CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

Safi sana.

Maamuzi mazuri kwa ajili ya mustakabali wa chama maana kuna watu walionekana untouchable
 
Jamani si nilisikia sheria mpya ya vyama vya siasa ni kuwa kama haujafikisha mwaka mmoja kwenye chama cha siasa hauna nguvu ya kugombea au ilikuwa sio ivyo tena

Sent using komputa mpakato
 
Sasa kesi ya msikiti inaanza upyaaaa na mengine mengi yatatafutwa! Membe awe makini hii ni afrika zaidi hii ni Tz zaidi sana hii ndo awamu ya tano.

Maisha ni magumu na mabaya mmno, wafanyakazi njaa Kali,biashara nishida,kilimo kimedororeshwa elimu ni yakutumia ubabe ziro zipotee bila kuboresha process siasa za ubabe haki hats ya kuongea inakandamizwa!!!

Tumeichoka awamu hii yatano inayotaka kusujudiwa na kusifiwa tuu. Aibu sana
 
Hakuna mwana ccm yeyote sasa hivi ambaye ni popular nchini ni watu ambao wamekaa kimaslahi zaidi.

Membe sio popular na pia hana mvuto wowote kisiasa na ndio maana hata ccm hawakupata shida kumfukuza na wanajua vizuri kuwa hata aende chama gani kwenda kwake huko hakutakuwa na any political consequence itakayoweza kukiathiri ccm.
 
Kwani chadema imeathirika nini kwa kuondokewa na akina Lowasa? Sumaye ? Na wengine? Cha msingi hapo ni kuangalia NET EFFECT.... Impact assessment ifanyike then maamuzi yanaweza kufanyika . Cha msingi chadema iangalie salio kama lipo ama halipo kabla ya kuja akina Lowasa na kuondoka kwao... Je salio linasoma ngapi ?
 
Wasipousikia ushauri wako mtoa maada wasianze kutafutana baadae.. chadema kuna majembe ya kutosha kabisa kugombea urais na wakapata kura yangu..
Membe acha azikane na Ccm wenzake.
 
Ni lini ulisikia amelalamika mkuu? Yeye alishasema angetaka angewashtaki kamati kuu ila anaacha yapite. Chama kikaamua kuchukua hatua. Halafu mambo ya CCM waachie wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kosa la Membe ni kutaka kuchuwana na Magufuli ndani ya chama. Adhabu kama hiyo alipewa shibuda alipo nuwia kuchuwana na JK. Conclusion ni kuwa mwenyekiti wa chama hapingwi ndani ya CCM.
 
Yudatade Edesi Shayo,
Kama ni mtego kwa chadema kama ilivyokuwa kwa lowasa na nikifikiria ufanis mkubwa waliopata chadema kwa ujio wa lowasa na wing wa wabunge waliopatikana na kuomgeza ruzuku bas huu mtego una manufaa sana kwa chadema yenyew.

Tukubaliane tu kwa ihalisia CCM huwez kuitoa madarakan had sheria kadhaa zibadilishwe na tuwe na vyama halis vya upinzan. Tuko bado kwenye siasa ajira. Hatuna mbadala wa CCM. kinachobak ni chama kimoja kimoja kudaka wing wa kura si kuongoza serikali
 
Haijalishi Membe ataenda chama kipi cha upinzani, athari kwa CCM ni negligible!

Ila akihamia ACT upepo wa siasa za upinzani nchini lazima uathirike!
Ndiko atakoenda huko, mpaka sasa ACT hawana presidential material kwa upande wa bara, hivyo nafasi ipo wazi kwake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom