GT
Huko serikalini kuna mambo hayapo sawa hili lipo waazi kabisaa.
Huyu mzee namheshimu sanaa kama naye kafika hatua ya kuongea hivi something is wrong and burning 🔥 inside samia government wazalendo wnapuuzwa
Siyo maji tu yamemwagika. Lakini kwa ufahamu wa kisayansi uliopo sasa; hata hayo maji yangemwagika kweli, leo hii tungeweza kuyazoa na kuyahifadhi..
Bahati mbaya sana kwetu sote, ni damu ya waTanzania imemwagika. Pamoja na teknolojia yooote iliyopo leo hii, kamwe damu hiyo hatuna uwezo wa kuizoa na kurudisha uhai wa waTanzania wenzetu..
Msamaha huu unaoombwa...
Ni dhahiri hakuna aliyejuwa kilichomo moyoni mwa waovu hawa. Sote ni mashuhuda wa hadaa na ulaghai mwingi uliokuwa ukitumika kuaminisha waTanzania kuwa kufuata taratibu za matakwa ya Katiba iliyopo, ndilo jambo pekee lililokuwa sahihi kwa wakati huo.
Nani angejuwa ndani ya watu kama hawa kuna sumu kali ya kuliangamiza taifa hili?
Msamaha ni haki ya waTanzania kuamua kuutoa kama ulivyo ombwa; lakini je; hawa waliopo kwenye nafasi hizo hizo na wanashiriki kwenye maangamizi ya waTanzania nao kuna siku watajitokeza kuja kuomba "wasamehewe?
Maneno ya mhusika; hasa kuhusu hayo maji yanaonyesha uelewa mkubwa wa maswala haya, lakini je, bado na yeye anashikilia nafasi za uteuliwa katika hali ya namna hii iliyopo sasa?
Haya maneno mazuri, pamoja na msamaha ulioombwa ni lazima yashirikishe vitendo vinavyoonyesha msamaha unastahili kutolewa.