CCM yeteka kwa mabavu ofisi za CHADEMA Rombo

CCM yeteka kwa mabavu ofisi za CHADEMA Rombo

Hata kama ni moja ni aibu kwa chama, maana hiyo moja inaweza kusababisha zingine nazo zifungwe. Kumbuka, alianza kutoka diwani mmoja sasa wamefika 201. Alianza kutoka mbunge mmoja sasa wamefika 20!
Hao hawakutoka bali walitolewa kwa vitisho na ahadi za vyeo.Hata hivyo haijasadia kushawishi Uma na ndiyo maana suluhisho lao kwao ni kuwaondoa wagombea wote wa CHADEMA.Sitashangaa pia kama hatua itakayofuata sasa ni kuwanunu viongozi wao wa chini kabisa ili wafunge matawi yao nchi nzima katika mwendelezo wa hila zile zile.Yaani wameshindwa kuifuta CHADEMA kwa kuuza Sera zao kwa wananchi badala yake wanapambana kuifuta kwa HILA kubwa kupitia mihilimi yote.SHAME.
 
Nimeshangaa kuona baadhi ya Watanzania/wanaCHADEMA wakizifunga ofisi za CHADEMA na kufuta nembo ya maandishi yanayokitambulisha CHADEMA kwenye kuta za nyumba.

Kinaendelea kitu gani nchini mpaka ofisi za CHADEMA zinafungwa na kufutwa maandishi yanayokitambulisha ukutani?

Kilichonishangaza zaidi haya yanatokea katika jimbo la Rombo mkoani Kilimanjaro kama ambavyo wahusika wanajitambulisha.

Video ya tukio
View attachment 1267947
Wangese tu, wakati zinaandikwa nani aliona? Mbona hamkuonyesha? Vipi kama ofisi imehama na kupelekea jingo kutumika kwa matumizi mengine?

Umeulizwa zimefutwa ngapi? Zimebaki ngapi?
 
Sababu iliyo muondoa Dr. Slaa ndo sababu inayo iua CDM.
 
Nimeshangaa kuona baadhi ya Watanzania/wanaCHADEMA wakizifunga ofisi za CHADEMA na kufuta nembo ya maandishi yanayokitambulisha CHADEMA kwenye kuta za nyumba.

Kinaendelea kitu gani nchini mpaka ofisi za CHADEMA zinafungwa na kufutwa maandishi yanayokitambulisha ukutani?

Kilichonishangaza zaidi haya yanatokea katika jimbo la Rombo mkoani Kilimanjaro kama ambavyo wahusika wanajitambulisha.

Video ya tukio
View attachment 1267947
chama kisicho na heshima kimepoteza msisimuko kwa wananchi hawakitaki tena ni aibu kukutwa na hiyo nembo
 
Anacho kitamka mwanachadema yoyote ndivyo anavyo fikiri/ona kimtazamo, kama Rais wa nchi anatekeleza Ilani ya chamachake kwa kujenga Barabara, Reli, Vituovya Afya, Madarasa, Vituo vya nguvu za umeme, mwendokasi, Maktaba,Elimu ya bure, kupambana na mfumuko wa bei, kusimamia bei za pembejeo za kilimo na kuondoa pembejeo feki, miradi ya meme na maji vijijini na mijini n.k
bado wanakwambia ayo ni maendeleo ya vitu na si watu sasa unatarajia kwenye mikutano yao ya kisiasa kutakua na lipi jipya?

Hata huko Spain Barcelona na Real Madrid ndio zinazobeba kombe lao mara zote, lakini timu nyingine zipo na zina washabiki wa kumwaga. Mbona hao mashabiki wote wasiache timu zao na kuhamia hizo zinazobeba kombe tu? Kwa taarifa yako chama chochote kitakachokuwa madarakani kitatekeleza hayo yote tena kwa ubora mkubwa na kuheshimu demokrasia juu. Hivyo asikudanganye mtu eti rais akitekeleza sehemu fulani ya wajibu wake, basi ana haki ya kunajisi box la kura ili chama chake kichaguliwe.
 
chama kisicho na heshima kimepoteza msisimuko kwa wananchi hawakitaki tena ni aibu kukutwa na hiyo nembo

Ni hivi cdm ipo na hata mkiifuta kwa hila, bado watu hawawezi kuipenda wala kuikubali ccm. Pita sehemu yenye kampeni uone ccm imeachiwa goli wazi lakini haina watu kabisa. Hata muifanyie cdm hila za wazi kiasi gani haimanishi watu walioikinai ccm wataikubali. Sana sana mtaishia kununua viongozi mkindhani hao viongozi watuvuta watu. Hao viongozi wa cdm mnaowanunua, hata mimi siwashauri kuacha hela za mabwege wanaolazimisha kupendwa.
 
Upuuzi tu.Chadema watakuwa walikodi nyumba ya mtu na wameamua kuhama sasa wewe unalazimisha hata wakihamisha ofisi waneno wayaache mwenye nyumba afute mwenyewe?
Wanahamia wapi uncle, maana Chadema ni taasisi wanapohama tunayo haki ya kujua wapi wamehamia
 
Ni hivi cdm ipo na hata mkiifuta kwa hila, bado watu hawawezi kuipenda wala kuikubali ccm. Pita sehemu yenye kampeni uone ccm imeachiwa goli wazi lakini haina watu kabisa. Hata muifanyie cdm hila za wazi kiasi gani haimanishi watu walioikinai ccm wataikubali. Sana sana mtaishia kununua viongozi mkindhani hao viongozi watuvuta watu. Hao viongozi wa cdm mnaowanunua, hata mimi siwashauri kuacha hela za mabwege wanaolazimisha kupendwa.
kwahiyo lazaro naye kala mpunga? kweli hakuna upinzani hata wwe nakuona unaroho ya ccm
 
kwahiyo lazaro naye kala mpunga? kweli hakuna upinzani hata wwe nakuona unaroho ya ccm

Lazaro kala mpunga kitambo na mwenzake Joshua Nassari, huyo Lazaro alikuwa anaona aibu kuondoka.
 
Lazaro kala mpunga kitambo na mwenzake Joshua Nassari, huyo Lazaro alikuwa anaona aibu kuondoka.
bado rafikiyake na lazaro ambaye ni lema karibuni atarudi home naye
 
Upuuzi tu.Chadema watakuwa walikodi nyumba ya mtu na wameamua kuhama sasa wewe unalazimisha hata wakihamisha ofisi waneno wayaache mwenye nyumba afute mwenyewe?
Inawezekana hujasikia walichokuwa wanakisema hao vijana kwenye video!
 
Kwa hiyo Akili yako inakwambia na Chadema itakuwa imefutika ktk Mioyo ya Raia !?
 
Back
Top Bottom