MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,996
Ninakubaliana kwa kiwango kikubwa na angalizo lako!Waasisi wa CHADEMA walikuwa na maono ya kuwa chama mbadala kwa sera. Baadaye kikavamiwa na magenge ya wapiga deals na watetezi wa mabeberu! Ona sasa ni aibu! Lowassa kawakimbia na hajulikani alipo! Madiwani, wabunge woote nduki. Wamebaki masalia choka mbaya!
Madiwani 201 na wabunge 20 mbona wachache sana, tulianza kuikubali cdm ikiwa na wabunge watano. Hiyo cdm hata akiondoka Mbowe au yoyote yule na cdm ikafutwa juu, bado hakuna uwezekano tuikubali ccm. Tumeshaamka siku nyingi sana. Ccm kilikwisha kupoteza mvuto, saa hii inabidi kitumie mabavu tu kufanya siasa. Hiyo ccm sasa hivi ni kama mziki wa hizi nazo, wengi wanaosikiliza ni wazee, lakini cdm ni kama mziki wa kizazi kipya ndio chenye mvuto.
Sidhani kama CHADEMA wana majumba ya kwao ambayo wameyafanya ofisi wakati hata Makao Makuu hakuna jumba la chama kiofisi.Nimeshangaa kuona baadhi ya Watanzania/wanaCHADEMA wakizifunga ofisi za CHADEMA na kufuta nembo ya maandishi yanayokitambulisha CHADEMA kwenye kuta za nyumba.
Kinaendelea kitu gani nchini mpaka ofisi za CHADEMA zinafungwa na kufutwa maandishi yanayokitambulisha ukutani?
Kilichonishangaza zaidi haya yanatokea katika jimbo la Rombo mkoani Kilimanjaro kama ambavyo wahusika wanajitambulisha.
Mlichokosea ni kuchagua viongozi wasio na akili
Zama zinabadirika na sela zinabadirika
Enzi zile wananchi walikuwa hawaikubali kabisa serikali kwakuwa ilikuwa dhaifu, ndo maana waliwasupport
Mlivyoingia awamu hii ambapo wananchi wako upande wa serikali mlitakiwa muwe upande wa wananchi
Icho ndo kilichowauwa
Mi ni mwananchi wa kawaida, sikukatazi ufikirie kuwa chama chako kiko hai
Unachekesha walionuna, kipimo cha kujua wananchi kama wako upande wa ccm/serikali ni kuheshimu uchaguzi na sio kufanya ukatili na uhayawani wa wazi kwenye chaguzi. Chini ya awamu hii ya tano chaguzi zimeacha box la kura likibakwa kimacho macho. Katika mazingira haya unapimaje kukubalika kwa serikali? Kuwatia wananchi hofu na kutaka waamini kile tu wanacholishwa na serikali ndio kipimo cha kukubalika?
Ngoja nikupe mfano wa timu za simba na Yanga, umeona washabiki na wanachama wake, wote wako kwa mapenzi yao na hakuna matumizi yoyote ya vyombo vya dola au hujuma zilizowapatia hizo timu mashabiki na wanachama wao. Ili ccm/serekali ipime kukubalika kwake ilipaswa iache uhuru wa watu kuchagua kama simba na Yanga zinavyopata wanachama na washabiki wake.
Sidhani kama CHADEMA wana majumba ya kwao ambayo wameyafanya ofisi wakati hata Makao Makuu hakuna jumba la chama kiofisi.
Yawezekana kukosekana kwa ofisi ikawa moja ya sababu ya kuenguliwa kwa wagombea wao kwani huenda fomu zilijazwa nyumbani kwa wagombea na kuwasilishwa bila mihuri. Kwani kutokuwepo kwa ofisi, mihuri itatunzwa wapi kama siyo nyumbani kwa kiongozi mhusika!
Matumizi ya RUZUKU, iwe moja ya agenda kuu wakati wa chaguzi za ndani za chama nchini kote.
Hata ungekuwa wewe ungefanyeje kama ukigundulika tu kuwa wewe ni mpinzania unapigwa risasi, unaharibiwa mashamba yako, polisi wanashinda nyumbani kwako wakipekua hapa na pale, unaswekwa rumande, unaburuzwa mahakamani kila siku. Kwa maoni yangu bora wapinzani waache siasa, waendelee na shughuli zingine ili turudi kwenye ukoloni wa chama kimoja. Hata kama tutaanza kupigwa viboko kama zana z ukoloni sawa tu. Mpaka hapo nawasifu sana wapinzani kwa roho ngumu ya kuvumilia mateso.Hata kama ni moja ni aibu kwa chama, maana hiyo moja inaweza kusababisha zingine nazo zifungwe. Kumbuka, alianza kutoka diwani mmoja sasa wamefika 201. Alianza kutoka mbunge mmoja sasa wamefika 20!
Sina ufaham na mambo ya uchaguzi, kama ni kuigiza ama vipi, ila nachojua ni katika mazingira niishipo watu hawaiamini CHADEMA tena
Sasa kama watu hawaiamini CHADEMA mbona mnawazuia wagombea wao? Si mngewaacha tu ili waanguke kwenye kura? Mtu ambaye haaminiki unamwogopa wa nini kwenye sanduku la kura?Sina ufaham na mambo ya uchaguzi, kama ni kuigiza ama vipi, ila nachojua ni katika mazingira niishipo watu hawaiamini CHADEMA tena
Mimi najiuliza, kama wameweka mpira kwapani uchaguzi wa serkali za mitaa na mitaa yote ikachukuliwa na CCM, sasa uchaguzi wa madiwani na ubunge wataushindaje?Kwani hujui, Wagombea wao hawakutaka wasuse uchaguzi wa serikali za mitaa lakini viongozi wao wa juu wamefanya maamuzi yao binafsi na wao wameamua kufuta jina la chama ili wao wabakie na makao makuu yao.
Huu uhuni ndio mnauita uchaguzi. Ujinga huu mnaoufanya ukitupeleka ile njia ya Zimbabwe mtapata faida gani. This is very silly.Mimi najiuliza, kama wameweka mpira kwapani uchaguzi wa serkali za mitaa na mitaa yote ikachukuliwa na CCM, sasa uchaguzi wa madiwani na ubunge wataushindaje?
Kupata diwani au mbunge 2020 wategemee sana huruma ya CCM. La sivyo tutashuhudia bunge la chama kimoja.
Sasa kama watu hawaiamini CHADEMA mbona mnawazuia wagombea wao? Si mngewaacha tu ili waanguke kwenye kura? Mtu ambaye haaminiki unamwogopa wa nini kwenye sanduku la kura?
CHADEMA haijawahi kunyimwa ruzuku za kuendesha chama!..... mnawanyima ruzuku ya kuendeshea shughuli za chama chao, halafu unakuja hapa na viswali vyako vya kitoto!
Tokea uchaguzi mkuu umalizike ofisi yetu ya kata hapa njombe imefungwa haijafunguliwa wanachama tumeshindwa kupata huduma.
View attachment 1268051
SOURCE:Mbowe tusaidie ukarabati wa ofisi