CDF Mstaafu Mabeyo ametaka kufikisha ujumbe. Je, wananchi tumeuelewa ujumbe?

Mbona katiba iko wazi sana juu ya nani atakua rais kama rais wa madarakani atafariki?? Ni wewe ndio huelewi labda.
 
Hatari sana mkuu, hiyo ngazi ni ngumu kuipanda kama unapenda haki.

Makando kando ni mengi , mtu anatafuta wadhamini kwa makubaliano ukipata inabidi na mimi uje unipe kitu (katika jimbo either kupitisha biashara ya magendo/kukwepa kodi nk nk) .wengine hufikia kuua wapinzani wao hasa akimuona ni mwiba kihoja kwake
 
Mbona katiba iko wazi sana juu ya nani atakua rais kama rais wa madarakani atafariki?? Ni wewe ndio huelewi labda.
Shida sio kuelewa yeye , inaeleweka shida ilikuwa kwenye kuifuata ndio maana CDF akasema kulitokea mvutano inawezekana watu waliisahau katiba. Sio walisahau hapo kaongea Kiutu uzima
 
Hiyo ndiyo "paradox of political pugilism".

Ni kama vile ili upiganie principles unazozisimamia, inakulazimu uzivunje hizo principles unazozipigania.

N aukizivunja tu, watu wanachukua faili lako na kulihifadhi, ukifika juu siku moja na kuwasaliti wanawaga mchele wote kwenye kuku wengi.

Matokeo yake, hata wale wanaoanza kwa kusema watavunja principles ili wapande juu wazitetee principles, wakifika juu wanaishia kuwa mateka wa system.
 
Na ile ngazi ni kama imeshikiliwa na wachache ambao wanataka apite ambaye anawafaa wao. Asiyetaka longo longo ambaye sisi wananchi tunamtaka hafiki kwa ile ngazi
Iko vile bandugu !
 
So sad 😞
 
Mbona katiba iko wazi sana juu ya nani atakua rais kama rais wa madarakani atafariki?? Ni wewe ndio huelewi labda.
Iko wazi kimaandishi lakini in reality it’s different !
Ndio maana wale waliotaka kupindua meza wanajua hivyo na wakataka kufanya yao !
 
Shida sio kuelewa yeye , inaeleweka shida ilikuwa kwenye kuifuata ndio maana CDF akasema kulitokea mvutano inawezekana watu waliisahau katiba. Sio walisahau hapo kaongea Kiutu uzima
Barafu ya moto amekurupuka, hakumsoma mtoa mada Bams kwa ajili ya kuelewa (He read without understanding). Msamehe
 
Kelele zote zile za kusema nchi itapigwa mnada alikuwa anajua fika kifuatacho.

Kumtegemea binadam ni risk sana kwa haya maisha yetu ya leo yupo anaekupa jeuri lakini kesho hayupo, lazima ushuke tu taka usitake.
 
Asee watu wa ajabu sana , wakang'ang'ana kila mtu anaitaka nafasi
Tamaa mbaya sana, wengi wanapenda kuwa pale juu hiyo ni hulka ya binadam wengi kwenye madaraka. Shida inaanzia kutaka hadi kukiuka taratibu.
 
Kelele zote zile za kusema nchi itapigwa mnada alikuwa anajua fika kifuatacho.

Kumtegemea binadam ni risk sana kwa haya maisha yetu ya leo yupo anaekupa jeuri lakini kesho hayupo, lazima ushuke tu taka usitake.
Naam.

Halafu jitahidi sana usimdharau mtu kwa kuwa huyu mdogo, huyu hana cheo, huyu mbwa tu si mwenye mbwa, huyu mwanamke.

Maisha yanabadilika sana na juu panakuwa chini wakati chini panakuwa juu.

Sasa Ndugai ubabe wote ule kwa sababu ya kujua Magufuli yupo umekwisha.
 
Hakika mkuu, tatizo madaraka yanawalevya baadhi ya viongozi wetu na kuona washayamaliza maisha kumbe bado safari ni ndefu.

Huwa nasema usimdharau mtu yeyote yule, kushindwa na maanguko mengine ni ya kujitakia.
 
Aibu ikamtengua kabla ya kutenguliwa saivi kimyaa asee dharau na kiburi mafikio yake mabaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…