CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

Leo imetoka taarifa ambayo imewashtua watu wengi ya kufukuzwa kwa mwanachama nguli wa ccm mh bernard camilius member kutoka kwenye chama chake cha ccm akituhumiwa kwa makosa ya maadili..hili jamabo nililitegemea hasa tukielekea kwenye uchaguzi wa october.kwangu mimi nimenusa hataribya mtego uliotegwa na ccm kwa chadema kama wasipojinasua wakaingia kichwa kichwa wameliwa mazima na watabaki historia

Kama chadema wataamua kurudia kosa la 2015 na kumchukua member hakika atapata umaarufu mkubwa then atawaletea kiasi fulani cha mtaji wa kisiasa hata sehemu ya kusini ambaye yeye ndo prominent politicina ,na maeneo mengine ambako kuna ccm asili inayooneka kutengwa kwa siku za karibuni.lakini madhara yake ya takuwa makubwa sana huko mbeleni

Kama member ataamua kwenda ACT litakuwa pigo kubwa kwa chadema lakini ahuheni kwa ccm,ACT kitakuwa chama kikubwa cha upinzani ambacho kitaleta ushindani mkubwa kwa chadema na kuzigawa kura upinzani,lakini ni bora chadema kubaki na wanacham wake loyal ambao na amini watakuwa na impact kiasi kuliko kutema bigiji kwa karanga za kuonjeshwa!ushauri wangu

Chadema wakae mbali na membe kam ukoma kama kweli wanataka ku sustain after october 2020 tuko kwenye kipindi kigumu cha siasa ambacho ccm wamechokwa kila idara ila watatumia kila mbinu hata kama ni kimfukuza uwanachama Raisi mstaafu ili upinzani uingie kwenyw mtego ni bora kutumia silaha ulizozizoe kuliko kukodi silaha ambayo itakuletea madhara!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo madhara ya kofia mbili,ANC waliyaona haya mwafrika yeyeto bila kumuwekea mfumo wa kumdhibiti ni lazima ataumiza wenzie.

Ni kawaida kwa mwanadamu yeyote asipodhibitiwa hata magharibi wana mifumo ambayo ni advanced sana ya kudhibiti kuliko hata ya Muafrika.
 
Ni ushamba tu wa Watanzania kuona baadhi ya figures kubwa zikihama chama kimoja kwenda kingine, eti kwa kusema kwamba ni kinyume na msimamo! Nchi nyingine ni jambo la kawaida kabisa, wala haishangazi hata aliyehama akirudi tena alikotoka.

Siasa ni mchezo wa maslahi mafupi mafupi. Mwanasiasa fulani anaweza akawa na maslahi na chama fulani kwa wakati fulani tu. Vivyo hivyo, chama fulani kinaweza kikawa na maslahi na mwanasiasa fulani kwa wakati fulani tu. Ni jambo la kawaida kabisa. Maslahi yakiisha au yasipotimia, wanaachana na linafanyika jaribio lingine.

Huku Tanzania tunalazimisha eti uasili, kwamba mtu akihamia kutoka upande tofauti anaanza kutazamwa kwa tahadhari! Hakuna cha tahadhari, kama anawafaa anapewa, kama kinamfaa anahamia, baada ya miaka mitano hata wakiachana haitakiwi kuwa habari ya mjini.
 
Kilichomponza membe ni kutaka kuonja sumu,makamba,nape,kinana wamesamehewa sababu hawana mpango wa kugombea nafasi yeyeto ya juu ni just kuulinda tu biashara zao
 
MLALAMIKAJI ANAONGOZA KIKAO CHA KUAMUA KUHUSU WALALAMIKAJI. HAPO INAKAAJE? HAKI ITATENDEKA? HAJI MANARA ANAKUWA REFARII KWENYE MECHI YA YANGA NA SIMBA, MWEEEEE
Ni lini ulisikia amelalamika mkuu? Yeye alishasema angetaka angewashtaki kamati kuu ila anaacha yapite. Chama kikaamua kuchukua hatua. Halafu mambo ya CCM waachie wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom