Zanzibar haina mzawa halisi, wengi Pale ni wakongo wanaojiita wakati wanayamwezi.
Kile ni Kisiwa hakuna Mfugaji angeweza kukimbilia Kwenye Kisiwa badala ya kuishi bara .
Maalim Seif akiwa Rais tutakua tumepiga hatua kubwa sana na kujenga utu.
Ni kweli kabisa CCM ya Zanzibar na bara pia imejenga mfumo wa watu wenye Roho mbaya sana sana na ukatili wa kupindukia . Hali inayopelekea watu kuishi kwa kuwaziana visasi na kuombeana dua mbaya.
Waislama wa Kweli wafikirie pia kuhusu Kesho ahera kuliko kuwaza Urais tuu na kupata madaraka utafikiri wataishi milele.
Kwa nini nchi yenye watu wa imani moja kama Zanzibar wanaishi kwa dhulma kiasi hicho?
Mnasababisha watu washindwe kuupenda uislama ,dini inayesemwa kuwa ni dini ya Mwenyezi Mungu.
Kweli kabisa ni aibu kubwa wanasiasa kuwajengea watu Roho za dhulma kwa sababu ya vyama vya siasa na waumini wa dini moja wanakubali kuishi hivyo kwa sababu tu ya madaraka na kupata fedha.
Mnaabisha sana kwa kweli. Tumeona Muislama kabisa anaswali swala tano lakini anakubali kupindua matokeo ya kura na ijumaa anaswali na anajiona ni muumini wa dini inayojiita ya haki.
Shame on you!! Simamisheni haki duniani kama mlivyosoma kwenye dini vinginevyo mjiite wamataifa tu wasiomjua Mwenyezi Mungu na dini ya haki.
Kadhalika Wakristo viongozi Wote na wasimamizi wa uchaguzi ujao wamuige Mh. Magufuli amabaye amejinyenyekeza kwa Mungu na kujua kuwa Taifa linahitaji Rehema na kumtii Mungu hasa kipindi cha Korona. Tuendelee kumtii Mungu wakati wote na kutenda haki.
CCM wamsimamishe yeyote lakini haki itendeke na Zanzibar iwe Mbele ya maslahi ya watu na vyama.
Watu wachache waliopewa jukumu la kusimamia uchaguzi wasijione kuwa wao ndio kila kitu na hakuna aliye juu yao duniani na hata mbinguni.
Hata Shetani ni mbaya lakini anamuogopa Mwenyezi Mungu. Awamu hii Tume ya uchaguzi Zanzibar isilipake Matope taifa letu. Watu wachache wasiwawekee mazingira magumu ya kuishi wazanzibari wasio na hatia kwa sababu tu wanataka kukalia kiti cha Urais.
Wanataka nini Ikulu kwa nguvu zote hizo. Ni kweli ni kuwatumikia watanzania tu au kuna kingine?
Nitashangaa kuona Mtu amekua Waziri miaka 25 lakini bado anavuruga uchaguzi au anafanya njama za ushindi.
Uchaguzi wa haki uheshimiwe na wote. Lakini dhulma isikubalike kuwa ndiyo maisha ya waafrika muda wote.
Miaka 25 za uchaguzi Zanzibar inatosha kwa CCM kujiandaa kushirikiana na vyama vingine na kuwaachia nafasi ya kuongoza na wao wakashika umakamu.
Ni jambo baya sana kwa wachache kujiona ni haki yao kuwa na maisha maziri na ya anasa kupitia dhulma.
Mungu Ibariki Tanzania Bara na Visiwani pia.
Kwani pia Maalim Seif Sharrif ukimfuatilia Kiundani kabisa Ndugu hasa Chimbuko lake unadhani ni Mtanzania halisi kama tulivyo Mimi na Wewe?