CCM Yawazuia Wanachama Wake Kuvaa Sare za Chama Katika Mkutano wa Katibu Mwenezi,Amos Makala.

Simiyu – Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewaelekeza wanachama wake kutovaa sare za chama katika mkutano wa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa chama hicho, Amos Makala, unaotarajiwa kufanyika leo mjini Bariadi.

Taarifa ya chama hicho iliyosambazwa kwa wanachama imeeleza kuwa walioalikwa kuhudhuria mkutano huo wanapaswa kuvaa mavazi ya kawaida badala ya sare rasmi za chama.

“Kwa wote watakaokwenda Bariadi kwenye mkutano, wasivae nguo za chama, vaeni nguo za kawaida – ni maelekezo ya chama,” imesema sehemu ya ujumbe huo.

Hata hivyo, sababu ya uamuzi huo haijawekwa wazi, huku wadadisi wa masuala ya siasa wakitaja huenda ni jitihada za chama kuondoa taswira ya mikutano ya kisiasa kuwa ya kishabiki au kujenga mazingira ya kuwasilisha ujumbe bila ushawishi wa mavazi ya chama.

Mkutano huo unatarajiwa kukutanisha wanachama na viongozi wa chama kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Simiyu.
Wasivae mavazi ya chama ili kwenye mkutano waseme watu 54 waamia ccm kutoka chadema
 
Upumbavu mtupu
 
Hili la mavazi ya CCM kwenye mikutano yao lilijadiliwa humu humu, tena wiki iliyopita.
Ni wazi mikutano ya CCM ni ya WANACHAMA T, SIYO YA WATANZANIA WOTE!

Wana CCM wasipohudhuria mikutano hiyo, mikutano haipo.

Sasa wanataka ionekane kuwa ni mikutano ambayo waTanzania wa aina yoyote wamehudhuria; kwa vile hawajitambulishi kwa mavazi.
 
Back
Top Bottom