Nimeona Mabeyo akisema Magufuli {RIP} alivyoona hali yake ni mbaya na hawezi kupona tena, alimwambia Mabeyo amrudishe nyumbani.
Lakini Mabeyo akamwambia hawezi kuamuru hivyo, Magufuli akaonekana kumshangaa hata wewe CDF unashindwa kuamuru nirudishwe nyumbani?, Mabeyo akamwambia jukumu la kuamuru hivyo haliko chini yangu, hilo ni jukumu la madaktari.
Hata hili la Samia kuwa Tanga kwa shughuli za kiserikali, nalo linaweza kuwa tofauti na wengi tunavyodhani kwamba alifichwa.
Inawezekana ulikuwa mpango wao kutuficha sisi tusijue nini kinaendelea kumuhusu Magufuli, ndio maana hata PM nae akaja na hadithi Magufuli yuko mzima anachapa kazi, hii imekuwa tabia yao kutuficha hata ugonjwa wa viongozi wengine.
Unless Samia mwenyewe aje kuthibitisha vinginevyo, kwangu inawezekana kabisa licha ya Samia kuwa Tanga bado alikuwa anafahamu kila kitu kinachoendelea kuhusu afya ya Marehemu Magufuli, ni siri zao huko serikalini.