CDC Africa: Vipimo vya Corona Virus vinavyotumika Tanzania vinafanya kazi vizuri

CDC Africa: Vipimo vya Corona Virus vinavyotumika Tanzania vinafanya kazi vizuri

Hizi Test Kits za Covid-19 zilitoka China kama msaada uliotolewa na tycoon Jack Maa kusaidia nchi za Kiafrika katika kupambana na Covid-19. CDC ndo walipewa jukumu la kusambaza hizo Kits kwa nchi za Kiafrika.
Je, inakuwaje Tanzania peke yake ndo wawe na Kits fake/defective?
Lakini pia kama ingelikuwa ni nji insyoongozwa na mtu makini Serikali walipaswa kupeleka SAMPLES zenye Utata kwa jirani zao wenye Kits Kama hizo kujiridhisha k.m. Kenya,Uganda, Rwanda, RSA n.k kuliko KUANZA kupayuka hadharani....!!!!!

Such thinking is equally nice but remember also there is that lonely perspective of Jesus or a drunkard, let's encourage diversity in opinion and thinking
 
I care less of what they say, i thank God after so many decades we have a true son of Africa and good enough he is a capitalist too

You must be really joking....!!
Magufuli?The same Magufuli I know being a true son of Africa?
What gonna you say about the following:
  1. Mwl. J.K.Nyerere-rip(Father of our nation).
  2. Sheikh Aman Abeid Karume(rip)1st presida Zanjbar.
  3. Nelson Honlala Mandela(rip)-1st Black presida to RSA.
  4. Kwame Nkhruma(rip)-Ghana.
  5. Patrice Lumumba (rip)-1st PM-DRC.
  6. Samora Moises Machel(rip)-Mocambique 1st Presida.
  7. etc!
 
You must be really joking....!!
Magufuli?The same Magufuli I know being a true son of Africa?
What gonna you say about the following:
  1. Mwl. J.K.Nyerere-rip(Father of our nation).
  2. Sheikh Aman Abeid Karume(rip)1st presida Zanjbar.
  3. Nelson Honlala Mandela(rip)-1st Black presida to RSA.
  4. Kwame Nkhruma(rip)-Ghana.
  5. Patrice Lumumba (rip)-1st PM-DRC.
  6. Samora Moises Machel(rip)-Mocambique 1st Presida.
  7. etc!
Ur entitled to ur opinion, may I equally and frankly open another version of sons and daughters of Africa, am buzzing up not to be rigid, may you agree to disagree
 
Where are
PhD holders
Professors

Ndo nimegoma kurud shule mpaka leo..Bora nibakie na kaelimu kangu..nitafute hela tu

Sent using Jamii Forums mobile app

There's only one PhD holder and Professor in Tanzania. His Excellency Dr. John Joseph Pombe Magufuli!
The rest of them graduands must listen dearly and carefully from Chatoo!
 
Ur entitled to ur opinion, may I equally and frankly open another version of sons and daughters of Africa, am buzzing up not to be rigid, may you agree to disagree
Agree to disagree.....!!!🤣🤣
Can you please elaborate this kind of an odd statement?
 
Hizi Test Kits za Covid-19 zilitoka China kama msaada uliotolewa na tycoon Jack Maa kusaidia nchi za Kiafrika katika kupambana na Covid-19. CDC ndo walipewa jukumu la kusambaza hizo Kits kwa nchi za Kiafrika.
Je, inakuwaje Tanzania peke yake ndo wawe na Kits fake/defective?
Lakini pia kama ingelikuwa ni nji insyoongozwa na mtu makini Serikali walipaswa kupeleka SAMPLES zenye Utata kwa jirani zao wenye Kits Kama hizo kujiridhisha k.m. Kenya,Uganda, Rwanda, RSA n.k kuliko KUANZA kupayuka hadharani....!!!!!
Ulichosema ni sahihi kabisa; na ndio maana hata argument ya Magu inaonakena kiroja kutokana na njia aliyotumia!
Angetumia njia muafaka, leo hii angekuwa appraised kila mahali!

Kinyume chake, eti leo wanaunda tume kukagua kits na wafanyakazi... tume yenyewe ya kwao wenyewe! Nani atatoa matokeo yanayoweza kumkasirisha mfalme! Ndo yale yale ya akina Mruma na Makinikia, na mwisho kuibuka na kiroja cha kudai 425 trilioni, na hadi kesho hata senti 5 haijatoka!
 
Hili jamaa la Africa CDC bonge la dunderhead!

Unajuaje hakuna manufacturing defect ?

Hata ukinunua gari jipya Japan, zero mileage, halafu ukawapigia simu baada ya wiki mbili kwamba gari lenu bovu, hawawezi kukubishia "hilo gari ni zima!!!!

Wakati wewe consumer ndio unacho chombo mkononi na una experience chombo kibovu!
But how many ? Nchi ngapi za afrika zimelalamikia vifaa mpaka sasa? Well ni tz tu.
Inamaana vya wenzetu ni.orijino vyetu fake...?

Si kazi yake kukagua defective medical device. Tuna mamlaka zetu hapa.zimejaa wataalam. Wao wako tu kama watazamaji wkt wangetakiwa wahusike.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata ingekuwa mimi ninge reject pia.
Hivi kweli mtu unaweza kwenda porini kukimbizana na kware ili upate sample ya kuwategeshea lab technicians! Hivi mapapai na mafenesi na kipimo cha RNA ya kirusi cha Corona wapi na wapi. Hii quality assurance na quality control ya wapi?

Yaani wenzetu wako busy kupambana na ugonjwa kwa kuchukua decisive measures. Sisi tunapima mbuzi, kondoo na mafenesi.
Sad but tunaonekana fools uko nje. Till today najiuliza was it necessary kufanya hayo.. au anatafuta watu wa kuwadondoshea lawama baada ya kuona meli inamshinda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
There's only one PhD holder and Professor in Tanzania. His Excellency Dr. John Joseph Pombe Magufuli!
The rest of them graduands must listen dearly and carefully from Chatoo!
To be honestly Dr.magufuli is not a professor.
And not the only person with PhD holder in africa.
A lot of leaders and non-gov leadears in afrca has phd.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona alikuwa wazi tuu alisema kuna jambo haliko sawa. Pengine wataalamu au vifaa au kuna jambo bado halijagundulika. Na jambo lililofanyika ni la kisayansi kabisa.
 
Ila kuna watu ni mizigo ya haja kabisa.

Jiwe pamoja na PhD koko ya UDSM bado kichwa kimejaa uozo, hajastaarabika kabisa.

Elimu imedunda kabisa
Wewe PhD yako ni ya chuo gani ??
 
I got your point, but people are still sick and dying, whats the cause?
That was the point of doing the investigation, they're trying to look for a root cause. The machines could be faulty, may be there was a plot to sabotage the image of the country, some of the test kits could have been deliberately infected, there are a lot of questions to be answered.
 
Tatizo Rais wetu haoni shida ofisi kupotezewa heshima?

Yeye angeyaacha haya mambo kwa wataalam wanasayansi. Yeye siyo mwanasayansi. Kama ana mashaka yoyote, alistahili kueleza mashaka yake kwa wanasayansi. Wanasayansi ndiyo wangeifanya kazi ya quality control and analysis. Kosa kubwa ni pale Rais anapofikiria kuwa TISS wanaweza kumpa majibu ya uhakika. TISS wengi tunawafahamu, siyo wanasayansi. Wengine hata hawastahili kuwepo huko TISS. Wameigeuza kazi ya Intelligence kuwa sawa na umbea/majungu.

Rais Magufuli amesoma masomo ya Sayansi lakini hajawahi kuwa mwanasayansi.

Tangu amalize PhD yake, hajawahi kuingia maabara kufanya study yoyote ya Sayansi, hajawahi kushiriki conferences zozote za kisayansi ambazo huelezea maendeleo katika fani mbalimbali za Sayansi, hajawahi kushiriki kufanya research zozote za Sayansi.

Kimsingi, yeye ni mwanasiasa. Muda wake mwingi wa maisha yake umeutumia kwenye siasa. Ni mwansiasa kuzidi hata waliosomea masomo ya siasa ambao hawajawahi kufanya siasa.

Ni kosa kubwa kufikiria kuwa ukisomea masomo tu ya sayansi, basi wewe ni mwanasayansi au ukisomea tu masomo ya sheria basi umekuwa mwanasheria, japo unakuwa na advantage ndogo ya uelewa yakiwa yanaongelewa mambo ya fani ambayo masomo ya fani hiyo ulipata kuyasoma.

Rais ni mwanasiasa. Anashinda anaongea siasa, anawaza siasa, analala akiota siasa. Huyu ni mwanasiasa. Asisahau kuwa kuna watu ni wanasayansi, kuna watu ni wataalam wa maabara. Wanashinda kwenye maabara, mazungumzo yao karibia yote yanahusu mambo ya maabara, semina na conferences zote wanazohudhuria, zinahusu maabara, makala nyingi wanazosoma zinahusu maabara, hawa ni wataalam wa maabara.

Vifaa vya maabara havinunuliwi kama mashati. Mtengenezaji wa vifaa vya maabara ili vifaa vyake viweze kufanya kazi iliyokusudiwa, hufanyiwa majaribio, na huidhinishwa na WHO. Kama kweli kuna hitilafu ya uwezo wa vifaa vinavyotumika maabara yetu ya Taifa, wa kwanza tunaotakiwa kuwashutumu ni WHO ambao wameruhusu vifaa hivyo vitumike. Wengine wanachanganya kati ya vifaa vya maabara kwaajili ya kupima Covid 19 na quick test kits za Covid 19. Kuja baadhi ya nchi wamelalamikia quick test kits LAKINI siyo vipimo vya maabara kama hiki tunachokilalamikia sisi. Sasa wewe kulalamikia kitu ambacho hakijaonesha hitilafu sehemu nyingine yoyote, unastahili kufanya scientific tests hasa, na hizi za kuoima mafenesi na kwale wakati mtengenezaji hajaeleza kama kifaa hicho kinaweza kupima hivyo vitu.

Huwezi kwenda kuilaumu WHO kwa namna alivyofanya Rais wetu. Kulistahili kufanyika detailed scientific studies kuweza kuzidisqualify idara za WHO zilizoidhinisha kutumika kwa vifaa hivi.

The whole approach to this matter has been disgracefully wrong. Mwisho wa yote ni aibu kwa Rais wetu na kwa Taifa kwa ujumla.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwanza, rais wetu amasumbuliwa na ugonjwa wa wanasiasa wengi wa Tanzania. Ugonjwa huo ni kuwakosoa wataalam na kuwanyong'onyeza kila wamapopata nafasi. Wengi watakumbuka enconter ya rais na yule mhandisi kule Dodoma. Pili, rais wetu amesoma chemistry na ingawa hajaifamyia kazi anaamini yeye ni mwanasayansi nguli. Ndiyo maana bila consultation yoyote alihitimisha chlorine haiwezi kuua virusi! Lakini hata angekuwa mwanasayansi nguli, bado kwa nafasi yako hakustahili kuhitimisha jambo lolote bila ushauri wa kutosha wa kitaalam. Tatu, rais wetu amepungukiwa karama ya uongozi. Sifa moja muhimu ya uongozi ni kusikiliza.
 
Back
Top Bottom