakaigeuza shamba la bibi yao kama si mzaa mama ni baba
zingatia kanun za uandishi kiongozi.
 
...three dimensions of understanding! Asanteni nyote.
Asante japo sidhani kama umenielewa vizuri ...namaanisha pale picha inapoonyesha watu 20 badala ya 10 waliopo!
Drone camera
Endapo kama ungekuwa ni mzalendo halisi, ungehudhuria mikutano ya vyama ili uone na siyo kupokea maneno ya kujazwa katika kichwa chako ndipo ungejua kama picha zimetengenezwa au ni uhalisia.
Acha maneno ya vijiwe vya kahawa pale chini ya mti mbele ya Shina la Wakereketwa.
 
1544a97e6a64f3c41c37b8aeafe78748.jpg


Ipi taarifa sahihi kati izo mbili??
 
Back
Top Bottom