Elections 2010 CCM yatoa tamko kuhusu kitendo cha wabunge wa CHADEMA

Elections 2010 CCM yatoa tamko kuhusu kitendo cha wabunge wa CHADEMA

Mheshimwa William! Heshima sana Mkuu.
Sasa utakubaliana na mimi kuwa SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA. CCM imepoteza kabisa confidency mbele ya umma kwa kuendekeza viongozi wabovu kama huyo Mzee aliyeita waandishi wa habari akasema Bashe sio raia wa Tanzania na kisha akaingia mitini, leo anataka kuwafukuza Wabunge, yeye amekuwa Spika??? Hata Spika hawezi ila mpaka pale sababu za Kanuni na sheria zitakaporuhusu kufanya hivyo
CCM ina kila dalili za kuanguka na wale tunaoipenda tutabaki midomo wazi. EL amemshauri Mh. Pinda achunguze ni kwa nini vijana wana hasira na CCM, inawezakana EL ameliona hili na anajua madhara yake kwa siku za Usoni, lakini hao wengine hapo wanataka kumpendeza rais hata ikibidi kufuta vumbi la viatu watafanya lakini they don't want to face the reality.
Amini usiamini madudu yanayoendelea yanazidi kuizamisha ccm na itazimi ingawa si kwa mapenzi yetu


- Mkuu heshima yako sana, Kama kuna adhabu yoyote kikatiba kuhusiana na kususa kwa wabunge wa Chadema, ni Spika, Naibu Spika na labda Katibu wa Bunge ndio naamini wenye mamlaka ya kuongelea adhabu kwa Wabunge hao, hapa Ndugu yangu sana Mh. Chiligati amechemka sana na ni vyema CCM kama chama tawala wakajiepusha publicly na hizo kauli.

- Otherwise, hii ni kesi ndogo sana ni ya ya Political Public Relations zaidi kuliko ushindani wa katiba, Wabunge wameajiriwa na wananchi sio bunge sasa kama Wabunge wanafanya kinyume na wananchi waliowaajiri, kesi yao ipeleke kwa Wananchi wale wale waliowaajiri: exactly what Bill Clinton did, Spika wa Republican Gingrich, aliamua kufunga Federal Government akidai ndio kazi aliyotumwa na wananchi, Clinton hakupingana naye kabisa kwenye katiba wala serikali, alichofanya alipeleka kesi yake kwa wananchi, wananchi wakaangalia hoja za Gingrich na Clinton, waakaamuita Gingrich kuwa ni Crying Baby na kuwaadhibu Republicans kwenye kura!

- Kina Mh. Chiligati wajifunze sasa kwamba hizi ndio siasa za kisasa yaani smart modern politics kwamba zinashindaniwa kwa nguvu ya hoja kuliko hoja ya nguvu, waende kwa wananchi na kuwaonyesha kwa hoja na evidence kwamba hawa wabunge 46 na chama chao hawawafai kwa sababu one, two, three and four kutokana na kususia kwao hotuba ya Rais, au kutomtabua Rais aliyechaguliwa na wananchi hao hao, I mean kuwatishia kuwafukuza bungeni ni majibu rahisi sana ya maswali magumu!

- Na infact wanaotakiwa kutoa kauli za adhabu kwa Wabunge hao ni Spika, Naibu Spika na Katibu Wa Bunge, sio mbunge na kiongozi wa CCM! Haya mambo mengine yanaudhi sana!


William.
 
Ndugu zangu,

Jana wananchi tumehabarishwa kupitia katibu mwenezi wa ccm mzee chiligati kuwa ccm inaandaa tamko kwa kushirikiana na vyama vingine vya upinzani kuhusiana na kitendo cha chadema kususia hotuba ya jk bungeni. Katika kuandaa tamko hilo, wanatafuta pia vifungu vya sheria na kanuni kuona namna wanavyoweza kuwaadabisha chadema ikiwa ni pamoja na kuzuia wasishiriki vikao vya bunge.

Binafsi natambua kwamba kwa chama kilichozoea na kukuzwa na sifa bandia, ambacho hata kikifanya kosa kubwa lililo dhahiri bado kinapigiwa makofi, tukio lile lilikuwa la udhalilishaji mkubwa kwake. Najua kitendo kile kimewauma sana. Lakini jambo moja ningeomba wakumbuke na kama hawafahamu basi sasa wahafamu kwamba hiyo ndiyo gharama ya DEMOKRASIA na wataendelea kuilipa siku zote as long as mazingira ya siasa yataendelea kuwa hivi ilivyo sasa.

Ushauri wangu wa dhati kwa ccm ni mdogo tu. Wasipoteze muda wao kutafuta vifungu vya kuiadabisha chadema. Havipo na wala kwa hali ilivyo sasa havitakuja vitokee. Wanachopaswa kufanya ni kukaa na kutafakari wapi wamekosea na nini wafanye ili kurejesha hali ya utulivu wa kisiasa nchini. Na zaidi ya yote waanze kutekeleza ahadi walizotoa kwa wananchi maana kufumba na kufumbua 2015 itawadia. Wakiendelea kupambana na chadema wataendelea kupandisha hasira za wananchi na nchi haitatawalika kamwe. Ninawaonea huruma viongozi wa serikali watakaoteuliwa sijui watafanya kazi na nani kwenye majimbo yote yaliyo chini ya chadema. CCM HESABUNI GHARAMA KABLA YA KUTENDA.
 
Bogus are u CHADEMA who act like college students.Plus ur leader who need to go to anger management,he is a manipulater and tribalism .All for his personal selfishness.
Pole Mikese naona kitendo cha wabunge wa chadema kimekutachi sana ndiyo siasa, mlitegemea siasa za kizamani za kupigiana makofi zimepitwa na wakati, jaribu kutembelea mabunge mbalimbali ya Urusi UK Marekani hata hapa jirani zetu uone yanavyoendeshwa. Usitegemee bunge hili liwe kama bunge letu la 80s kukaa kama kamati ndiyo imepita, na huo ni utangulizi tu picha yenyewe haijaanza, salamu kwa Makinda.
 
Army guys are not the smartest.Kila wakati ni kutekeleza amri and very little room for reasoning.Msameheni bure huyu jamaa as always mchemkaji:embarrassed:
 
Jamani atupe basi ni kifungu gani cha katiba na hasa ni kanuni gani ya bunge imevunjwa?

Wakuu nimeanza kuwa na mashaka na hali ya bunge la sasa. Sijui kama kweli CCM ina haki ya kikatiba ya kuwafukuza wabunge waliochaguliwa na wananchi, sijui kama kweli Chiligati anasema hilo kwa jazba au anasema kutokana na kanuni za bunge, sheria au ni uelewa finyu.

Mpaka sasa bado sijui kama kuna sheria, kanuni au taratibu zozote zinazokiruhusu chama chochote kuwafukuza wabunge wa chama kingine kwenye bunge la jamhuri.

Kuna wakati inatakiwa wasemaji wawe watu makini, isiwe watu wanaoongea tu kwa kuwa kazi yao ni kuongea. Haiingii akilini hata kidogo.
 
Chadema wamebeep.............dons watapiga kweli. Kususa hotuba ni kitendawili ambacho ccm inabidi wasikitegue.
 
Tatizo hapa ni kwamba akina Chiligati wanamfhamu bvizuri bosi wao, the reactions could be just a show off kupoza mfadhaiko ambao the apologists think mkuu atakuwa amepata baada ya tukio lile.
 
Hamna mtu atakayewafukuza, ila kama wataendelea kutokuitambua serikali ya Rais, hawatakuwa na cha kufanya bungeni.
 
- Mkuu heshima yako sana, Kama kuna adhabu yoyote kikatiba kuhusiana na kususa kwa wabunge wa Chadema, ni Spika, Naibu Spika na labda Katibu wa Bunge ndio naamini wenye mamlaka ya kuongelea adhabu kwa Wabunge hao, hapa Ndugu yangu sana Mh. Chiligati amechemka sana na ni vyema CCM kama chama tawala wakajiepusha publicly na hizo kauli.

- Otherwise, hii ni kesi ndogo sana ni ya ya Political Public Relations zaidi kuliko ushindani wa katiba, Wabunge wameajiriwa na wananchi sio bunge sasa kama Wabunge wanafanya kinyume na wananchi waliowaajiri, kesi yao ipeleke kwa Wananchi wale wale waliowaajiri: exactly what Bill Clinton did, Spika wa Republican Gingrich, aliamua kufunga Federal Government akidai ndio kazi aliyotumwa na wananchi, Clinton hakupingana naye kabisa kwenye katiba wala serikali, alichofanya alipeleka kesi yake kwa wananchi, wananchi wakaangalia hoja za Gingrich na Clinton, waakaamuita Gingrich kuwa ni Crying Baby na kuwaadhibu Republicans kwenye kura!

- Kina Mh. Chiligati wajifunze sasa kwamba hizi ndio siasa za kisasa yaani smart modern politics kwamba zinashindaniwa kwa nguvu ya hoja kuliko hoja ya nguvu, waende kwa wananchi na kuwaonyesha kwa hoja na evidence kwamba hawa wabunge 46 na chama chao hawawafai kwa sababu one, two, three and four kutokana na kususia kwao hotuba ya Rais, au kutomtabua Rais aliyechaguliwa na wananchi hao hao, I mean kuwatishia kuwafukuza bungeni ni majibu rahisi sana ya maswali magumu!

- Na infact wanaotakiwa kutoa kauli za adhabu kwa Wabunge hao ni Spika, Naibu Spika na Katibu Wa Bunge, sio mbunge na kiongozi wa CCM! Haya mambo mengine yanaudhi sana!


William.

Mkuu unajua inasikitisha sana, kuona watu kwenye nafasi za juu za chama wanafanya mambo ya kijinga na ya kitoto. Sikutegemea kauli kama hii kutoka kwa Chiligati. Huyu jamaa ni captain wa jeshi, na mkuu wa idara muhimu ya chama na ni mbunge, kutoa kauli kama hiyo inaonesha kuwa uwezo wake umefika mwisho, na hastahili kuendelea na nyadhifa hizo.

Kwanza anaingilia majukumu ya bunge, speaker na ya vyama vya upinzani. CHADEMA ina mwenyekiti wake, kwa hiyo kama mwanachama wake akifanya vibaya basi yeye ana uwezo wa kumwajibisha, kuna whip wa opposition anaweza pia kushghulikia issue kama hiyo kwa namna yake. Chiligati is very low, ni bora chama kiwe na mtu mwingine kwenye nafasi hiyo. Jamaa amekuwa anaongea pumba mra kwa mara. Inabidi sasa Chama kiwe na utaratibu wa kuongea kwa niaba ya chama si kila mtu aongee.
 
Tusome Ibara ya 71 ya katiba ya tanzania,imeeleza wazi sababu zinazoweza kumfanya mbunge apoteze kiti chake cha ubunge,kitendo cha wabunge wa chadema hakiwezi kuwafanya wapoteze nafasi zao .Kesho nabandika kanuni


Mkuu, hapa nilipo nimelazimika kulipigia kompyuta yangu saluti. Nilidhani kwamba utakua unaniona ili ukapokee heshima zako hizo. Hakuna kitu ninachokiheshimu kama mjadala (1) kwa njia ya kutumia NUKUU zenye kutambulika na kuheshimika, (2) Mantiki na mifano hai, (3) upembuaji jambo kwa kutumia 5Ws + H, na (4) facts, Figures na tafsiri zake ...

Mkuu big up sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Taarifa ya Tbc ya sa2 usiku mjumbe wa Nec,chiligati amesema Chadema wakiendelea ivo wabunge wa ccm wataagizwa kuwafukuza bungeni wabunge wa chadema. Pia kaongeza kusema kuwa wamevunja katiba,ila ajafafanua wamevunja katiba ya nchi gani maana mpaka sasa napekua katiba sijaona kipengele kilichovunjwa. Kwa iyo inapaswa kuwepo katiba mpya itakayokuwa na kipengele cha kuwabana wabunge kumheshimu rais wakati anahutubia bunge. Kuwepo kwa katiba mpya chadema itakuwa imepata dai lake la kwanza. Pili kapt.Chiligati amesema Rais ni sehemu ya Bunge kwa iyo chadema kutoka bungeni imekimbia ofisi yake ya kazi. Ila katiba ninayoijua mimi ya Jamhuri wa muungano wa tz inasema taasisi ya rais itakuwa mhimili mmoja na mihimili 2 ni Bunge na Mahakama. Hapa kuna kitu pia kinaitwa "seperation of power" na "checks and balance" je kweli chiligati ni mbumbumbu wa kuchanganua au ni udikteta au ni utukutu au hakuyaona madarasa ya shule. Great thinkers,bila kujali itikadi zetu za kisiasa,ebu tuelezane ukweli hapa maana sisi ni wasomi na weledi. Nawasilisha.

nimeamini ccm italeta vurugu nchini viongozi wake hawako makini kujenga umoja taifa mawazo yao yapo kwenye uvyama udini na ukabila jee leo wabunge wa chadema wakirudi majimboni kuhamasisha wananchi wajitenge na tanzania hapo ccm watafurahi kama walivyo furahi pale wajumbe wa nyumba kumi toka zeenj kugombea na kukalia viti vya wabunge wa chadema...
 
Nadhani KAMBA HUENDA KATIKIA PABOVU mkononi mwake Ndg Kikwete endapo atadiriki kuongozwa na HASIRA ZAKE hizo.

Nadhani ilikua ni busara kubwa kwa Wabunge wa CHADEMA kutoka nje au ni MUNGU tu alitaka kuwakwepeshe HAMAKI ambayo ingewakuta baada ya kusikia Hutuba unaofanana kuandaliwa kwa ajili ya kikao cha wana CCM pekeyao na kujikweza zaidi.

Hebu safiri kidogo kimawazo na utagundua kwamba kote dunia, natanguliza samahani kwa lugha hii, ukisikia mtu KAMBAKA mzazi wako (DEMOKRASIA) halafu awe amepangiwa hafla ya kuzungumzia hilo hata akaja kabisa hadi Bungeni uliko utadiriki kabakia kwenye kiti kweli na kutoa HESHMA kwake kwa hilo, inakuja kweli???

Isitoshe, jamaa kaja rasmi na na kutamka maudhui yake ya kuzindua tangu juzi harakati nyinginezo za UBAKAJI mwaka wa 2015 hadi hapo huoji kwamba aliyejeruhiwa kama CHADEMA anaweza kushindwa kujizuia na mengi sana??? Hasira za CCM ni kwamba DHORUBA ZA MABADILIKO TANZANIA yanakuja mithili ya Tsunami lakini mambo yanakwenda KISAYANSI MNO kiasi kwamba wanashindwa hata pa kuagizia DOLA kwenda kupiga mtu.

Si ajabu hata huko kwenye MAJESHI YETU mambo sio yenyewe kabisa. Kwani na wao ni Wa-Tanzania kabla hawajaitwa Wana-Jeshi tena letu sisi Wananchi hivyo HAYA BABAYA YOTE YANAYOTUSIBU nao pia huenda ikawa inawauma kweli. Tusishangae Jeshi nalo likisema NO kwa MAFISADI kama muitiko wao kutetea MASLAHI YA TAIFA na wala sio MASLAHI ya kikundi.

Asante Mungu kwa kuhepusha hayo yote.
 
Kuna watu humu akili zao na Chikigati ziko sawia sana.

Nashauri mjifunze kanuni za Bunge msiwe kama Chiligati anayesema JK ni sehemu ya Bunge! Jielimisheni ni kwa nini wabunge wa CDM walitoka nje wakati raisi anaanza kuhutubia na sio kabla ya kuhutubia?

Ninyi msioelewa hayo nilioeleza hapo juu jielimisheni vizuri kisha mrudi hapa jukwaani kuchangia hoja objectively nadhani Kishongo atakuwa na ufahamu mzuri tu. Naamini mtaelewa vizuri badala ya kuwapotosha watu kuwa CDM walitoka nje kwa sababu hawamtambui raisi. Kwamba wabunge wa CDM walikuwa haki kabisa ya kutoka nje na kwamba CCM kisheria haina uwezo wa kumfukuza mbunge Bungeni. Pia hakuna kipengele chochote cha katiba ya nchi kilichovunjwa.
 
Imagine Chiligati huyu ndio alikuwa Waziri ktk serikali iliopita!! Pata picha ya uwezo wake kumshauri raisi acha kutimiza majukumu yake. Mliofuatilia hotuba ya JK kuzindua Bunge mtakumbumba kuwa alisema anakusudia kuwa na baraza la watu makini na wachapa kazi. Naamini anawafahamu watu Chiligati walivyomleti down.
 
@kiungani hilondilo jibu kwa yule kijana anayekulupukia mambo pasipo kutadhimini na kuyachambuwa,huo ndio ukweli wenyewe,kamwe ccm na wabunge wake hawawezi na hawatadhubutu kuliongelea hilo labda wale mbumbu wasiojuwa sheria kama @kishongo go to hell man,you dont have time to live,lets iron people express what they think its right


mapinduziiiiiii daimaaaaa
 
Kumekuwa na maoni tofauti juu ya uamuzi wa chadema kutoka bungeni wakati kikwete anaanza kulihutubia. Hiyo ni haki ya kila mmoja wetu.

Taarifa yake kwa vyombo vya habari juu adhabu ya itakayotolewa dhidi ya chadema ikiwa ni pamoja na kufukuzwa bungeni inapotosha na kwamba inaingilia mamlaka za bunge. Na endapo speaker atamuunga mkono, basi atakuwa anaunga matakwa ya chama tawala na sio kujadili hoja. Huko tuendako siko na kwa hili sikubaliani naye
 
Source; TBC newz

Chama Cha Mapinduzi, CCM, kinaandaa tamko na mkakati rasmi kuhusiana na kitendo cha Wabunge wa Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kuondoka katika ukumbi wa Bunge hapo jana wakati Rais alipokuwa
akilifungua bunge hilo rasmi kwa ajili ya vikao vya awamu ya 2010 - 2015.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni mstaafu John Chiligati amekutana na waandishi wa Habari leo huko
Dodoma na kusema CCM inapingana na hatua ya Wabunge wa CHADEMA kuondoka Bungeni.

Amesema kwamba chama chake kitapeleka tamko rami Bungeni ili ikiwezekana kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na
Taratibu za Bunge, basi Wabunge wa CHADEMA waondoshwe katika ushiriki wa shughuli na vikao vyote vya Bunge
hadi hapo watakapotambua kuwa aliyechaguliwa kwa asilimia nyingi zaidi katika uchaguzi uliopita ni Jakaya Mrisho Kikwete
na ndiye Rais halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Hahahahaa! Jamani mbavu zanguuuuu! Mbona hii ni Ze Comedy ya NGUVU sana!

Hivi ndani ya CCM kuna watu waliosoma kweli?

Nyie mlidhani kwamba CHADEMA waliposema kwamba wao ni "watu makini" walidhani ni utani ule wa Mkwere na Mndengereko? Hawa ni watani wa jadi hawa, lakini CHADEMA haitanii NG'O! Kalaghabahoooo!

Kambi ya upinzani ilipokuwa inatamka, mara kwa mara, kwamba Katiba ya nchi ina kasoro, kwamba inalinda mazingira ya chama kimoja - CCM - kuendelea kutawala daima, CCM walipinga na kusema kwamba yenyewe ndiyo iliyoridhia vyama vingi kuwapo, licha ya kwamba wananchi hawakutaka vyama vingi, kwa mujibu wa utafiti uliofanyika miaka ya 90. Tukumbuke kwamba mfumo wa vyama vingi hauna hata miaka 20 hapa nchini! Labda una miaka kumi na ushee.

CHADEMA wameonesha kwa vitendo kwamba, Katiba hiyo hiyo yenye kasoro, yenye kuitetea CCM, inaweza kutumika KUIPINGA na KUIUMBUA CCM bila wao kuchukuliwa hatua zozote zile za kisheria. Hakuna kanuni wala sheria ndani ya Bunge inayoweza kumfukuza Mbunge kwa kutomtambua Rais. Labda niwe sijaisoma. Vivyo hivyo, Katiba - ambayo ni sheria mama - imeainisha Haki ya Kutoa Maoni (ambayo, kwa tafsiri ya sheria, kupinga ni mojawapo ya njia ya kutoa maoni...), sasa sijui watatumia Sheria ipi.

CHADEMA imeweka historia ya kuwa chama cha kwanza cha siasa barani Afrika kupinga mfumo mbovu unaopendelea chama kimoja dhidi ya vingine, kwa kuamua kutomtambua Rais aliyewekwa madarakani na mfumo huo, na pia, kutoutambua mfumo huo.

CHADEMA ingeweza kujifukuza Bungeni moja kwa moja iwapo ingewaamrisha Wabunge wake kukataa kuapishwa kuwa Wabunge. Walifanya uchunguzi. Kwa kuwa wameapa kuwa Wabunge kupitia Katiba ya nchi, na wameapa kuilinda katiba (na wameamua kupinga uhalali wa Rais kwa kuwa kulikuwa na UKIUKWAJI wa Katiba), hawatafukuzwa Bungeni.

Chiligati na wenzake wanatapatapa. Wameumbuliwa mchana kweupe. Na wale wote walioipigia kura CCM nao pia wameumbuliwa. Nyie mlikuwa mnadhani MNAWAKOMOA CHADEMA, kumbe MNAJIKOMOA WENYEWE! Mmeula wa chuya! Imekula kwenu!

Sasa mrudi, mjipange upya kutoa tamko la kukubali UKWELI, si kuwafukuza Wabunge wa CHADEMA kutoka Bungeni. Hilo halipo!

KALAGHABAHOOOOOOO!

> Mwana wa Haki

P.S. 2010 HATUDANGANYIKI! Mapambano yanaendelea! Mpaka KIELEWEKE! Huu moto ndio kwanza unakolea, wala haujawaka kisawasawa. Zipo hatua kubwa zaidi ambazo CHADEMA ingechukua, lakini hii ndogo tu IMEWATIA KIWEWE! Rasha rasha tu hizi. Yakija MASIKA sijui mtakimbilia wapi? Kwi kwi kwi kwi kwi!

Anayecheka mwisho HUCHEKA ZAIDI!
 
Bahati mbaya sana kwa chadema sababu kwa kushinda majimbo zaidi ya ishirini wamejiona wako karibu sana na ushindi...ndoto za mchana hizo, serikali imeliona hili na watabana kote waliookuwa wamewalegezea. Sio hatia nzuri kwa wanachadema sababu Richmond hakuna Tena 🙂 sijui safari hii nini! Wananchi waliowachagua wanategemea wawafanyie mabadiliko na kuleta maendeleo sio vinginevyo. Na tuone mabadiliko yatatokea wapi kwa majimbo ya chadema.Afadhali Zitto awe mwenyekiti maana Chadema ni kwa maslahi ya wafanyabiashara wachaga!!!huo ndo ukweli.
 
CCM hawajui sheria hawasomi kanuni ni wavivu,wazembe,wamejaa majungu na vijembe tu, mda wao wote wanautumia kuwaza jinsi ya kuibia hii nchi watasoma saa ngapi kanuni?!! majuzi wamemtoa SITTA sasa saivi wanawaza wafanyaje kuweka Rais fisadi 2015?!

Miaka yao imeisha na hilo hawataweza kulizuia. hata wakijificha kwenye vichaka vya udini na upuuzi wa ukabira.
 
Kwa kuwa bado haijaeleweka kwamba ni Sheria gani itakayotumika kuwadhibiti/kuwaadhibu Wabunge wa CHADEMA, au CHADEMA yenyewe kwa kutoitambua Serikali ya Rais Kikwete (jambo ambalo ni tofauti na kutomtambua Kikwete mwenyewe... tusichanganye mafuta ya taa na maji hapa!), nimeona nifanye utafiti baada ya kupata dokezo humu ndani.

Ninaambatanisha hapa ibara za katiba zinazo toa matamko kuhusu Muda wa Wabunge kushika Madaraka (Ibara ya 71) na Wabunge Kutoa Taarifa ya Mali (Ibara ya 70).

Kama kuna yeyote ambaye anafahamu mahali ambapo imeainishwa adhabu ya kutoitambua Serikali iliyopo madarakani ambayo Mbunge yeyote anaweza kuadhibiwa nayo, tufahamisheni. Ibara ya 71 na 70 hazitamki adhabu kwa "kosa" hilo.

Nawasilisha hoja.

> Mwana wa Haki

PEOPLE'S POWER!
 

Attachments

Back
Top Bottom