Elections 2010 CCM yatoa tamko kuhusu kitendo cha wabunge wa CHADEMA

Elections 2010 CCM yatoa tamko kuhusu kitendo cha wabunge wa CHADEMA

a party of emotional youth. Kila action inayofanyika ni kama ya mtoto aliyekarika na kuanza kuvunja glass na sahani. Hasira ikiisha ataomba maji ya kunywa wakati hana glass. Simple example. People are not happy in whatever words you put.
 
E bwana eeeee............then wananchi watawakilishwa na nani huko bungeni. Majimboni hakutatosha.
 
Taarifa ya Tbc ya sa2 usiku mjumbe wa Nec,chiligati amesema Chadema wakiendelea ivo wabunge wa ccm wataagizwa kuwafukuza bungeni wabunge wa chadema. Pia kaongeza kusema kuwa wamevunja katiba,ila ajafafanua wamevunja katiba ya nchi gani maana mpaka sasa napekua katiba sijaona kipengele kilichovunjwa. Kwa iyo inapaswa kuwepo katiba mpya itakayokuwa na kipengele cha kuwabana wabunge kumheshimu rais wakati anahutubia bunge. Kuwepo kwa katiba mpya chadema itakuwa imepata dai lake la kwanza. Pili kapt.Chiligati amesema Rais ni sehemu ya Bunge kwa iyo chadema kutoka bungeni imekimbia ofisi yake ya kazi. Ila katiba ninayoijua mimi ya Jamhuri wa muungano wa tz inasema taasisi ya rais itakuwa mhimili mmoja na mihimili 2 ni Bunge na Mahakama. Hapa kuna kitu pia kinaitwa "seperation of power" na "checks and balance" je kweli chiligati ni mbumbumbu wa kuchanganua au ni udikteta au ni utukutu au hakuyaona madarasa ya shule. Great thinkers,bila kujali itikadi zetu za kisiasa,ebu tuelezane ukweli hapa maana sisi ni wasomi na weledi. Nawasilisha.
Chiligati kwa kukurupuka ni kama Makamba tuu. Hivi kama kuwafukuza watatumia kipengele gani cha katiba?
Hivi haya mambo ya kutishana mpaka miaka hii bado yapo tuu?
Kuna watu kweli hawakustahili hata kuwa kwenye uongozi kwa mawazo mabovu kama haya.
Nadhani hata jumuiya ya kimataifa ikisikia mambo haya watashangaa sana.
Mtu anaongea kama anaongea na wamachinga wa mchikichini wasiojua haki yao.
 
Nasikia Chadema nao wanampango wa kuwafukuza wabunge wa CCM kwa kuzomea bungeni wamevunja kifungu cha kumi cha katiba ya Chadema hii ndiyo TZ bwana ukisikia nyingine ni ya uongo ndio maana kina RA hawataki kuondoka.

mkuu sasa si itakuwa ngonjera? Umeniacha hoi mkuu. Sasa si siku moja wataamua kuwekeana makufuli kwenye malango ya bunge? Nkafikiria siku moja mbowe kaenda mapema bungeni na kufunga malango kwa kofuli ili msemo wa ukimwaga ugali namwaga mboga utimie! Nadhan hatutafika huko,mafisadi wameshaanza kuona aibu! Jeyki kasema atawawekea baraza la mawaziri waadilifu. Ni dhairi apa hatogusa list of shame/11 first eleven,pia akina mama meghji wasahau uwaziri kama alivosema.
 
Please Chiligati fanya upesi iwezekanavyo. Naona unachelewa mchakato ungetakiwa uanze hata kesho. CHADEMA walitishia kumsusia Kikwete na wakafanya kweli. Yeye anatishia. Afanye kweli kama yeye ni mwanaume
 
kwa nini chadema haikupata wabunge zaidi ya 100. Wabunge kiduchu kilele nyingi. Hawana adabu. Dhara kubwa. Eti wanatambua serikali lakini si matokeo. Kwa nini walitoka badala ya kueleza hoja yao kwa njia nyingine. Badala ya kuchezea chombo kikubwa kama bunge. Wachochezi wakubwa . Chadema has a devil sipirit.
Chaka chua matokeo(CCM) is a devil
 
Usichoelewa ni kwamba, CHADEMA hawamtambui Kikwete kwa sababu hakupewa madaraka yale kwa mujibu wa Katiba. Wao wameapa kuilinda katiba, na kwa kuwa katiba hiyo ilivunjwa wakati wa kumsimika Kikwete, basi hawamtambui Kikwete kama rais. Iwapo Kikwete angesimikwa kwa kufuata Katiba kuwa watu walipiga kura, zikahesabiwa sawasawa na kujumlishwa bila makosa, basi tatizo hili lisingekuwapo.

Mkuu, huwa nashindwa kuelewa inakuwaje mambo yaliyo wazi namna hii watu wanashindwa kuyaona ??
Hii elimu ya kata wanayopewa siku hizi watanzania wenzetu ni sumu kwa maendeleo yetu.
 
Mkwele aachie ngazi kama ameshindwa kuongoza nchi...Wadanganyika tumeshaamka na maneno ni mbele kwa mbele mpaka CHADEMA iingie IKULU tushaichoka "CHI CHI EMU" tokea nantini kweusi mpaka leo wanang'ang'ania madaraka.Waachie ngazi kabla hawajaangukia pua 2015
 
Chiligati hakuchagua wabunge hawa wananchi ndio waliowachagua na wanataraji kupata maendeleo kupitia kwao la kujiuliza hapa je wabunge hao watashiriki vipi kujadili hotuba ya Rais wakati waliondoka na wataijadili vipi wakati aliyeitoa hawamtambui kama Rais, Yaani ni Chadema tu waliotoka CUF, TLP na vingine ? WE Mboe acha dharau hiyo ! tunataka kusikia toka kwako hoja za msingi sio kumsusia Rais hali ukijua kuwa huwezi kubadili kitu sasa cha msingi tukae tupiganie namna ya kubadili katiban yetu ndio yenye mapungufu makubwa tukiweza hapo basi tumepata serikali.
 
NDG CHILIGATI, NASEMA SITAKI

Mara baada ya kusoma hayo mawazo ya Kpt Chiligani, kwa haraka haraka, nyuma ya ujumbe wake huo, nimebaini kwamba haswa ndiye 'MSOMI WA VYUO VIKUU MKOA WA DODOMA' aliyetukarimia TAMKO zuri lile. Kama huamini, rudia kuusoma huo ujumbe hapo juu na ulinganishe upepo ulioko kwenye KOO na LADHA ya MATAMSHI inayotoka mdomoni na utagundua kitu.

Sasa kwa kuridhika na hicho nilichokigundua kwenye taarifa hizo mbili, na CUF kukimbilia kiti cha Upinzani Bungeni hata kabla Guu la mwisho la Mwana-CHADEMA kuishia mlangoni wanavyotoka nje na CUF pamoga na NCCR-MANUNUZI kuendelea kuisakama kusikoisha CHADEMA, nasema kwa nguvu hapa (kama Mhariri Mkuu wa Daily News alivyoonyesha uwezo Mkubwa kuliko Sheik Yahaya KUTABIRI kwamba Dr Slaa HATOINGIA ikulu AFTER-ALL) kwamba kwa dakika hii Werema, Mkono na yule Ringo Tenga mkubwa WANAKAMILISHA MUSWADA kwa ajili ya CCM kuwapokonya RASMI Umma wa Tanzania hata huo uwakilishi mdogo walioipa CHADEMA. Kwa msingi huu, ndi maana nasema:

(1) Sitaku Kumzungumza Kpt Mstaafu John Chiligati kwa kuwa taaluma yake ni UTII KWANZA maswali baadaye, na wala HAKI na DEMOKWASIA ni sayari nyingine kabisa kwake,:bump:

(2) Sitaki kumzungumza Chiligati Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM kwa kuwa PROPAGANDA ndio silaha yake ya kufanyia kazi hiyo, nasema

(3) Sitaki kumzungumza Waziri wa Zamani wa Ardi na Maendeleo ya makazi anayetumia muda wake 80 % kwa chama na 10% mapunziko 5% ofisini, na wala

(4) Sitaki kumjadili mheshimiwa sana huyu kwa vigezo vya lipi CCM ina uwezo wa kufanya bungeni kwa sababu CHADEMA haikupata ridhaa ya uwakilishi Bungeni ili watekeleze maelekezo SAHIHI ya chama hicho kwa kuwa naelewa fika kwamba Tanzania yangu sio kisiwa wa kutekeleza UKIRITIMBA WOWOTE usioafikika na Jumuiya ya Kimataifa,

Ninachoomba jamvini hapa, nipeni tu mawazo yake aliyoyatoa kwenye kioo TBC na pia Wanasheria wetu tumwagieni VIFUNGU ndio tupate KUTENDEA HAKI STAHILI mawazo yake hayo. Kumbukeni, Chiligati anayo haki ya kutetea anachokipenda, CCM nacho kama taasisi pia kina haki ya kusikilizwa humu jamvini lakini haki zote hizo zinakosa nguvu na ushawishi wowote mbele ya UMMA mpaka KWANZA WATANGULIE KUTUAMBIO KWA DHATI KABISA NINI WANACHOKIJUA KUHUSU MADAI YA 'MPANGO MZIMA WA UCHAKACHUAJI UCHAGUZI KULE HOTEL LAKAIRO' Mwanza ambayo ndi imetufikisha hapa tulipo leo hii.

Wana JF, Bila VIFUNGU sahihi hapo nembo yetu ya GREAT THINKERS itachuja, Bila majibu ya Njama za Kuiba Kura Uchaguzi Mkuu 2010 kama ambavyo tulivyoshuhudia sote nako tunasema si CCM wala Chiligati anapata MORAL STANDING ya kusikilizwa humu licha ya kuonekana LEGALLY existing.

Niwashilishe kwenu ...
 
E bwana eeeee............then wananchi watawakilishwa na nani huko bungeni. Majimboni hakutatosha.

Hapo sasa ndipo hakutakuwa na mwenye uwezo wa kuwatuliza wananchi.
Wale raia wa Arusha mjini tu waliwatoa kamasi mpaka wakasalenda wenyewe.
 
Ubavu huo hawana hata kidogo, wanaona aibu tu kwa kuumbuliwa na madudu ambayo wameyafanya.
 
Hiri ri nchi bana limejaa vichekesho kweeri.

Yaani wakti wa Uchaguzi Mkuu NEC walivunja Katiba waziwazi kwa kuwanyima Watanzania karibu milioni 12 haki yao Kikatiba kupiga kura. Hakuna aliyelalamika hata mmoja si CCM,CUF,TLP wala UDP kuwa NEC walikuwa wanavunja Katiba.

Lakini leo kwa CHADEMA kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge kumwonyesha rais kuwa hawakubaliani na namna Uchaguzi ulivyoendeshwa wanavunja KATIBA sijui ipi.
 
.........,chiligati amesema Chadema wakiendelea ivo wabunge wa ccm wataagizwa kuwafukuza bungeni wabunge wa chadema. ..........

He is stupid!!
kwamamlaka gani? Kwani ccm ndio waliowachagua wabunge wa CDM?
Tell him to go back to school.
 
Hawana ubavu huo hata kidogo Wanaona aibu tu kwa kuumbuliwa na madudu ambayo wanaendelea kuyafanya.
 
kikwete akiwa ikungu pale alipozaliwa tundu lissu alisema ni bora slaa kuwa rais kuliko lissu kuwa mbunge,wanjua nini kitakachowapata mijadala ya bunge ikianza,hiyo defensive mechanism yao ni mbaya,naliona anguko la ccm
 
Nyie ndio wabaguzi msiotakiwa katika nchi hii. Najua inawauma sana kwa mswahili kukaa pale Ikulu na itawauma sana 5 more years.

wewe shkh yahya.. huna hata aibu...

watanzania walio wengi wanataabika wewe unaunga mkono ujinga..

Aluta kontinua mapambano yameaanza mpaka kieleweke.
 
Back
Top Bottom