CCM Zanzibar yamfuta uanachama Balozi Ali Karume

CCM Zanzibar yamfuta uanachama Balozi Ali Karume

Halmshauri Kuu Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kusini Unguja imemfuta uanachama kada wake Balozi Ali Karume.

Kikao cha kumfuta uanachama Balozi Karume kimefanyika saa saba usiku wa kuamkia leo Jumamosi Julai 8, 2023 chini ya Katibu wa Mkoa wa CCM Amina Mnacho.

Taarifa ya kumuondosha kwenye chama hicho ilitolewa na Katibu Mwenezi wa Mkoa huo, Ali Timamu Haji.

Hatua hiyo inakuja baada ya chama hicho kumpa onyo kutoka na kauli zake zake akidaiwa kukidhalilisha chama na kuwatukana viongzi wakuu hadharani.

Source: Mwananchi
 
Aende ACT Wazalendo kuendeleza siasa zake za kukinyuka chama cha mapinduzi. Huyu balozi ni shujaa, hakuogopa jitu kubwa ccm kulipa za uso
 
shida ya balozi ajakubali kutesa kupokezana zama za karume zimefikia tamati mtunnze mlichonacho sio kila appointment tuwakute kina karume maisha hayaendi hivi hata kaama kuwakumbuka wakumbukwe wakina baba mdogo mjomba shangazi watoto wao akijikubali angekula mema ya nchllll
 
Ni lini alianza kuwa mwanachama halali wa CCM?

Je tuhuma za Balozi jarume kuhusu wizi wa Kura unaoratibiwa na CCM ni wa kweli?
Asanteni
 
Back
Top Bottom