CDF mstaafu Mabeyo amelikoroga, Makamu wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais

CDF mstaafu Mabeyo amelikoroga, Makamu wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais

Chain of command
PRESIDENT >>V. P>>P. M huyo CDF ni mbali Sana anaripoti kwa waziri wa Ulinzi, Inakuwaje top secret ifahamike na CDF halafu VP na PM wasijue?

Pengine mwendazake alihisi kuna wasaliti hivyo akaamua kuvunja chain of command??
CDF anaripoti kwa Waziri wa ulinzi??

Jamani tupumzisheni kidogo.
 
Katiba mpya haijitekelezi yenyewe. Inahitaji watu ili itekelezwe. Hata hii ya sasa haijitekelezi. Inahitaji watu kutekelezwa.

Labda tatizo kuu si katiba. Pengine tatizo la msingi ni watu!

Kama walio na dhamana ya kuitekeleza hii ya sasa hawafanyi ipasavyo, hiyo mpya itawabadilisha hao watu na kuanza kuitekeleza?
 
Katiba mpya haijitekelezi yenyewe. Inahitaji watu ili itekelezwe. Hata hii ya sasa haijitekelezi. Inahitaji watu kutekelezwa.

Labda tatizo kuu si katiba. Pengine tatizo la msingi ni watu!
Constitution vs Constitutionalism.

Unaweza ukawa na Katiba lakini watu wakaipindisha na hakuna kitu venye mtawafanya.

Ukibisha unapigwa rungu la ugoko na vikosi vya usaRama.

Kiufupi bado watanganyika hawana upeo wa kuelewa nini maana ya katiba. Hawa ni mbuzi tu wakiongozwa na KIZIMKAZI mwenye DIVISHENI FOO.
 
There you go! 💯%.
 
Huyo mkewe mwenyewe alipata taarifa baada ya waziri mkuu na katibu mkuu kujua...mwanamke anabaki kuwa mwanamke kwenye mambo mazito..ndio maana unaona Samia ni rais wa mambo mepesi mepesi..safari za ulaya na arabuni, sherehe za kizimkazi, kucheza ikulu na wasanii pamoja na kina mwijaku na kina steve nyerere, kubadili mitandio na kujifukiza udi kwa chetezo cha umeme..kwenda kuangalia taarabu bwawani hotel.

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
Hahah kisa mwanamke sio na bado hamjasema mitano tena kwa mama
 
1. Aliyestahili kumpatia taarifa Makamo wa Rais juu ya kifo cha Rais Magufuli ni daktari wa Rais.
2. CDF Mabeyo alikuwa mkuu wa majeshi ndiyo, yeye pamoja na viongozi wengine wa vyombo vya usalama walitakiwa pia kupatiwa taarifa na Makamo wa Rais (Baada ya yeye kuwa mtu wa kwanza kabisa kufahamishwa) ili kuhakikisha tu usalama wa nchi upo vizuri.

3. Makamo wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais inaendeleaje.

4. CDF anachukua majukumu ya kuwa msaidizi mkuu wa Rais na mtoa taarifa kwa Makamo kuwa Rais amefariki (Kosa kubwa) mbaya zaidi Makamo wa Rais anakuwa mtu wa nne kuambiwa baada ya Waziri mkuu, CS na Taasisi ya kiswahili (Baada ya kujadili mpaka cheo cha Amiri jeshi mkuu)

Kosa ni la nani? Hayati Magufuli kujiundia kikundi chake cha siri kwa mambo yao huku wakimuondoa Makamo? Wasaidizi wake wakati Rais ni mgonjwa? Makamo wa Rais yupo Tanga anaongea kawaida tu huku Rais yupo kitandani akipigania uhai na wala hajulishwi hadi umauti tena masaa manne mbele baada ya mijadala ambayo kimsingi watu hawaijui katiba. Inafikirisha.

Sishangai kuona daktari binafsi wa hayati Rais Magufuli Prof. Mabula Mchembe kupotea ulingoni baada ya Samia kuwa Rais? Hivi yuko wapi huyu mtu?

Tusilaumu tu, twende kwenye uhalisia.

Kuna wakati, hata kwenye familia, nani apewe taarifa kwanza juu ya hali ya mgonjwa kuzorota au kifo, hutegemea zaidi wewe mwenyewe umejiweka karibu kiasi gani na huyo mgonjwa au marehemu.

Kama huwa unaenda kumwangalia mgonjwa kila mara, unapenda kujua hali ya mgonjwa kila mara, wewe ndiye utajulishwa mabadiliko ya hali ya mgonjwa kila mara. Je, Samia akiwa makamu wa Rais alijihusisha kwa ukaribu kiasi gani na hali ya mgonjwa, ndiye ingeamua ataarifiwe mapema kiasi gani. Nadhani taarifa ya kifo cha Magufuli walipewa kwanza watu wale walioonekana kujihusisha kwa ukaribu zaidi na hali ya mgonjwa. Makamu wa Rais alipewa tu taarifa kutokana na nafasi yake.

Ifahamike pia kuwa, katika uhalisia, makamu wa Rais kwa Tanzania ni cheo kisichokuwa na uzito wowote. Ni mtu wa kutumwa. Asipotumwa, anashughulika na masuala tu ya Mwungano na mazingira.
 
Si angemuita mkewe aliokawa hapohapo dar mbona hakumkumbuka?
Boss tunaongele mambo ya Nchi Mzee.....ishu ya mke inakujaje hapa, Yani uwe rais WA Nchi uone kabisa huna pa kutokea uite mkeo, unaniangusha Boss, ukishakuwa na madaraka makubwa kama ya Urais inakuwa Nchi kwanza, mambo ya familia badae.
 
Ni
Katiba kuhusu Rais na Makamu wake inafanana na katiba ya marekani kuwa Rais akifa Makamu anakuwa Rais. Sasa wewe unaonekana hujaangalia movie na series za kimarekani kuhusu vita iliyopo kwa Makamu kuutaka Urais!

RC Chalamila akiwa katika lindi la huzuni alisema kwa Katiba hii basi Rais aombe asipate Makamu Mchawi maana atamuondoa fasta akae yeye.

Kwa ilivyo Rais ni Taasis inayojiendesha kivyake na Makamu nae ni Taasis inayojiendesha kivyake kwa nchi yetu Rais ndio executive na Makamu wake anashughulika na Mazingira na Muungano basi. Mambo ya executive anapewa na Rais yale yaliyo katika level yake na ya vikao vya baraza la mawaziri so to say presidential general issues lakini exclusive zinabaki kwa Rais mwenyewe na vyombo vya dola vya nchi
Ni kweli kuna mambo ambayo kikatiba Rais hawezi kukasimu kwa mtu yeyote.
 
Magufuli aliweza kuagiza Mapadri waende, lakini alishindwa kuagiza aitiwe Makamu wake, hata amuachie wosia juu ya Majukumu anayomuachia, naona bado kuna vumbi halijatuama, nasubiri story zaidi.

Kwa hatua kama hiyo, kilichokuwa muhimu zaidi ilikuwa ni maisha yake ya baadaye, yaani maisha baada ya kifo. Ndiyo maana alitaka zaidi viongozi wa kiroho kuliko mwingine yeyote.

Tunafundishwa kuwa katika ufufuo hakuna hata familia wala ndugu wa damu, wote huwa ni sawa kama alivyo mwingine yeyote.
 
Wabongo bwana ujuaji mwingi Sana

Hivi unadhania mpaka mtu anakuwa CDF ni Jambo simple simple Sana eh

So wewe unajua utaratibu kuliko mkuu wa majeshi?

Tuache kujifanya wajuaji sana

Kwa hali aliyokuwa nayo marehemu wakati huo, ilikuwa ni wakati delicate sana. Hofu ilikiwa kwamba wabaya wake wangeweza kuitumia kummalizia. Ndiyo maana wakuu wa vyombo vya usalama wote walikuwa pale ili kuwa na uhakika kuwa hali yake mbaya ya kiafya haitumiwi na mahasimu wake. Hivyo hata kuwaweka mbali wale wote waliopo kwenye nafasi ya kuyarithi madaraka yake kama angefariki, huenda ulikuwa ni mkakati uliokuwa umepangwa na hao watu wa usalama.
 
1. Aliyestahili kumpatia taarifa Makamo wa Rais juu ya kifo cha Rais Magufuli ni daktari wa Rais.
2. CDF Mabeyo alikuwa mkuu wa majeshi ndiyo, yeye pamoja na viongozi wengine wa vyombo vya usalama walitakiwa pia kupatiwa taarifa na Makamo wa Rais (Baada ya yeye kuwa mtu wa kwanza kabisa kufahamishwa) ili kuhakikisha tu usalama wa nchi upo vizuri.

3. Makamo wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais inaendeleaje.

4. CDF anachukua majukumu ya kuwa msaidizi mkuu wa Rais na mtoa taarifa kwa Makamo kuwa Rais amefariki (Kosa kubwa) mbaya zaidi Makamo wa Rais anakuwa mtu wa nne kuambiwa baada ya Waziri mkuu, CS na Taasisi ya kiswahili (Baada ya kujadili mpaka cheo cha Amiri jeshi mkuu)

Kosa ni la nani? Hayati Magufuli kujiundia kikundi chake cha siri kwa mambo yao huku wakimuondoa Makamo? Wasaidizi wake wakati Rais ni mgonjwa? Makamo wa Rais yupo Tanga anaongea kawaida tu huku Rais yupo kitandani akipigania uhai na wala hajulishwi hadi umauti tena masaa manne mbele baada ya mijadala ambayo kimsingi watu hawaijui katiba. Inafikirisha.

Sishangai kuona daktari binafsi wa hayati Rais Magufuli Prof. Mabula Mchembe kupotea ulingoni baada ya Samia kuwa Rais? Hivi yuko wapi huyu mtu?
Hatari hii....
 
Nimeona Mabeyo akisema Magufuli {RIP} alivyoona hali yake ni mbaya na hawezi kupona tena, alimwambia Mabeyo amrudishe nyumbani.

Lakini Mabeyo akamwambia hawezi kuamuru hivyo, Magufuli akaonekana kumshangaa hata wewe CDF unashindwa kuamuru nirudishwe nyumbani?, Mabeyo akamwambia jukumu la kuamuru hivyo haliko chini yangu, hilo ni jukumu la madaktari.

Hata hili la Samia kuwa Tanga kwa shughuli za kiserikali, nalo linaweza kuwa tofauti na wengi tunavyodhani kwamba alifichwa.

Inawezekana ulikuwa mpango wao kutuficha sisi tusijue nini kinaendelea kumuhusu Magufuli, ndio maana hata PM nae akaja na hadithi Magufuli yuko mzima anachapa kazi, hii imekuwa tabia yao kutuficha hata ugonjwa wa viongozi wengine.

Unless Samia mwenyewe aje kuthibitisha vinginevyo, kwangu inawezekana kabisa licha ya Samia kuwa Tanga bado alikuwa anafahamu kila kitu kinachoendelea kuhusu afya ya Marehemu Magufuli, ni siri zao huko serikalini.
Mkuu! Nakubaliana na wewe!
 
Kwa hali aliyokuwa nayo marehemu wakati huo, ilikuwa ni wakati delicate sana. Hofu ilikiwa kwamba wabaya wake wangeweza kuitumia kummalizia. Ndiyo maana wakuu wa vyombo vya usalama wote walikuwa pale ili kuwa na uhakika kuwa hali yake mbaya ya kiafya haitumiwi na mahasimu wake. Hivyo hata kuwaweka mbali wale wote waliopo kwenye nafasi ya kuyarithi madaraka yake kama angefariki, huenda ulikuwa ni mkakati uliokuwa umepangwa na hao watu wa usalama.

Very possible
 
Back
Top Bottom