CCM ni chama outdated ambacho kinafosi kuongoza updated country. Mwaka 2015 kilipata kura walizopata sababu ya Magufuli as Magufuli lakini sio sababu ya chama imara. Yani mentality ya viongozi wa CCM imefika ukomo wa kurun nchi na wananchi sababu wananchi wako mbele zaidi kimawazo kuliko wao.
CCM wanatutangazia sasa tumeingia uchumi wa kati wakati hatuooni huo uchumi uko wapi. Au uchumi ni mabarabara na madaraja na maviwanja ya ndege? Tunatangaziwa tuko uchumi wa kati lakini hapohapo tunaambiwa hakuna pesa za kuongeza mishahara! Huo uchumi uko wapi? Hizi propaganda za mwaka 1970 haziwezi kufanya kazi kwenye kizazi cha mwaka 2020.
Maisha ya binadamu hayajawahi kwenda kinyumenyume. Always huwa yanaenda mbele katika nyanja zote. Unaweza ukadanganya kwa muda mchache lakini huwezi danganya muda wote. Hata wale wazee wasiojua kusoma na kuandika wanasema CCM imeshindwa kufikia mafanikio waliyotegemea. Tangu enzi za chama kimoja mpaka sasa imeshapita miaka 28 tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, ni CCM imekuwa madarakani lakini maisha yao yamebaki vilevile. Wanapiga marktime tuu.
Uchaguzi huu CCM wana hali mbaya. Kuanzia chama mpaka mgombea wao hawauziki. Mgombea ndio kabisaa hakubaliki kuanzia ndani ya chama mpaka nje ya chama. Furaha ya maisha ya binadamu haijawahi letwa na vitu. Kwa miaka 5 wamejikita kwenye maendeleo ya vitu tuu, wakasahau vitu havina uhai bali watu ndio wenye uhai, watu wana limited lifespan ila vitu vina infinity lifespan.
CCM wao wenyewe wanaifahamu hii fact kwamba hawauziki. Ndio maana kila apitapo mgombea wao basi shughuli nyingi zinasimama na raia wanasombwa kwenda kuongeza idadi ya wahudhuriaji ili ionekane wamejaza uwanja.
Sisi raia wa nchii tunawaambia hamna chama chenye hakimiliki ya uongozi wa nchi. Wekeni mazingira sawa kwa vyama vyote kisha mtuachie sisi tuchague tunachotaka. Kama mnavyotuambia tujiajiri, basi nanyi kubalini kushindwa ili mrudi mtaani kujiajiri kama sera yenu ilivyo.
Wakati ni ukuta, ukishindana nao utaumia mwenyewe.