Tetesi: CCM yalizwa na CHADEMA uchaguzi mdogo Uyui Tabora

Hivi hii teknolojia ya kutengeneza picha kama hivi (kuonyesha watu wengi hivi) inapatikana wapi?

Endapo kama ungekuwa ni mzalendo halisi, ungehudhuria mikutano ya vyama ili uone na siyo kupokea maneno ya kujazwa katika kichwa chako ndipo ungejua kama picha zimetengenezwa au ni uhalisia.

Acha maneno ya vijiwe vya kahawa pale chini ya mti mbele ya Shina la Wakereketwa.
 
cocochanel nakusalimia habari za muda huu??
wewe vijiji 12 kati ya 83 unapagawa kihivyo kweli
Uyui wilaya hii tabora huko ndio ngome za CCM. Si unajua maeneo mengi ya vijijini kwenye umasikini sana ndio CCM huwa inashinda uchaguzi? Inavyoonekana wananchi wamechoka Na hiki chama miaka zaidi ya 50 bado watu wana umasikini uliokithiri.
mbona umepotea unahabari ulikuwa unadanganywa? CCM imeshinda tena vibaya pole sana. mchezo huu hauhitaji hasira
 
Tunaombeni matokeo tafadhalini, .... Tunapenda kujua namna alivyoangukia pua
 
Uyui wilaya hii tabora huko ndio ngome za CCM. Si unajua maeneo mengi ya vijijini kwenye umasikini sana ndio CCM huwa inashinda uchaguzi? Inavyoonekana wananchi wamechoka Na hiki chama miaka zaidi ya 50 bado watu wana umasikini uliokithiri.

Kuwa ngome ya CCM hakuna tabu, wamepata mtihani sasa wa kujibadili kwa walipo pungua, wasipotumia akili wanalo mbeleni.

Kabla ya kusema ni masikini, jiulize wananchi wanajaribu kufanyaje walipo kupata kipato kujiendeleza? Je hawana mashamba, hawatafuti kazi, hawalimi yaani wanataka nini? Au unataka serikali iwe inawapatia pesa za matumizi kila wiki au mwezi? Wana viongozi na wanaotaka kupata vyeo huko vijijini kazi ni wao kufanya yanayotakiwa mengi na hao wananchi watakipenda tu chama tawala bila hata kusita. Mengi yapo, tabu viongozi na wapenda vyeo hawana ule ujuzi na hawajiendelezi kujua ya kufanya kukarisha wafuasi kupenda wawaongoze...wengi matumbo mbele na kufikiria mbele sekunde moja au kuwa nyuma dk 5, badala ya kuwa mbele dk 5.

Hao waliochaguliwa nao wana kazi kubwa kwa sababu sasa wapo kwenye mizani ya wananchi, wakipwaya wanalo mbeleni.. njia kuelekea 2020 sio mbaya kupima wengine wakoje katika uongozi na ahadi zao kama watatekeleza na kubadili wananchi wanachotaka kukiona. Kwa hiyo usishangilie kivileeeeee.... kazi mnayo Mr. Chadema. Kawapeni maarifa ya kujipaisha hata mbeleni wapigiwe kura na wengi. Sio mnaishi mitandaoni


Duh!!! nakuandikia gazeti kama vile utanilipa... nasepa bye
 
Wewe umejuaje kama 2020 JPM atashinda? au ndio nyie mnaonza kuiba matokeo kuanzia sasa?

Kwa hiyo mfano ukiwa na mtihani utajiambia huo mtihani nitafeli au utajipa moyo kuwa utafaulu!?
 
TUNAOMBENI MATOKEO YA UYUIIIIIIIIII.......

Mbona mmepotea ghafla??????
 
Mkuu kuna kilaza mmoja katupotosha kuwa ccm ndiyo iliyoshinda
 
Safi sana!

Waendelee tu na viburi na dharau zao wakizani Bombardier na treni ya umeme ndio kila kitu.
Hizo bomberdier mkulima wa karanga debe tatu na gunia 2 za makopa huku kwetu idongalyosi ananufaika nazo kitu gani?
 

Hahahaha mkuu hutaki wapumue? Waacheni kidogo wajitekenye na kucheka wenyewe.
 
zingatia kanun za uandishi kiongozi.
 
...three dimensions of understanding! Asanteni nyote.
Asante japo sidhani kama umenielewa vizuri ...namaanisha pale picha inapoonyesha watu 20 badala ya 10 waliopo!
Drone camera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…