Halmshauri Kuu Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kusini Unguja imemfuta uanachama kada wake Balozi Ali Karume.
Kikao cha kumfuta uanachama Balozi Karume kimefanyika saa saba usiku wa kuamkia leo Jumamosi Julai 8, 2023 chini ya Katibu wa Mkoa wa CCM Amina Mnacho.
Taarifa ya kumuondosha kwenye chama hicho ilitolewa na Katibu Mwenezi wa Mkoa huo, Ali Timamu Haji.
Hatua hiyo inakuja baada ya chama hicho kumpa onyo kutoka na kauli zake zake akidaiwa kukidhalilisha chama na kuwatukana viongzi wakuu hadharani.
Source: Mwananchi