Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 157
- 155
Simiyu – Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewaelekeza wanachama wake kutovaa sare za chama katika mkutano wa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa chama hicho, Amos Makala, unaotarajiwa kufanyika leo mjini Bariadi.
Taarifa ya chama hicho iliyosambazwa kwa wanachama imeeleza kuwa walioalikwa kuhudhuria mkutano huo wanapaswa kuvaa mavazi ya kawaida badala ya sare rasmi za chama.
“Kwa wote watakaokwenda Bariadi kwenye mkutano, wasivae nguo za chama, vaeni nguo za kawaida – ni maelekezo ya chama,” imesema sehemu ya ujumbe huo.
Hata hivyo, sababu ya uamuzi huo haijawekwa wazi, huku wadadisi wa masuala ya siasa wakitaja huenda ni jitihada za chama kuondoa taswira ya mikutano ya kisiasa kuwa ya kishabiki au kujenga mazingira ya kuwasilisha ujumbe bila ushawishi wa mavazi ya chama.
Mkutano huo unatarajiwa kukutanisha wanachama na viongozi wa chama kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Simiyu.