Mwanakijiji, hujakosea kabisa, walisema hivyohivyo, wataenda watarudi. Ukweli ni kwamba, CCM ktk mambo ambayo hawakuyategemea ni lile la wajumbe wa CDM kutoka hotuba ya JK. Walipigwa na Butwaa na hata JK mwenyewe. Lile somo la CDM ni somo ambalo watanzania wote jana wamejifunza na hata kudhubutu kufahamu kuwa, kumbe mtanzania ana uhuru wa kutokukubaliana na Rais, kitu ambacho wengi wao walikuwa hawakijui. Kama ni somo la Uraia (Civics) basi CDM wataingia ktk historia ya watanzania.
MY TAKE: CCM naomba wasome alama za nyakati.....ukweli ni kwamba ugumu na ubishi wao ktk kukubaliana na hali halisi, kutatuletea matatizo hapa nchini. Na ikiwa kama watafanya hayo ya kutaka Bunge liwasimamishe wabunge wa CDM, wafahamu kuwa, wanawanyanganya mamillioni ya watanzania haki yako ya kuwakilishwa Bungeni na wala si wale wabunge 56 wa CDM. Na hapo sasa, itabidi watanzania watafute njia muafaka nyingine ya kudai haki zao. Kama NEC ilichakachua kura, wasidhani inawezekana kuchakachua pia wabunge wa CDM pale mjengoni: Naona hali inavyozidi kwenda, waliowengi wanachoshwa na mambo haya ya ukandamizaji, chonde chonde, watu wakipoteza uvumilivu hapatakalika hapa. Na kwanini tufike huko?? Kwa ukweli, kila siku matamko ya hao waheshimiwa, yanaifanya hali ya siasa nchini kuwa tete...., Wenye masikio ya kusikia na wasikie kwani wasidhani watakuwa salama!