Elections 2010 CCM yatoa tamko kuhusu kitendo cha wabunge wa CHADEMA

Nasikia Chadema nao wanampango wa kuwafukuza wabunge wa CCM kwa kuzomea bungeni wamevunja kifungu cha kumi cha katiba ya Chadema hii ndiyo TZ bwana ukisikia nyingine ni ya uongo ndio maana kina RA hawataki kuondoka.
 
nitafurahi sana kama hao vilaza wa CCM watafanya kama huyu, mdaku wao alivyoeleza maana nitakuwa wa kwanza kwenda kumwagia ya upupu nami kutoa chongo askari mmoja kwa manati. Anafikiri Tundu Lissu, Mbowe, Mnyika et al wametoka wasijue what to do the next if CCM waki-react whatever?
 

Usichoelewa ni kwamba, CHADEMA hawamtambui Kikwete kwa sababu hakupewa madaraka yale kwa mujibu wa Katiba. Wao wameapa kuilinda katiba, na kwa kuwa katiba hiyo ilivunjwa wakati wa kumsimika Kikwete, basi hawamtambui Kikwete kama rais. Iwapo Kikwete angesimikwa kwa kufuata Katiba kuwa watu walipiga kura, zikahesabiwa sawasawa na kujumlishwa bila makosa, basi tatizo hili lisingekuwapo.
 
Kwani hao CHADEMA wameikosea CCM?
Huyo Chuligati anahusika nini na mambo ya wabunge, au yeye ni kibaraka wa Makinda?
Naona Chiligati afunge domo lake haraka, mambo hayo hayamuhusu!!!!
:embarrassed:
 
kilichofanyika jana ni kwa manufaa ya Chadema si wananchi walio watuma. Loud and clear

Umejuaje? Au na wewe sasa watunga riwaya yako............upendavyo...................
 
kwa nini chadema haikupata wabunge zaidi ya 100. Wabunge kiduchu kilele nyingi. Hawana adabu. Dhara kubwa. Eti wanatambua serikali lakini si matokeo. Kwa nini walitoka badala ya kueleza hoja yao kwa njia nyingine. Badala ya kuchezea chombo kikubwa kama bunge. Wachochezi wakubwa . Chadema has a devil sipirit.
 
Kwani hao CHADEMA wameikosea CCM?
Huyo Chuligati anahusika nini na mambo ya wabunge, au yeye ni kibaraka wa Makinda?
Naona Chiligati afunge domo lake haraka, mambo hayo hayamuhusu!!!!
:embarrassed:

Labda chiligati ni kiongozi wa wabunge wa CCM
 


Ni wanasiasa uchwara kama huyu ndio wanaopayuka bila kutafakari. Sishangai kutochaguliwa na wapigakura wake... wamesema HAPANA, PUMZIKA BABA! Bora apumzike tu sasa! Akili hizo za Mbayuwayu wala hana!

Wafukuzwe bungeni kwa mamlaka ya nani? Kwa kukiuka kipengele gani cha Katiba?
 
Nasikia Chadema nao wanampango wa kuwafukuza wabunge wa CCM kwa kuzomea bungeni wamevunja kifungu cha kumi cha katiba ya Chadema hii ndiyo TZ bwana ukisikia nyingine ni ya uongo ndio maana kina RA hawataki kuondoka.

Mkuu hapa umeniacha hoi kabisa....:laugh:
 
Kama mambo ni rahisi hivyo basi CCM wawafukuze Chadema. Hivi ndugu yangu umeshawahi kuisoma list ya watu wanaitwa martyrs? CCM wakifanya hivyo watashangaa jinsi matokeo ya kitendo hicho yatakavyokuwa. Sometimes kutishiana huwa hakuna mpango. Ni muhimu kufanya unalosema ili watu wajue how serious you are.
 

Huna akili weweee, CHADEMA wao HAWAMTAMBUI RAIS kutokana na Kuingia madarakani Kwa wizi!!! Hawajasema hawawatambui wabunge!! Ujue unatakiwa kuwa na akili, ufikilie ndo upost kitu, SIO KUPOST TUUUU uonekane.

Kama HUNA HOJA, ni bora kukaa kimya utaheshimika kuliko kuwa kama Makamba....
Na kama HAWAMTAMBUI MBUNGE YEYOTE WATAENDA MAHAKAMANI, vipi KUHUSU HUYO KILAZA Mwenzenu MWENYEKITI?

Bunge ni muhimili unaojitegemea na RAISI akiingia ndani SIO SEHEMU YA BUNGE kilaza wewe, bungeni huyo kilaza mwenzenu anawakilishwa na Pinda, kwa hiyo hata kuingia kwake inabidi vifungu fulani vitenguliwe na mwanasheria mkuu ili aingie kwa kuwasilisha hoja Kilaza wewe.

Na kwa taarifa yako siku za usoni watatoka hata wabunge wa CCM, shukulu tu jana alikuwa bado hajatangaza Baraza la mawaziri ndo maana unaona Wabunge wa CCM walijifanya wanyenyekevu wakisubili kuteuliwa, subili wakishaona hawana chao ndo utajua, MTAGEUKANA WENYEWE

CCM mkubwa we!!!!
 

hahaaa yaani bonge la uppercut maana amepigwa ngumi mapaka udenda umeruka kwa washabiki...hahaaaaa
 

Nimewahi kulisema hapa. Asante kwa kulitilia msisitizo
 
Du!
 
Endelea kuungana na wanaoisapoti Chaka Chua Matokeo. Ni haki yako hapa JF. Acha na wasio kwenye chama chako watoe maoni yao hata kama yanakuumiza.
kwa kumalizia Soma signature yangu.
 
  1. Kwanza CHADEMA kina wanasheria waliobobea kwenye nyanja ya Laws,kwa uchache tu wapo Mabere Marando na Tundu Lissu. Hivi wanafikiri hii miamba ya LAWS inaweza kukurupuka tu kama CCM ambavyo huwa wanakurupuka? CHADEMA knows what they are doing! CCM sahauni kufukuza Mbunge hata mmoja wa CHADEMA. CHADEMA wametumia haki yao Kikatiba kutoa mawazo yao kwa kutoka nje ya Bunge kuonyesha kuwa hawakubaliani na Wizi wa Kura na ukiukwaji wa taratibu za Uchaguzi uliofanywa na NEC.
  2. Pili Chiligati atuambie ni KIFUNGU GANI CHA KANUNI ZA BUNGE KILICHOVUNJWA AU KIFUNGU KIPI CHA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO KILICHOVUNJWA na Waheshimiwa Wabunge wa CHADEMA. Otherwise ni bla bla za CHAMA CHA MAFISADI-CCM. Naona CCM bado mnaota ndoto za mfumo wa chama kimoja!
  3. Tatu kinachotakiwa kwa CCM kwa sasa ni kuanza kufikiria namna ya kukaa chini wao wenyewe na Mwenyekiti wao Kiwete(Rais wa watu 5 milioni kati ya Watanzania 45 milioni) ili kumaliza kadhia ya mgogoro uliojitokeza wakati wa Uchaguzi wa mwaka huu. Lazima CCM waanze kufikiria kuwa sasa Watanzania tunataka KATIBA MPYA na si vinginevo.
  4. Nne kwa vile Chiligati anajiita Captain wa Jeshi asifikiri anaweza kuwatisha CHADEMA?????Kama CCM wana ubavu huo mbona hawakufukaza CUF walipokuwa wanasusia vikao vya Baraza la Wawakilishi? Iweje lae wanataka kuikomalia CHADEMA?
CCM hebu badilikeni. Acheni udikteta hapa.
 
Bunge ni taasisi inayojitegemea nje ya taasisi ya Uraisi.......hivyo hakuna mahali ambapo wabunge wanawajibika kwa Raisi...........hata kiapo chao cha utii ni kwa Katiba na wala siyo kwa Raisi..............tatizo la CCM ni mkusanyiko wa mambumbumbu tu na hii miaka mitano ijayo wajiandae kujifunga kibwebwe....kutakuwa na upinzani dhidi yao ndani na nje ya Bunge........................dhuluma ya CCM kwa mpigakura haiwezi ikavumilika hata kidogo
 
Kwani kuchakachua iko ndani ya katiba?? Issue hapa ni kuchakachua kulikomuweka madarakani ndio cha msingi sio serikali. Acha majibu rahisi kwa maswali mazito ndugu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…