Kuna mshua mmoja namuheshimu sana aliongoza taasisi ambayo ina historia ya kutoa wabunge, yani si viongozi wakuu tuu, mpaka wale waliowafuatia wakurugenzi walikuwa wakistaafu wanagombea ubunge na kupata.
Sasa, yule mshua alivyostaafu, na yeye akaambiwa, kwa rekodi yako ya utumishi, na nondo unazotoaga kila siku, utafaa sana kugombea ubunge.
Yule mshua mtu fulani wa dini sana, unajua ile kibongobongo maadili maana yake ni dini. Akasema ataliweka hilo suala kwenye maombi na kupata baraka za Mungu kama hilo ni jambo linalofaa au lisilofaa. Kwangu mimi "Komredi" nachukulia hiyo kama ilikuwa namna yake ya kutafakari kwa kina na ku meditate kuhusu uamuzi huo mkubwa.
Baada ya muda fulani, yule mshua alikuja kujibu kwamba hataweza kugombea ubunge. Sababu alizotoa ni kwamba, ile process ya kugombea ubunge imejaa mambo ambayo yanapingana na principles zake za maisha.
1. Kugombea ubunge kulikuwa kama biashara fulani ya gharama kubwa, kulihitaji pesa nyingi sana. Pesa hizi, mtumishi wa umma ambaye alifanya kazi kwa uadilifu ni vigumu sana kuwa nazo, labda atumie kiinua mgongo chake chote. Na akifanya hivyo itakuwa kama anawekeza katika biashara, atalipwa vipi?
Kulikuwa na option ya kupata wafadhili, wafanyabiashara wakubwa, wampe hizo hela. Lakini, yeye maisha yake yote alikataa kuchukua pesa za wafanyabiashara wakubwa, kuna kipindi Muhindi mmoja alikuwa tayari kumsomesha mtoto wake Ulaya au Marekani, akakataa, akisema kuwa ukichukua fadhila hizi, kuna siku moja waliokupa fadhila nao watadai uwalipe kwa kuwafanyia mambo yao wanayoyataka. Hivyo, aliona matatizo mengi sana kwenye chaguzi zinazotawaliwa na fedha na rushwa.
2. Aliona kugombea ubunge kunahusisha siasa nyingi za majitaka, siasa za udini makanisani. Hakutaka kufanya siasa hizo.
3. Aliona kugombea ubunge kunahusisha sana siasa za kudanganya wananchi kwa ahadi zisizotekelezeka, zinahusisha kujipanga kwenye kauli na miongozo ya chama ambayo haitekelezeki na wala haina uhalisia.
Aliona sababu nyingi zinazo compromise principles zake za morality. Akaamua asigombee ubunge.
Na mtu kama huyo angegombea ubunge, pengine angepata nafasi ya kuwa Waziri na Rais.
Na mtu kama huyo, ndiye anayefaa kuwa waziri na rais.
Lakini, hizo sifa zake nzuri ambazo zinamfanya afae kuwa mbunge, waziri na rais, ndizo hizo hizo zilizomzuia kuwa hata mbunge.
Ndiyo maana nasema ngoma yetu ngumu, watu wenye sifa zinazofaa hawawezi kupanda ngazi ya uongozi, kwa sababu hawatakiwi huku juu na sifa zao haziwaruhusu kupanda ngazi ya uongozi wa kisiasa. Watu wasio na sifa, wale ruthless wanaotaka uongozi at any cost, kw auongo, kwa wizi, kwa rushwa, ndio wanaopata uongozi.
Sasa tunategemea rais aliyeanza kujifunza rushwa tangu akiwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi chuoni, aka graduate na kupata shahada ya pili ya rushwa akigombea ubunge, akapata Ph.D ya rushwa kwenye uwaziri, akaenda kuwa mkuu wa chuo cha rushwa kwenye urais, aongoze vita dhidi ya rushwa?