CDF Mstaafu Mabeyo ametaka kufikisha ujumbe. Je, wananchi tumeuelewa ujumbe?

CDF Mstaafu Mabeyo ametaka kufikisha ujumbe. Je, wananchi tumeuelewa ujumbe?

Ndiyo mjifunze sasa kwamba Makamu wa Rais si pambo tu.

Siyo mtu wa kukata utepe kufungua miradi ya serikali, kuhudhuria sherehe na kupigia kelele habari za muungano na mazingira tu.

Ukimuweka mtu kuwa mgombea mwenza na Makamu wa Rais, umempitisha kuwa Rais muda wowote Rais akifariki.

Yani nchi inaweza kuwa kwenye vita, Rais akafariki, halafu huyo Makamu wa Rais akawa Rais na Amiri Jeshi Mkuu aongoze vita.

Imagine Vita vya Kagera tunapigana na Nduli Idi Amin Dada halafu Rais wetu Samia !
Hapo mwisho kuna point kubwa sana
 
Basi ndio maana Jobo hakudumu kwenye awamu hii.
Hii ilikuwa wazi kabisa tangu anajiuzulu, zile sababu zilikuwa geresha tu.

Sababu halisi ni kwamba kulikuwa na timbwili kubwa tangu enzi za Magufuli. Yale mambo ya "Siongei na mbwa, naongea na mwenye mbwa".

Na ile move ya kuutaka urais kinyume na katiba ndiyo iliyomaliza kila kitu. Ni vigumu sana kuwa na Spika na Rais wana beef Tanzania. Hususan kama beef lenyewe linahusisha issue ya Spika kutaka kumputa Rais urais. Rais atakuwa muda wote anajiona anawekewa mitego tu na Spika.Mwishowe Spika akakubali matokeo tu.

Sasa mara paap, mbwa kageuka mwenye mbwa.

Lazima uwe mdogo tu.
 
Asee watu wa ajabu sana , wakang'ang'ana kila mtu anaitaka nafasi
Kwa sababu wanajua kwa mujibu wa Katiba ni mtu mmoja tu ndio huwa ana madaraka yooote !
Kwahiyo walipoambiwa huyo mtu amesha tangulia mbele ya haki wakajua kwamba sasa wanaweza wakaamua chochote wanachotaka kufanya !
Hiyo ndiyo mikanganyo iliyomo kwenye hii Katiba iliyopo !!
 
Tatizo Tanzania kila mtu ana matatizo yake, huyu dhaifu, huyu kichaa, huyu anapenda rushwa.

Yani ni kama vile ile ngazi ya kufika juu kwenye uongozi haiwezi kumuacha mtu salama.

Wanaofaa hawajulikani, wanaojulikana hawafai.

Choose your poison.
Na ile ngazi ni kama imeshikiliwa na wachache ambao wanataka apite ambaye anawafaa wao. Asiyetaka longo longo ambaye sisi wananchi tunamtaka hafiki kwa ile ngazi
 
Lakini pia Rais mstaafu Kikwete, wakati Ndugai alipoondolewa kwenye nafasi ya uspika, alieleza kuwa Rais alipofatiki, spika alimwendea na kumwambia kuwa kwa mujibu wa katiba, yeye spika ndiye anatakiwa kuwa Rais. Yeye Kikwete alimkatalia.
Hili sasa uunganishe na lile la TL kutopatiwa matibabu na ofisi ya huyu mheshimiwa ikiwa ni pamja na kukatwa mshahara wake
 
Lakini pia Rais mstaafu Kikwete, wakati Ndugai alipoondolewa kwenye nafasi ya uspika, alieleza kuwa Rais alipofatiki, spika alimwendea na kumwambia kuwa kwa mujibu wa katiba, yeye spika ndiye anatakiwa kuwa Rais. Yeye Kikwete alimkatalia.
Hii sikupata isikia mwenye link tafadhali
 
Na ile ngazi ni kama imeshikiliwa na wachache ambao wanataka apite ambaye anawafaa wao. Asiyetaka longo longo ambaye sisi wananchi tunamtaka hafiki kwa ile ngazi
Kuna mshua mmoja namuheshimu sana aliongoza taasisi ambayo ina historia ya kutoa wabunge, yani si viongozi wakuu tuu, mpaka wale waliowafuatia wakurugenzi walikuwa wakistaafu wanagombea ubunge na kupata.

Sasa, yule mshua alivyostaafu, na yeye akaambiwa, kwa rekodi yako ya utumishi, na nondo unazotoaga kila siku, utafaa sana kugombea ubunge.

Yule mshua mtu fulani wa dini sana, unajua ile kibongobongo maadili maana yake ni dini. Akasema ataliweka hilo suala kwenye maombi na kupata baraka za Mungu kama hilo ni jambo linalofaa au lisilofaa. Kwangu mimi "Komredi" nachukulia hiyo kama ilikuwa namna yake ya kutafakari kwa kina na ku meditate kuhusu uamuzi huo mkubwa.

Baada ya muda fulani, yule mshua alikuja kujibu kwamba hataweza kugombea ubunge. Sababu alizotoa ni kwamba, ile process ya kugombea ubunge imejaa mambo ambayo yanapingana na principles zake za maisha.

1. Kugombea ubunge kulikuwa kama biashara fulani ya gharama kubwa, kulihitaji pesa nyingi sana. Pesa hizi, mtumishi wa umma ambaye alifanya kazi kwa uadilifu ni vigumu sana kuwa nazo, labda atumie kiinua mgongo chake chote. Na akifanya hivyo itakuwa kama anawekeza katika biashara, atalipwa vipi?

Kulikuwa na option ya kupata wafadhili, wafanyabiashara wakubwa, wampe hizo hela. Lakini, yeye maisha yake yote alikataa kuchukua pesa za wafanyabiashara wakubwa, kuna kipindi Muhindi mmoja alikuwa tayari kumsomesha mtoto wake Ulaya au Marekani, akakataa, akisema kuwa ukichukua fadhila hizi, kuna siku moja waliokupa fadhila nao watadai uwalipe kwa kuwafanyia mambo yao wanayoyataka. Hivyo, aliona matatizo mengi sana kwenye chaguzi zinazotawaliwa na fedha na rushwa.

2. Aliona kugombea ubunge kunahusisha siasa nyingi za majitaka, siasa za udini makanisani. Hakutaka kufanya siasa hizo.

3. Aliona kugombea ubunge kunahusisha sana siasa za kudanganya wananchi kwa ahadi zisizotekelezeka, zinahusisha kujipanga kwenye kauli na miongozo ya chama ambayo haitekelezeki na wala haina uhalisia.

Aliona sababu nyingi zinazo compromise principles zake za morality. Akaamua asigombee ubunge.

Na mtu kama huyo angegombea ubunge, pengine angepata nafasi ya kuwa Waziri na Rais.

Na mtu kama huyo, ndiye anayefaa kuwa waziri na rais.

Lakini, hizo sifa zake nzuri ambazo zinamfanya afae kuwa mbunge, waziri na rais, ndizo hizo hizo zilizomzuia kuwa hata mbunge.

Ndiyo maana nasema ngoma yetu ngumu, watu wenye sifa zinazofaa hawawezi kupanda ngazi ya uongozi, kwa sababu hawatakiwi huku juu na sifa zao haziwaruhusu kupanda ngazi ya uongozi wa kisiasa. Watu wasio na sifa, wale ruthless wanaotaka uongozi at any cost, kw auongo, kwa wizi, kwa rushwa, ndio wanaopata uongozi.

Sasa tunategemea rais aliyeanza kujifunza rushwa tangu akiwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi chuoni, aka graduate na kupata shahada ya pili ya rushwa akigombea ubunge, akapata Ph.D ya rushwa kwenye uwaziri, akaenda kuwa mkuu wa chuo cha rushwa kwenye urais, aongoze vita dhidi ya rushwa?
 
Mwandishi wa daily news alitakiwa aulize siku na tarehe hayati aliyoomba aitiwe padri na kadnali pengo Ili wampe Toba
Naam,

Watu wangeweza kuhakiki vizuri nyendo za Paroko na Kardinali siku gani zilikuwaje.

Ile haikuwa interview, ile ilikuwa kama lecture.

In fact, it was a sermon, not even a lecture. Kwenye lecture huwezi kuuliza swali tu kwanza lazima unyooshe mkono.

Muandishi wa Daily News hata hakunyoosha mkono, alikuwa kama kakaa kanisani anasikiliza mahubiri, akinong'ona ni kama anasema "Preach" "Halleluyah".

Ukiangalia na kusikiliza unaona na kusikia kabisa muandishi kasahau kazi yake ya kuuliza maswali, kakaa pale anamuogopa, anamtukuza, anamuhusudu, anamshangaa Mabeyo.

Waandishi wa Daily News walishapewa maagizo kwamba wasimuulize swali wala kumuingilia Mabeyo, wamuache aseme alichotaka kusema tu.

Daily News ni chombo cha serikali, hapa kuna propaganda za serikali zinaendelezwa.

Ndiyo maana Mabeyo hajatoa hizi habari kwenye mkutano na waandishi wa habari au kwenye chombo binafsi cha habari ambako angeweza kubanwa vizuri kwa maswali.
 
Back
Top Bottom