Elections 2010 CCM yatoa tamko kuhusu kitendo cha wabunge wa CHADEMA

Elections 2010 CCM yatoa tamko kuhusu kitendo cha wabunge wa CHADEMA

Hakuna kitu kama hicho..
Pia Chadema naiamini kwa kubeba wanasheria makini..
 
Inanikumbusha enzi zile tukitaka kugoma shuleni, tunatishiwa kufukuzwa na wakati haki tunayo. Leo ndo nashtukia kumbe ilikuwa system ya ccm kutupandikiza nidhamu ya woga. CHADEMA kaza buti babake...!
 
CCM ni chama sio watanzania, watu ndio power; so hakuna kuogopa, hawana lolote kwani wnageacha kuloloma?
 
Usichoelewa ni kwamba, CHADEMA hawamtambui Kikwete kwa sababu hakupewa madaraka yale kwa mujibu wa Katiba. Wao wameapa kuilinda katiba, na kwa kuwa katiba hiyo ilivunjwa wakati wa kumsimika Kikwete, basi hawamtambui Kikwete kama rais. Iwapo Kikwete angesimikwa kwa kufuata Katiba kuwa watu walipiga kura, zikahesabiwa sawasawa na kujumlishwa bila makosa, basi tatizo hili lisingekuwapo.

Hapa umesema the 'ideal substance!' katiba ni tukufu...kama CDM waliapa kuilinda, hawa wahuni na wachakachuaji wanaoingia madarakani kwa kuifisadi katiba, sio tu wabunge wa chadema kuwakataa, bali watanzania wote wawapinge hata waendapo ktk ziara zao mikoani...hakuna tena woga kwa haki ya kila mtanzania. pamoja daima, bila dhuluma.
 
Nawashangaa watu wana deal na matamshi sijui ya chiligati, hee wake up comrades, hamna issue ya kujadili wa kujitetea hapo, wewe una dhahabu anatokea m2 anakuambia hiyo si dhahabu ni chupa tu nipe mimi nikupe dhahabu(tubadirishane) na kumbe ndo ukapewa chupa haswaa (by baba wa taifa). Kama chiligati ana uwezo huo aendelee na kitakachotokea sisi hatumwambii in advance! Chadema hiyo ilikuwa day 2, sasa tunatakiwa tuingie day 3 na day 4 na kuendelea ya harakati. Ccm ni kama mashetani fulani ambayo yamezoea kutenda maovu mbalimbali.
 
sidhani kama mtu mwenye akili timamu anaweza kutoa tamko kama hilo
 
Maalim Seif nae anadiriki kuilaumu CHADEMA. Je Maalim Seif yupo tayari kubeba damu ya watu waliouawa zanzibar kwa ajili ya kudai demokrasia? Leo hii maalim ni CCM, kina Chiligati wapo wengi
 
We ni kada wa cccm
Tusijidanganye. CCM know what they are talking about.
Itakuwa vigumu kwa wabunge wa Chadema kufanya kazi bungeni iwapo chama chao hakiitambui serikali inayotawala.
Cha ajabu ni kwamba walishaapa kuilinda katiba ambayo ndiyo iliyomweka Rais wasiyemtambua madarakani.
Motion inayopelekwa na CCM itapita na wabunge watafukuzwa bungeni. Take my word.

Mnaojiita wasomi, weledi, bla bla ... hamlioni hilo?

Liko wazi hata kwa sisi wa kawaida.
 
By th way kama huyu Chiligati ndo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM. Basi tatizo la hiki chama ni kubwa kuliko nilivyo dhani coz nikiunganisha na akina Kinana ndo naelewa kuwa kimeoza kuanzia kwenye shina lake.
 
Tusijidanganye. CCM know what they are talking about.
Itakuwa vigumu kwa wabunge wa Chadema kufanya kazi bungeni iwapo chama chao hakiitambui serikali inayotawala.
Cha ajabu ni kwamba walishaapa kuilinda katiba ambayo ndiyo iliyomweka Rais wasiyemtambua madarakani.
Motion inayopelekwa na CCM itapita na wabunge watafukuzwa bungeni. Take my word.

Mnaojiita wasomi, weledi, bla bla ... hamlioni hilo?

Liko wazi hata kwa sisi wa kawaida.

Na ndiyo itakuwa kaburi la ccm. refer madhara waliyoyapata kwa kumsimamisha Zito Kabwe. Huyo alikuwa mmoja tu Je wabunge 46?
 
Hawana ubavu huo hata kidogo Wanaona aibu tu kwa kuumbuliwa na madudu ambayo wanaendelea kuyafanya.
Hana mamlaka ya kuwazuia watu wasicheze KIDUKU CHAO. Awaache waendelee kucheza wakimaliza tutawauliza iwapo hicho ndicho tulichowatuma.
 
Nafikiri huyo Chiligati alikuwa anatumia mdomo kwa sababu anao. Ungekuwa unalipia maneno unayoongea naamini hasingeweza kupoteza hela yake kwa kuongea upupu huo. Kama wanaweza kuwafukuza sasa wanasubiri nini?? Bunge halina huo ubavu huo. Mahakama inaweza imuondoe mbunge kama kulikuwa na petition halali iliyokuwa inahusiana na uchaguzi wake.

Tofauti na hapo CCM wanataka kutumia tu midomo yao kwa sababu wanadamu tulipewa.
 
mtatumia maneno yote lakini ukweli utabaki palepale. To the party chadema is right to the public they are wrong. wananchi wanajua rais yupo. Lakini rais wa chadema hayupo. Vikao wanahurudhuria vya nini. Wasuse kila kitu mpaka 2015 tutawaelewa kweli hawana serikali. Wabunge wametumwa kuwakilisha wananchi si chama. Tatizo la jf ni kutaka kuona kila mtu anasurpot chadema whis is imposible.

hapo kwenye rangi am part of the public and i say they are damn right well done chadema
 
kwa nini chadema haikupata wabunge zaidi ya 100. Wabunge kiduchu kilele nyingi. Hawana adabu. Dhara kubwa. Eti wanatambua serikali lakini si matokeo. Kwa nini walitoka badala ya kueleza hoja yao kwa njia nyingine. Badala ya kuchezea chombo kikubwa kama bunge. Wachochezi wakubwa . Chadema has a devil sipirit.

hapa nadhani nampigia mbuzi gitaa lakini i will try:-
1. Chadema ilipata wabunge wachache sababu ya kuchakachua na wizi thats why wanaprotest
2. Wangeleta hoja bungeni isingesikiliwa ingezimwa tu, thats why wametumia the perferct way, message sent, and media coverage kibao thats why we are now talking about it now. Nadhani umeelewa dont worry hii ni elimu ya bure natoa
 
Inaonekana elimu ya uraia bado haijawaingia watanzani,kuna umuhimu kwa watanzania kuisoma katiba ili kujua mapungufu yaliyomo.Tuna kazi kubwa ya kuwaelimisha watanzania.Kitendo kilichofanywa na chadema kimemfanya Kikwete kuongea,pinda ameongea,chiligati ameongea,UVCCM wameongea,wanaojiita wasomi wa dodoma wameongea lakini spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania mh.Anne Makinda amenyamaza kimya..Why,kwanini hajaongea?Ni kwa sababu anajua walichofanya chadema kina maana gani katika kukuza demokrasia.Watanzania wengi ni waoga kwa sababu hawazijui haki zao
 
Chiligati = CCM Chili sauce, ni huyu Chili source alimfukuza uanachama wa CCM Bashe, aibu ikamrudia, ukitaka kujua anaongelea MDOMO na Si Ubongo wake, ni kanuni au sheria ipi ambayo eti wabunge wa CCM wanaweza kuwafukuza wabunge wa CHADEMA,...!!!!? anazeeka vibaya kweli huyu OLD DUDE, hawa CCM hawasomi nyakati wanalala, kuanzia uongozi wao wote madudu, sasa mwambie wajaribiu aliyoyasema ataona how it will Backfire the whole country, c'mon Chili do it, unajidanganya kweli
 
a party of emotional youth. Kila action inayofanyika ni kama ya mtoto aliyekarika na kuanza kuvunja glass na sahani. Hasira ikiisha ataomba maji ya kunywa wakati hana glass. Simple example. People are not happy in whatever words you put.
Naona kama vile hapa unajisemea mwenyewe, yaani you are talking to yourself kama yule mwendawazimu vile.
 
Tusome Ibara ya 71 ya katiba ya tanzania,imeeleza wazi sababu zinazoweza kumfanya mbunge apoteze kiti chake cha ubunge,kitendo cha wabunge wa chadema hakiwezi kuwafanya wapoteze nafasi zao .Kesho nabandika kanuni
 
Hayo aliyoyasema Chiligati ni kujitutumua, CCM inajua ikileta hoja hiyo itakuwa imefungulia CHADEMA mlango wakupeleka kesi yao kwa wananchi na hilo litawasha moto nchi nzima
 
Back
Top Bottom