Irenga
JF-Expert Member
- Dec 14, 2015
- 2,639
- 1,873
Sikua nafahamu hili, So Nchimbi ni mpango maalumu wa Kanisa Katoliki au Ni Coincidence????
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sikua nafahamu hili, So Nchimbi ni mpango maalumu wa Kanisa Katoliki au Ni Coincidence????
Katoliki ni kanisa na pia ni mfumo........wameandaa wengi tuSikua nafahamu hili, So Nchimbi ni mpango maalumu wa Kanisa Katoliki au Ni Coincidence????
Lisu alikua mkorofi na mjuaji sana 🐒Julius Nyerere, rais wa kwanza wa Tanzania, ambaye alipenda kuwa padre, alisoma katika Shule ya White Fathers Missionary school huko Musoma na baadaye kufundisha St. Mary High School. Wakati akisoma, alijihusisha sana na Kanisa na baadaye aliziandika Injili zote 4 kwa mfumo wa mashairi.
Benjamini Mkapa rais wa tatu wa Tanzania, alisoma katika Seminari ya Kigonsera akipenda kuwa padre, lakini aliona aende kwenye masomo mengine ya mambo ya kidunia.
John Magufuli rais wa tano wa Tanzania, alisoma katika Seminari ya Katoke, Biharamulo Kagera, lakini aliondoka kabla ya kumaliza kutokana na changamoto mbalimbali zilizomkumba akiwa shuleni.
Philip Mpango, makamu wa rais wa JMT, naye alikuwa akisoma katika Seminari ya Ujiji na Itaga, Tabora na pia alifikia uamuzi wa kutoendelea na masomo ya upadre.
Na sasa, mgombea mwenza wa CCM Emmanuel Nchimbi ni ex-seminarian katika Seminari Ndogo ya Mitume wa Yesu, Uru mkoani Kilimanjaro.
Wapo viongozi wengi sana nchini waliosoma seminari za Kanisa Katoliki na wametoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi. Hongera kwa Kanisa Katoliki na mtandao wa shule za seminari kwa kuwa viwanda vya kuzalisha viongozi wakubwa katika Taifa letu.
Ni coincidence tu ila ni matunda ya kazi nzuri ya Kanisa kuelimisha watanzania.Sikua nafahamu hili, So Nchimbi ni mpango maalumu wa Kanisa Katoliki au Ni Coincidence????
Yes.Uru ile seminary ilyokua inakua ya kwanza kila mwaka?
Katoliki ni kanisa na pia ni mfumo........wameandaa wengi tu

Hapa ulitumia nini kufikiri ndugu..Shida mkisikia katoliki mnadhani ni hao vatican tu,,,kumbuka hata orthodox nao ni wakatoliki, Afrika ni wazee wa kula na kipofu na Vatican ameshaanza kupoteza influence hasa huku kwa Africa ndo maana hata ukija pale TEC kuna mgawanyiko japo ni wachini chini kuna wale ambao bado ni loyal kwa Papa na kuna wale wanaoliangalia kanisa kwa upande wa kiAfrika,,,,,hio ishu walijaribu Anglikana walitikisa kiberiti majibu yao wakaja kuyapata kwahio kwa sasa hata Vatican kwa ukanda huu wa Afrika wanacheza kwa step kuna kauli walizitoa wakapima upepo wakaona panaelekea kua kama kwa Anglikana wakabadili kauli,, Afrika ikijitenga na vatican ni kama kanisa linakufa kabisa maana kwa sasa waumini wengi wa hilo kanisa ni kutokea Africa na pia hata mapadri wengi ni wa Afrika huko kwao kanisa limekufa ,,na hilo waseminari wanalijua wao ndo wameshikilia mpini kwa sasa kwa upande wa huku na wala sio papa....
...kuna AMECEA ,makao makuu ni Ethiopia muitaliano akikosea step jamaa wakajitenga kama Anglikana litakua pigo kubwa sana kwao maana pia wanauhasama na Ethiopia tokea waliposhindwa kuwatawala na sasa kanisa likihamishia Vatican yake Ethiopia ni pigo kubwa
Haha unataka siasa za kanisa.....waulize ukraine huko wanajua michezo ya papa na orthodox warusi.............na uzuri shina la hii nchi ni la mashariki zaidi kuliko magharibi.....Hapa ulitumia nini kufikiri ndugu..
Kwa Chadema☻☻Kachero alietumika ku neutralize Kambi ya Lowasa 2015 ndio mgombea rasmi wa urais Mwaka huu!
Linaonekana wazi kabisa!ikishindikana Mwinyi ata step up na eye kubaki makam!!
Aliepitishwa asili imemkataa na nyakati pia!
Wametoa mchango mkubwa wa kusababisha nchi yenye maliasili nyingi iwe na masikini wengi miaka zaidi ya 60 baada ya uhuru.Nyerere, Mkapa, Magufuli, Mpango na Nchimbi ni baadhi yao.
Julius Nyerere, rais wa kwanza wa Tanzania, ambaye alipenda kuwa padre, alisoma katika Shule ya White Fathers Missionary school huko Musoma na baadaye kufundisha St. Mary High School. Wakati akisoma, alijihusisha sana na Kanisa na baadaye aliziandika Injili zote 4 kwa mfumo wa mashairi.
Benjamini Mkapa rais wa tatu wa Tanzania, alisoma katika Seminari ya Kigonsera, Ndanda akipenda kuwa padre, lakini aliona aende kwenye masomo mengine ya mambo ya kidunia.
John Magufuli rais wa tano wa Tanzania, alisoma katika Seminari ya Katoke, Biharamulo Kagera, lakini aliondoka kabla ya kumaliza kutokana na changamoto mbalimbali zilizomkumba akiwa shuleni.
Philip Mpango, makamu wa rais wa JMT, naye alikuwa akisoma katika Seminari ya Ujiji na Itaga, Tabora na pia alifikia uamuzi wa kutoendelea na masomo ya upadre.
Na sasa, mgombea mwenza wa CCM Emmanuel Nchimbi ni ex-seminarian katika Seminari Ndogo ya Mitume wa Yesu, Uru mkoani Kilimanjaro.
Wapo viongozi wengi sana nchini waliosoma seminari za Kanisa Katoliki na wametoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi. Hongera kwa Kanisa Katoliki na mtandao wa shule za seminari kwa kuwa viwanda vya kuzalisha viongozi wakubwa katika Taifa letu.
Ni bora kuliko Somalia na Sudan.Wametoa mchango mkubwa wa kusababisha nchi yenye maliasili nyingi iwe na masikini wengi miaka zaidi ya 60 baada ya uhuru.