William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
Mheshimwa William! Heshima sana Mkuu.
Sasa utakubaliana na mimi kuwa SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA. CCM imepoteza kabisa confidency mbele ya umma kwa kuendekeza viongozi wabovu kama huyo Mzee aliyeita waandishi wa habari akasema Bashe sio raia wa Tanzania na kisha akaingia mitini, leo anataka kuwafukuza Wabunge, yeye amekuwa Spika??? Hata Spika hawezi ila mpaka pale sababu za Kanuni na sheria zitakaporuhusu kufanya hivyo
CCM ina kila dalili za kuanguka na wale tunaoipenda tutabaki midomo wazi. EL amemshauri Mh. Pinda achunguze ni kwa nini vijana wana hasira na CCM, inawezakana EL ameliona hili na anajua madhara yake kwa siku za Usoni, lakini hao wengine hapo wanataka kumpendeza rais hata ikibidi kufuta vumbi la viatu watafanya lakini they don't want to face the reality.
Amini usiamini madudu yanayoendelea yanazidi kuizamisha ccm na itazimi ingawa si kwa mapenzi yetu
- Mkuu heshima yako sana, Kama kuna adhabu yoyote kikatiba kuhusiana na kususa kwa wabunge wa Chadema, ni Spika, Naibu Spika na labda Katibu wa Bunge ndio naamini wenye mamlaka ya kuongelea adhabu kwa Wabunge hao, hapa Ndugu yangu sana Mh. Chiligati amechemka sana na ni vyema CCM kama chama tawala wakajiepusha publicly na hizo kauli.
- Otherwise, hii ni kesi ndogo sana ni ya ya Political Public Relations zaidi kuliko ushindani wa katiba, Wabunge wameajiriwa na wananchi sio bunge sasa kama Wabunge wanafanya kinyume na wananchi waliowaajiri, kesi yao ipeleke kwa Wananchi wale wale waliowaajiri: exactly what Bill Clinton did, Spika wa Republican Gingrich, aliamua kufunga Federal Government akidai ndio kazi aliyotumwa na wananchi, Clinton hakupingana naye kabisa kwenye katiba wala serikali, alichofanya alipeleka kesi yake kwa wananchi, wananchi wakaangalia hoja za Gingrich na Clinton, waakaamuita Gingrich kuwa ni Crying Baby na kuwaadhibu Republicans kwenye kura!
- Kina Mh. Chiligati wajifunze sasa kwamba hizi ndio siasa za kisasa yaani smart modern politics kwamba zinashindaniwa kwa nguvu ya hoja kuliko hoja ya nguvu, waende kwa wananchi na kuwaonyesha kwa hoja na evidence kwamba hawa wabunge 46 na chama chao hawawafai kwa sababu one, two, three and four kutokana na kususia kwao hotuba ya Rais, au kutomtabua Rais aliyechaguliwa na wananchi hao hao, I mean kuwatishia kuwafukuza bungeni ni majibu rahisi sana ya maswali magumu!
- Na infact wanaotakiwa kutoa kauli za adhabu kwa Wabunge hao ni Spika, Naibu Spika na Katibu Wa Bunge, sio mbunge na kiongozi wa CCM! Haya mambo mengine yanaudhi sana!
William.