Moshi25
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,555
- 4,118
Cedric Kaze nakukubali sana Mwalimu unajua sana kukaba mashabiki lia lia tunajua kuwa Yanga haifungiki sasa msimu huu mbona naona kama Yanga haiko imara sana pasi si nyingi kama mwaka jana, uwezo wa timu kumiliki mpira na kupasua katikati kwenda mbele kushambulia umepungua, mabeki wanarudisha sana mipira nyuma viungo wanachelewa kuchukua mpira na huo sio mpira wa Yanga, inatakiwa timu irudishe mpira wake wa kulazimisha kwenda mbele kushambulia kwa nguvu na kasi bila kuchoka kwa dakika 120 au mazoezi ya kukimbia na kukaba umeyapunguza ?
Timu yetu kwasasa haikabi kitimu, kitaalamu na kwa nguvu kama msimu ulioisha na tunafungwa magoli mepesi hasa kona na faulo mabeki wanajichanganya sana, umakini wa kujilinda umeshuka kama goli la Sakho lilituudhi sana hadi tukapasua TV na kuacha kuangalia mechi maana ni goli jepesi sana mabeki wote waliangalia mpira unakotoka na kuwasahau kabisa washambuliaji wa Simba na pia Diarra kapunguza umakini wa kucheza krosi hayo yasijirudie rekebisha hiyo bado mapema wachezaji wakipoteza mpira timu nzima ishirikiane wote kukaba tena kwa nguvu hadi wachukue mpira wao hicho ndo kilitupa makombe yote msimu uliopita!!
Ligi ya msimu huu ni ngumu sana kuliko msimu ulioisha wachezaji wa Yanga wajitume mara bilioni mbili bila hivyo kombe tutalirudisha Kolokoloni msimbazi
To go to the top ni kazi ngumu sana ambayo Yanga imeweza ila kubaki on top ni kazi ngumu zaidi
Daima mbele nyuma mwiko