CCM yatangaza kuachana na siasa za kibabe na kurudi kwenye siasa zake za asili za Upendo na Urafiki mwema!

SHIDA nikwamba upinzani ili waone wametendewa haki wao wanajuwa kuwa lazima washinde hata kama hawana ushawishi kwa raia
Kinachotakiwa ni TUME HURU ya uchaguzi, hayo mengine ni njozi zako za kichawi.
 
kwa hiyo wale wanachama tuliojitune kwenye ubabe tuhame chama?
 
Lini ilitangaza kuanza rasmi siasa za kibabe, chuki na uadui mpaka sasa (leo) itangaze kuacha rasmi?!!
.............Nadhani ungeiweka kuwa kwa tamko hili inakiri kuwa na siasa za kibabe, chuki na uadui na sasa inaamua kuachana nayo.

Hatuwapongezi wala nini........................ Walipaswa tu (kwa msemo wa Mh. Mwanri)...Sukuma ndani tu.........
 
CCM ya Mshikamano ndiyo tunayafahamu.
Namkumbuka sana Mfaume Rashid Makame na matembezi ya mashikamano!
 
Imerudi kama zamani hasa nasikia lugumi kapewa tenda ya jeshi na jeshi ni sekta nyeti haijdiliwi,na kweli imerudi ngoja tuone.
 

Kwani ubabe ndani ya ccm huwa unaletwa na chama, ama kiongozi na genge lake wanaokuwa madarakani? Akitokea kiongozi mwingine mwenye kiburi cha madaraka kama Magufuli, ccm hawana uwezo wowote wa kumdhibiti zaidi ya kufuata atakacho. Saa hii ccm wanafuata tabia ya mama Samia, na sio wao kama chama wameamua.
 
Wanakumbuka jinsi walivyofika kwenye siasa za visasi na ubabe?, Kama hawakumbuki basi kurudi ni sekunde. Awekeze ktk namna ya kudhibiti sababu zinazo wapeleka huko.
 
Hawa siawaamini Yaan
Ukiwaambia Mchakato wa Katiba mpya urejee Mezan hawataki
Yaan hawa kazi kutubrush tu kama Viatu vilivyoisha
Je TUME hii haiaminiki sisi tunaaminije maneno ya mdomoni tu
Naver again naver
 
Magufuli aliiua CCM na kubakisha genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala
 
We bwege tokea lini mkaacha ubabe na wizi wa kura?
 
Ubabe walikuwa wanamfanyia nani na kwa ulazima gani hadi wafikie huko na kwanini hawakutaka kufuata utaratibu wa kikanuni na sheria elekezi !?
Wanachotaka kusema ni kuwa kuna shetani aliwaingiza huko.

WanaCCM, wanaCHADEMA wenye mapenzi mema, wanaACT, wasio na vyama, watanzania wote wenye mapenzi mema, tushirikiane, tushinikize kupata katiba bora mpya kwa ustawi wa Taifa letu.

Katiba mpya italihakikishia Taifa kutokuangukia tena kwenye utawala dhalimu.
 
Huyo katibu mkuu uwezo wake wa elimu ya siasa na uchumi ni mdogo. Hajui chama chake ni cha mapinduzi na kipo kupigania matabaka ya chini kupata maendeleo na sio kudolola kwa kunyonywa na tabaka la kinyonyaji. Katika hali hiyo hali ni ya mapambano ya kitabaka.
 
Elimu yako ya kukariri sidhani kama itakuwa na msaada hata kwa familia yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…