CDF mstaafu Mabeyo amelikoroga, Makamu wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais

Chain of command
PRESIDENT >>V. P>>P. M huyo CDF ni mbali Sana anaripoti kwa waziri wa Ulinzi, Inakuwaje top secret ifahamike na CDF halafu VP na PM wasijue?

Pengine mwendazake alihisi kuna wasaliti hivyo akaamua kuvunja chain of command??
CDF anaripoti kwa Waziri wa ulinzi??

Jamani tupumzisheni kidogo.
 
Katiba mpya haijitekelezi yenyewe. Inahitaji watu ili itekelezwe. Hata hii ya sasa haijitekelezi. Inahitaji watu kutekelezwa.

Labda tatizo kuu si katiba. Pengine tatizo la msingi ni watu!

Kama walio na dhamana ya kuitekeleza hii ya sasa hawafanyi ipasavyo, hiyo mpya itawabadilisha hao watu na kuanza kuitekeleza?
 
Katiba mpya haijitekelezi yenyewe. Inahitaji watu ili itekelezwe. Hata hii ya sasa haijitekelezi. Inahitaji watu kutekelezwa.

Labda tatizo kuu si katiba. Pengine tatizo la msingi ni watu!
Constitution vs Constitutionalism.

Unaweza ukawa na Katiba lakini watu wakaipindisha na hakuna kitu venye mtawafanya.

Ukibisha unapigwa rungu la ugoko na vikosi vya usaRama.

Kiufupi bado watanganyika hawana upeo wa kuelewa nini maana ya katiba. Hawa ni mbuzi tu wakiongozwa na KIZIMKAZI mwenye DIVISHENI FOO.
 
There you go! 💯%.
 
Yaani kweli unaona sasa unakufa na una nafasi ya kutubu. Umuite Kiongozi umwachie wosia wa namna ya kuendelea na majukum na uache njia ya kutengeneza njia yako huko uendako? Inashangaza sana.
Angetubu na kufanya mengine Chief, nadhani vyote vingewezekana.
 
Hahah kisa mwanamke sio na bado hamjasema mitano tena kwa mama
 

Tusilaumu tu, twende kwenye uhalisia.

Kuna wakati, hata kwenye familia, nani apewe taarifa kwanza juu ya hali ya mgonjwa kuzorota au kifo, hutegemea zaidi wewe mwenyewe umejiweka karibu kiasi gani na huyo mgonjwa au marehemu.

Kama huwa unaenda kumwangalia mgonjwa kila mara, unapenda kujua hali ya mgonjwa kila mara, wewe ndiye utajulishwa mabadiliko ya hali ya mgonjwa kila mara. Je, Samia akiwa makamu wa Rais alijihusisha kwa ukaribu kiasi gani na hali ya mgonjwa, ndiye ingeamua ataarifiwe mapema kiasi gani. Nadhani taarifa ya kifo cha Magufuli walipewa kwanza watu wale walioonekana kujihusisha kwa ukaribu zaidi na hali ya mgonjwa. Makamu wa Rais alipewa tu taarifa kutokana na nafasi yake.

Ifahamike pia kuwa, katika uhalisia, makamu wa Rais kwa Tanzania ni cheo kisichokuwa na uzito wowote. Ni mtu wa kutumwa. Asipotumwa, anashughulika na masuala tu ya Mwungano na mazingira.
 
Si angemuita mkewe aliokawa hapohapo dar mbona hakumkumbuka?
Boss tunaongele mambo ya Nchi Mzee.....ishu ya mke inakujaje hapa, Yani uwe rais WA Nchi uone kabisa huna pa kutokea uite mkeo, unaniangusha Boss, ukishakuwa na madaraka makubwa kama ya Urais inakuwa Nchi kwanza, mambo ya familia badae.
 
Ni
Ni kweli kuna mambo ambayo kikatiba Rais hawezi kukasimu kwa mtu yeyote.
 
Magufuli aliweza kuagiza Mapadri waende, lakini alishindwa kuagiza aitiwe Makamu wake, hata amuachie wosia juu ya Majukumu anayomuachia, naona bado kuna vumbi halijatuama, nasubiri story zaidi.

Kwa hatua kama hiyo, kilichokuwa muhimu zaidi ilikuwa ni maisha yake ya baadaye, yaani maisha baada ya kifo. Ndiyo maana alitaka zaidi viongozi wa kiroho kuliko mwingine yeyote.

Tunafundishwa kuwa katika ufufuo hakuna hata familia wala ndugu wa damu, wote huwa ni sawa kama alivyo mwingine yeyote.
 
Wabongo bwana ujuaji mwingi Sana

Hivi unadhania mpaka mtu anakuwa CDF ni Jambo simple simple Sana eh

So wewe unajua utaratibu kuliko mkuu wa majeshi?

Tuache kujifanya wajuaji sana

Kwa hali aliyokuwa nayo marehemu wakati huo, ilikuwa ni wakati delicate sana. Hofu ilikiwa kwamba wabaya wake wangeweza kuitumia kummalizia. Ndiyo maana wakuu wa vyombo vya usalama wote walikuwa pale ili kuwa na uhakika kuwa hali yake mbaya ya kiafya haitumiwi na mahasimu wake. Hivyo hata kuwaweka mbali wale wote waliopo kwenye nafasi ya kuyarithi madaraka yake kama angefariki, huenda ulikuwa ni mkakati uliokuwa umepangwa na hao watu wa usalama.
 
Hatari hii....
 
Mkuu! Nakubaliana na wewe!
 

Very possible
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…