Alwatan Mabruki
Senior Member
- Sep 20, 2020
- 132
- 116
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa siri kuhusu wagombea wake kutoenguliwa na Tume ya Uchaguzi kwenye uchaguzi huu mkuu kwa kigezo cha kishindwa kujaza fomu. Aliyefichua siri hiyo alikuwa ni katibu mkuu wa chama hicho Dkt. Bashiru Ally, katika mahojiano na shirika la utangazaji la BBC, kuhusiana na mambo mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu. Katibu mkuu alijibu kuwa si swala la mbinu kwenye kufanya wagombea wa chama hicho kutoenguliwa na Tume bali ni swala la kufata sheria na kanuni.
Dkt. Bashiru alisema kwa upande wa CCM vitengo vya sheria vinavyosimamia na kuruhusu wagombea wa ngazi zote kujaza fomu na kisha kuhakikiwa na hali hiyo imefanya wagombea wa Ubunge 28 wa CCM wapite bila kupingwa na wanasubiri kuapishwa.