Mkuu wa jeshi ya Ulinzi ya Uganda (CDF), Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ametangaza kuondolewa kwa vikwazo vya matumizi ya mitandao ya kijamii kufuatia kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi nchini humo.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) leo Januari 26, 2026, Muhoozi amewashukuru wananchi wa Uganda kwa ushirikiano na msaada waliouonesha katika kipindi chote cha uchaguzi, akiwapongeza kwa ushirikiano wao.
“Tunafungua mitandao yote ya kijamii leo. Nawashukuru watu wote mahiri wa Uganda kwa msaada na ushirikiano wenu katika msimu huu wa uchaguzi. Ninyi ni watu mahiri zaidi duniani na mnatupa ujasiri wa kulitumikia taifa, Mungu awabariki nyote” aliandika Muhoozi.
Tamko hilo linakuja wakati ambapo Uganda imekamilisha mchakato wa uchaguzi uliopita, uliokuwa na mvutano mkubwa wa kisiasa na hatua kadhaa za kiusalama ikiwemo kudhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii. Serikali ilidai hatua hizo zililenga kulinda usalama wa taifa na kudhibiti taharuki.