CCM yatoa Baraka zote kwa DP World kufanya uwekezaji wa Bandari

CCM yatoa Baraka zote kwa DP World kufanya uwekezaji wa Bandari

Sidhani kama kuna aliyetegemea maamuzi tofauti kutoka kwenye hicho kikao. Ccm siyo ANC ya S/Africa ambayo ina uwezo wa kumng'oa Rais tofauti na ccm. Kumbuka sakata la Ndugai walivyomfanya pale Mwenyekiti wao,alipompomsimanga.
Hakuna aliyesimama na Ndugai.
Hili suala la bandari ni la moto hata wenyewe wanajua,lakini watamfanya nini Mwenyekiti wao?
Eti wawaelimishe wananchi kwa kutumia kina Kitenge na genge lake!!
 
Nimesoma mara kadhaa Sijui alimaanisha nini
IMG-20230709-WA0051.jpg
 
Sasa nimeanza kuelewa kilichosababisha mwaka 1964 zanzibar kumla kichwa yule bwana mkubwa.
 
Wewe kwani unadhani ni hela ya wapi iliyomfanya Huyo mama yako akashusha tu signature bila kufikiria….
Unapuyanga tu naona hujielewi. nimekuuliza swali bandari imeuzwa Tsh ngapi? Unanijibu trillion kadhaa kila mwaka, kila mwaka itakua inauzwa kwa trillion kadhaa ndio bei ya wapi? Huna jibu. Chuki kitu kibaya sana
 
1688930121996.png


Katika mkutano huo na waandishi, Sophia Mjema amesema leo 9 July 2023 siyo siku ya kujibu maswali kwani yeye amesoma kile ambacho wamekubaliana na Halmashauri na mambo mengine yasubiri wakati wake
 
Unapuyanga tu naona hujielewi. nimekuuliza swali bandari imeuzwa Tsh ngapi? Unanijibu trillion kadhaa kila mwaka, kila mwaka itakua inauzwa kwa trillion kadhaa ndio bei ya wapi? Huna jibu. Chuki kitu kibaya sana
Hata mimi nakuona unapuyanga kama huoni hio hela itakayokua inaingia kila mwaka ndio thamani ya bandari yetu then siwezi kukusaidia, chuki anayo Rais kwa watanganyika au hujui hilo?!
 
Hata mimi nakuona unapuyanga kama huoni hio hela itakayokua inaingia kila mwaka ndio thamani ya bandari yetu then siwezi kukusaidia, chuki anayo Rais kwa watanganyika au hujui hilo?!
Wewe hiyo hela itakayokuwa inaingia kila mwaka umeiona wapi? Ni shilingi ngapi?
 
Ambacho hawashtuki hii CCM iliyokaa hapo, ipo tofauti kabisa na CCM iliyopo nje, yaani kuna malalamiko makubwa sana kiufupi wanajitafuna wenyewe, wakija kushtuka itakuwa too late sana
 
Piga Ua.
IGA yenyewe imedai makubaliano hayo yawe yameridhiwa na vyombo vya juu vya nchi vinavyotoa ridhaa za uwekezaji Nchini...ikiwepo Bunge. Vilevile na Chama kilicho na hatamu...

Bunge letu lina Wabunge wa CCM na ni dhahiri wakati wanapitia yale walikuwa hawana Taarifa kamili, yaani vielelezo vya kutosha! Ikiwa ina maana Chama hakikukaa kama chama kujadili, kuchatua, kumega kukataa au kukubali mkataba huo na kuzua sintofahamu kwa baadhi ya walipopelekewa (nyaraka) ad-hoc Wabunge bungeni....ati leo hii ndio wamefanya hivyo? After the Fact? Halafu waseme iko sambamba na 59-92 ya Ilani ya Chama....Who cares


Suala hili limewashindwa CCM(wenzangu). Na tulipofikia ni kukaa pembeni kutafakari na kujitathmini. Na wakati tunafanya hivyo...Kiongozi yeyote yule anayeweza kuongoza Nchi wa Chama chechote kile cha siasa apigiwe Kura ya Ndio tuondoke madarakani kwani ni dhahiri tumeshindwa.
 
Nyie ni wajinga tu hoja zenu ni zile zile, mukiulizwa huo mkataba wa kupewa bandari zote uko wapi mna kenua tu meno, chuki mbaya sana ndo inao wasumbua.
Je ni kweli serikali haijaingia mkataba wowote na DPWorld? nisaidie kwa hilo.
 
Back
Top Bottom