CCM yeteka kwa mabavu ofisi za CHADEMA Rombo

CCM yeteka kwa mabavu ofisi za CHADEMA Rombo

Waasisi wa CHADEMA walikuwa na maono ya kuwa chama mbadala kwa sera. Baadaye kikavamiwa na magenge ya wapiga deals na watetezi wa mabeberu! Ona sasa ni aibu! Lowassa kawakimbia na hajulikani alipo! Madiwani, wabunge woote nduki. Wamebaki masalia choka mbaya!
Ninakubaliana kwa kiwango kikubwa na angalizo lako!

Makosa waliyoyafanya CHADEMA mwaka 2015 yanawatafuna!
 
Madiwani 201 na wabunge 20 mbona wachache sana, tulianza kuikubali cdm ikiwa na wabunge watano. Hiyo cdm hata akiondoka Mbowe au yoyote yule na cdm ikafutwa juu, bado hakuna uwezekano tuikubali ccm. Tumeshaamka siku nyingi sana. Ccm kilikwisha kupoteza mvuto, saa hii inabidi kitumie mabavu tu kufanya siasa. Hiyo ccm sasa hivi ni kama mziki wa hizi nazo, wengi wanaosikiliza ni wazee, lakini cdm ni kama mziki wa kizazi kipya ndio chenye mvuto.

Mlichokosea ni kuchagua viongozi wasio na akili
Zama zinabadirika na sela zinabadirika
Enzi zile wananchi walikuwa hawaikubali kabisa serikali kwakuwa ilikuwa dhaifu, ndo maana waliwasupport
Mlivyoingia awamu hii ambapo wananchi wako upande wa serikali mlitakiwa muwe upande wa wananchi
Icho ndo kilichowauwa

Mi ni mwananchi wa kawaida, sikukatazi ufikirie kuwa chama chako kiko hai
 
Nimeshangaa kuona baadhi ya Watanzania/wanaCHADEMA wakizifunga ofisi za CHADEMA na kufuta nembo ya maandishi yanayokitambulisha CHADEMA kwenye kuta za nyumba.

Kinaendelea kitu gani nchini mpaka ofisi za CHADEMA zinafungwa na kufutwa maandishi yanayokitambulisha ukutani?

Kilichonishangaza zaidi haya yanatokea katika jimbo la Rombo mkoani Kilimanjaro kama ambavyo wahusika wanajitambulisha.

Video ya tukio
View attachment 1267947
Sidhani kama CHADEMA wana majumba ya kwao ambayo wameyafanya ofisi wakati hata Makao Makuu hakuna jumba la chama kiofisi.

Yawezekana kukosekana kwa ofisi ikawa moja ya sababu ya kuenguliwa kwa wagombea wao kwani huenda fomu zilijazwa nyumbani kwa wagombea na kuwasilishwa bila mihuri. Kwani kutokuwepo kwa ofisi, mihuri itatunzwa wapi kama siyo nyumbani kwa kiongozi mhusika!

Matumizi ya RUZUKU, iwe moja ya agenda kuu wakati wa chaguzi za ndani za chama nchini kote.
 
Mlichokosea ni kuchagua viongozi wasio na akili
Zama zinabadirika na sela zinabadirika
Enzi zile wananchi walikuwa hawaikubali kabisa serikali kwakuwa ilikuwa dhaifu, ndo maana waliwasupport
Mlivyoingia awamu hii ambapo wananchi wako upande wa serikali mlitakiwa muwe upande wa wananchi
Icho ndo kilichowauwa

Mi ni mwananchi wa kawaida, sikukatazi ufikirie kuwa chama chako kiko hai

Unachekesha walionuna, kipimo cha kujua wananchi kama wako upande wa ccm/serikali ni kuheshimu uchaguzi na sio kufanya ukatili na uhayawani wa wazi kwenye chaguzi. Chini ya awamu hii ya tano chaguzi zimeacha box la kura likibakwa kimacho macho. Katika mazingira haya unapimaje kukubalika kwa serikali? Kuwatia wananchi hofu na kutaka waamini kile tu wanacholishwa na serikali ndio kipimo cha kukubalika?

Ngoja nikupe mfano wa timu za simba na Yanga, umeona washabiki na wanachama wake, wote wako kwa mapenzi yao na hakuna matumizi yoyote ya vyombo vya dola au hujuma zilizowapatia hizo timu mashabiki na wanachama wao. Ili ccm/serekali ipime kukubalika kwake ilipaswa iache uhuru wa watu kuchagua kama simba na Yanga zinavyopata wanachama na washabiki wake.
 
Sina ufaham na mambo ya uchaguzi, kama ni kuigiza ama vipi, ila nachojua ni katika mazingira niishipo watu hawaiamini CHADEMA tena
 
Sidhani kama CHADEMA wana majumba ya kwao ambayo wameyafanya ofisi wakati hata Makao Makuu hakuna jumba la chama kiofisi.

Yawezekana kukosekana kwa ofisi ikawa moja ya sababu ya kuenguliwa kwa wagombea wao kwani huenda fomu zilijazwa nyumbani kwa wagombea na kuwasilishwa bila mihuri. Kwani kutokuwepo kwa ofisi, mihuri itatunzwa wapi kama siyo nyumbani kwa kiongozi mhusika!

Matumizi ya RUZUKU, iwe moja ya agenda kuu wakati wa chaguzi za ndani za chama nchini kote.

Kama cdm ilikuwa hivyo je vyama vingine vya upinzani nao mbona walienguliwa? Ngoja nikupe ukweli usizunguke kutaka kupoteza ukweli. Ni hivi, kinachoendelea kwenye siasa za nchi yetu ni tabia binafsi za rais kwenye siasa za ushindani. Yeye hana uwezo wa siasa za ushindani toka zamani hata akiwa mbunge, angalia hata historia yake alikuwa hashindi kwa box la kura bali figisu. Tabia yake hiyo binafsi ndio kahamishia kwenye mfumo wa nchi nzima, kutokana na katiba yenye mapungufu makubwa yanayomuwezesha kufanya chochote na kuamrisha chochote bila kuhojiwa.

Kwa ujumla hawezi siasa za ushindani, na sasa anadhani anafanya jambo la maana kuua upinzani kwa faida yake binafsi na watu wanamuangalia, lakini atapandikiza kansa ambayo italitafuna taifa hili muda mrefu. Zaidi ya nusu ya viongozi wa ccm kwenye hizi serikali za mitaa wamepita kwa kutoa rushwa, kisha yeye ametumia madaraka yake kuwapitisha ili ionekane ccm yake inakubalika kitu ambacho sio kweli. Matokeo yake tutakuwa na viongozi wengi wala rushwa huko mitaani wakati yeye hawezi kuwadhibiti kwani kaua mfumo wa check & balance. Ukweli wa kuwa hawezi kudhibiti wizi na rushwa nchi hii zaidi ya kufanya siasa, angalia kwenye ziara zake zote alikutana na wizi wa kutisha, na hivi majuzi wizi wa pesa za korosho. Bakini mnashangilia siasa za kishenzi huku utawala wa mifumo ukiharibiwa na mtu mmoja anayesaka sifa binafsi, na kuweka viongozi wala na watoa rushwa bila ridhaa ya wananchi.
 
Hata kama ni moja ni aibu kwa chama, maana hiyo moja inaweza kusababisha zingine nazo zifungwe. Kumbuka, alianza kutoka diwani mmoja sasa wamefika 201. Alianza kutoka mbunge mmoja sasa wamefika 20!
Hata ungekuwa wewe ungefanyeje kama ukigundulika tu kuwa wewe ni mpinzania unapigwa risasi, unaharibiwa mashamba yako, polisi wanashinda nyumbani kwako wakipekua hapa na pale, unaswekwa rumande, unaburuzwa mahakamani kila siku. Kwa maoni yangu bora wapinzani waache siasa, waendelee na shughuli zingine ili turudi kwenye ukoloni wa chama kimoja. Hata kama tutaanza kupigwa viboko kama zana z ukoloni sawa tu. Mpaka hapo nawasifu sana wapinzani kwa roho ngumu ya kuvumilia mateso.
 
Sina ufaham na mambo ya uchaguzi, kama ni kuigiza ama vipi, ila nachojua ni katika mazingira niishipo watu hawaiamini CHADEMA tena

Unapima vipi watu kutokuwakubali hao cdm wakati kipimo cha kwanza cha kukubalika ni uchuguzi huru na haki? Kama watu hawaruhusiwi kufanya siasa na uchaguzi ukifika zinafanyika hujuma za wazi wazi, hapo unajuaje kukubalika au kutokukubalika kwa chama? Na hakuna popote katika nchi hii chama chochote kinakubalika na watu wote, hivyo sishangai hayo ya mtaani kwenu, ila ujue mtaa wenu sio Tanzania.
 
Sina ufaham na mambo ya uchaguzi, kama ni kuigiza ama vipi, ila nachojua ni katika mazingira niishipo watu hawaiamini CHADEMA tena
Sasa kama watu hawaiamini CHADEMA mbona mnawazuia wagombea wao? Si mngewaacha tu ili waanguke kwenye kura? Mtu ambaye haaminiki unamwogopa wa nini kwenye sanduku la kura?
 
Kwa nini ofisi moja ikifutwa nembo unatumia lugha ya wingi kuwa ofisi zinafutwa nembo na kufungwa?Wewe ni pandikizi tawi la JF?
 
Actual itikadi na imani ya mtu kwa chama chake inaendana jinsi mtu anavyo ikubali mikakati na sera za chama chake na watu wengi hatuamini kwenye muonekano wa vitu nikuwa kama mtu anaimani na sera za chama chake hata chama husika kikifa hataweza kukichagua chama kingine kuwa mbadala. Mie sijawahi kuwa na unasaba na ccm na haitatokea kwa sababu ya tabia zao chafu za ufisadi mkubwa ambao uliigharimu pakubwa maendeleo nchi yetu.

Hatabyanayofanyika sasa hatuitaji kujigamba nayo kwasababu yalitakiwa kufanyika miaka 50 iliyopita. Ila chama kilichokuwa kinaongoza kililea wezi na mafisadi na hadi leo tunayaona mafisadi bado yanajidai mitaani bila hata ya hofu

So chadema iko ndani ya mioyo ya watu na sio muonekano wa vitu.
 
Miaka 40 ijayo wajukuu wetu wanahoji: "Hivi babu mlikuwa mnaambiwa hakuna mikutano na nyie mnafyata mkia,Wenzenu wanabambikiwa kesi na nyie mnafyata mkia,wanapita bila kupingwa hata hamthubutu kuandamana.Eti Nasikia mlikuwa na vyama zaidi ya 10 lakini hamuungani.Nasikia CUF na Chadema wakiunga juhudi wakaingia ccm wanateuliwa mara moja halafu wafia chama ccm hamna la kufanya?"

Sasa mjukuu wangu ulitaka tufanyeje?
 
Kwani hujui, Wagombea wao hawakutaka wasuse uchaguzi wa serikali za mitaa lakini viongozi wao wa juu wamefanya maamuzi yao binafsi na wao wameamua kufuta jina la chama ili wao wabakie na makao makuu yao.
Mimi najiuliza, kama wameweka mpira kwapani uchaguzi wa serkali za mitaa na mitaa yote ikachukuliwa na CCM, sasa uchaguzi wa madiwani na ubunge wataushindaje?

Kupata diwani au mbunge 2020 wategemee sana huruma ya CCM. La sivyo tutashuhudia bunge la chama kimoja.
 
Huu uhuni ndio mnauita uchaguzi. Ujinga huu mnaoufanya ukitupeleka ile njia ya Zimbabwe mtapata faida gani. This is very silly.
 
Sasa kama watu hawaiamini CHADEMA mbona mnawazuia wagombea wao? Si mngewaacha tu ili waanguke kwenye kura? Mtu ambaye haaminiki unamwogopa wa nini kwenye sanduku la kura?

Kuniquote na kuniandikia kama mi ni mwanachama wa CCM ni kunikosea mkuu
Mi ni binadam wa kawaida asie na upande wa chama ata uchaguzi uliopita sikufanya uchaguzi kutokana na folen kuwa kubwa,
Ila ninaongea ninachoona, na CHADEMA hawakucheza karata vizuri kitu kinachonifanya nijiulize uwezo wao wa kufikiri

Mambo ya uchaguzi ni mengi, na kuna mengi nyuma ya pazia,
Kama we ni mtu mwenye akili timamu kila kitu kichukulie in probabilities, yawezekana na pia yawezekana ni mpango
 
Ningekuwa siyo mwana SISIEMU ningekuuliza kwenye karatasi ya kula inawekwa sura na bendera au sura na nembo ya hao vibaraka wa MABEBERU?
Ila kwasababu ni mwanachama wa SISIEMU sito kuuliza, nakuacha kama ulivyo.
 
Back
Top Bottom