CDF Mstaafu Mabeyo ametaka kufikisha ujumbe. Je, wananchi tumeuelewa ujumbe?

Kuna siku I think baada ya raisi mama Samia kuapishwa, Mstaafu Mabeyo alisema kuna kitu aliambiwa na Magufuli atamfata ofsini amueleze.

Iko ndio nilitamani sana kusikia nini?je kililihusu taifa ama?na je mzee Magufuli wakati anaaga na mengineyo akumwambia chochote cha kitaifa Mstaafu Mabeyo?

Ila Ki ukweli Hekima ilitumika sana, Hongera kwa Mama Samia, Mstaafu Mabeyo na wote. Maana nchi za wenzetu ungekuta kushachafuka, jinsi wasivyo wavumilivu
 
😂😂🔥

Katiba iko wazi Kabisa bwashee Katika hili

Sema tu ni mara ya kwanza Rais wa JMT anafariki!
Tukisema katiba iko wapi ni vema kutaja na kifungu hicho cha katiba kinacho weka uwazi huo ili kuwasaidia walio wengi waweze kufahamu.
 
Samia haogopi. Ukitukana wewe tukana yeye anapiga kazi, ukimkosoa anakusikia, kama kuna tija anachukua mawazo yako.
Huu ni upevu wa kisiasa. Ukikosolewa tazama kama ushauri huo una tija kwa Taifa uchukue.

Kwa sasa anachoogopa Mh Rais ni Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi. Huenda sio yeye hasa bali counterpart wa.....
 
Usimlishe maneno hakusema kuna kitu aliambiwa na Magufuli acha uongo.
 
Chawa wa Mama Kazini
 
Andiko zuri sana Bams umeutendea haki ubongo wako.

Bahati mbaya mama pamoja na kunusurika kuwa mhanga wa ubovu wa katiba, leo hii kasahau kila kitu.

Watu tunataka mabadiliko ya katiba ambayo huheshimika sana katika kila nchi ulimwenguni kote, yeye badala ya kuwa mstari wa mbele katika hilo bado anaona mabadiliko hayana maana wala umuhimu wowote, huku akiikebehi katiba kwa kuiita 'kijitabu'!

Kama kiongozi manusura kashindwa kuona umuhimu wa kuboresha katiba, vipi kuhusu hao wengine wasio manusura!?

Tuna bahati mbaya sana, na tuna safari ndefu sana.
 
Rais alivyouona utamu wa kiti kile amefika mbali zaidi kwa kusema kuwa SISI wananchi hatuna ufahamu na uelewa wa Katiba hivyo kwanza tuelimishwe kuhusu Katiba ndipo tupewe katiba mpya...

Kwa matamshi hayo anamaanisha kuwa Katiba ni mali yake binafsi na taasisi yake na siyo ya Watanzania. Hili ni kosa kubwa dhidi ya Katiba na kutukosea sisi wenye nchi
 

Madaraka yamempofusha kiasi cha kukosa kupata kwa yale ambayo yalitaka kimtokea.
 

Kauli ile ya Samia kuwa eti katiba ni kijitabu tu, kwa nchi za waelewa ilitosha kabisa kwa yeye kuondolewa mara moja kwenye kiti cha Urais.

Katiba uliyoapa kuilinda unaidharau na kuiita kuwa ni kijitabu!! Kama huheshimu katiba, unaongoza nchi kwa kufuata nini?

Rais hajui kuwa bila katiba anayoidharau, yeye si chochote, ni mama tu kama walivyo wamama wengine wananchi wa kawaida ambao hata wakifika mahali wanaweza wasiachiwe hata kiti. Kwani bila katiba, Samia ana nini cha pekee kuwazidi akinamama wengine?
 
Chawa wa Mama Kazini
Njoo na points za kunipinga, siyo kusema tu kiurahisi eti "chawa wa mama"!!

Yaani niache kusifia maendeleo na mafanikio ambayo nayaona nchini kisa eti baro ataniita chawa wa mama!!

Nyinyi mliokuwa chawa wa Magufuli mlikuwa mnamshangilia wakati anaharibu na kubomoa nchi. Amekufa na mama anarekebisha kwa speed ya 5G mnaumia
 
Unaweza kutudhibitishia juu ya yale waliyo yafanya hao ulio wataja?!, au ni ule mwendelezo wa zile propaganda zenu zinazoongozwa na chuki!?.
 
Magufuli aliharibu nchi wapi??
Embu toa ufafanuzi.
Miradi mingi mama anayotamba nayo ni ile kipindi cha Magufuli iliyoanzishwa.
 
Raisi anawezaje kutengua UBUNGE wa NDUGAI
Vitu vingine acheni SIFA kumpa ni SHERIA haimruhusu na haimpi haki ya kutengua UBUNGE wa ndugai lbda ubunge wa BASHIRU
 
Ebu tutajie mafanikio ya Mama kwa Trillion 30 alizokopa ?
 
Hatuna Bunge thabiti, Hatuna Mahakama inayojitambua tumebakia na Watawala headless.

Tutapaparika tu sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…