Cement za Rhino na Lucky

Cement za Rhino na Lucky

Kibela

Member
Joined
Mar 21, 2012
Posts
58
Reaction score
10
Habari wadau,

Kuna cement za aina ya rhino na lucky naziona sokoni zikiuzwa kwa 14,000/= na 14,500/= respectively.Je ni nzuri kwa kutumia kutengeneza matofali? Nipeni info kuhusu quality za cement hizo.
 
Ni nzuri sana hasa hiyo rhino na lucky inatengenezwa pakistan pia arabuni hapa dubai ghorofa nyingi sana ikiwemo burj kharifa (ghorofa refu kuliko yote duniani)limetengenezwa na hiyo lucky..ni nzuri sana ata mimi nimeshaitumia....hapa dubai inauzwa tsh 3500 kwa mfuko mmoja..nunua ni nzuri
 
Thanks for the useful info.
 
Rhino wamejenga kiwanda Mkuranga, na walianza uzalishaji wa saruji tangu mwaka jana. Rhino wamesababisha bei ya saruji kushuka bei sokoni sasa unaweza kupata saruji kwa shilingi 13,000.00
 
Ni nzuri sana hasa hiyo rhino na lucky inatengenezwa pakistan pia arabuni hapa dubai ghorofa nyingi sana ikiwemo burj kharifa (ghorofa refu kuliko yote duniani)limetengenezwa na hiyo lucky..ni nzuri sana ata mimi nimeshaitumia....hapa dubai inauzwa tsh 3500 kwa mfuko mmoja..nunua ni nzuri
Rhino cement haitengenezwi Pakistan wala Uarabuni ni bidhaa ya Athi river Mining wana kiwanda sasa huko Mkuranga
 
Rhino ni ya hapa hapa bongo, ni nzuri sana
 
Qatar wanakiwanda kiitwacho al jabal lar cement factory..ambacho kwa miaka mingi wamekuwa wakitengeneza cement ya jina la rhino..navyosikia sasa wana collaboration katika nchi nne za afrika Tz..Kenya..Rwanda..S africa..hizi nchi zote zina zalisha cement hiyo RHINO ..nadhani watakuwa na ubora unaofanana..thanks
 
mimi nina uzoefu na cement ya lucky. Nilianza kutumia lucky baada ya kushauriwa na fundi mmoja mjenzi wa magorofa kuwa cement za bongo uwa wanapunguza uzito kwa taribani nusu kilo au kilo moja kwa mfuko kwa hiyo ukinunua mifuko mingi unapigwa zaidi. Pia cement yao imefungwa vizuri inaweza kukaa muda mrefu bila kuharibika. Mimi nimejenga kwa kutumia lucky tu na ni nzuri sana
 
Habari wadau,

Kuna cement za aina ya rhino na lucky naziona sokoni zikiuzwa kwa 14,000/= na 14,500/= respectively.Je ni nzuri kwa kutumia kutengeneza matofali? Nipeni info kuhusu quality za cement hizo.

umeuliza swali zuri sana...mimi ni civil engineer na ninajua ubora wa cement mbalimbali...........ukweli ni kwamba watu wengi sana wanauziwa cement zenye ubora mdogo pasipo wao kujua..................kuna cement za barabarani ambazo huwa zinamwaga ili kufanya soil stabilization ambazo mara nyingi ubora wake ni mdogo ambao ni 30.2N hadi 32.5N kwa kiwango cha kiutalaam na watu wamekuwa wakiuziwa hizi cement na kujengea nyumba pasipo wao wenyewe kujua.Cement ambazo unatakiwa ujengee nyumba inatakiwa iwe 40N au 42N.Mimi katika mtaa ninapoishi watu wengi wanachakachuliwa cement pasipo wao kujua.Unakuta mtu anauza cement ambazo amezichanga na zile za barabarani ili apate faida kubwa.ukweli ni kwamba cement za barabarani bei yake ni ndogo kwa hiyo akizichanganya anapata faida kubwa.

NB:JITAHIDI UKIENDA NUNUA CEMENT SOMA MFUKO HADI UONE 40N AU 42N UBORA WA CEMENT.MAFUNDI WENGI HAWAJUI KIINGEREZA NDIO MAANA HAWAWEZI KUJUA LAKINI WANAWEZA ANGALIA HIYO NUMBER 40N AU 42N.
 
Habari wadau, Kuna cement za aina ya rhino na lucky naziona sokoni zikiuzwa kwa 14,000/= na 14,500/= respectively.Je ni nzuri kwa kutumia kutengeneza matofali? Nipeni info kuhusu quality za cement hizo.
Kilimanjaro Cement ni nzuri zaidi, inatoka kiwanda cha cement kigamboni(geza ulole)
 
(1) Zingatia Post Na 10 ya Swash Bizo.
(2) kwa kawaida usipende kununua cementi zinazotoka nje ya nchi, bali zilizotengenezwa Tanzania. Hii si kwa sababu ya kusaidia uchumi wetu tu, bali hasa kwa sababu sementi za nje hutumia muda mrefu safarini hadi zifike hapa na kuuzwa. Sementi ina shelf life isiyo kubwa na hutakiwa kutumika si muda mrefu baada ya kutengenezwa. Bora zaidi itumike si zaidi ya miezi 2 - 4 kufuatana na namna inavyohifadhiwa.
 
Maelezo yako ni mazuri sana lakini unaposema cement ya nje utumia mda mrefu mpaka kufika hapa!!!ni wiki 2 tu inakuwa sokoni tokea huko ilipoagizwa..si zaidi ya hapo pili ni lazima ipitie tbs hivyo hakuna hofu yoyote
 
Qatar wanakiwanda kiitwacho al jabal lar cement factory..ambacho kwa miaka mingi wamekuwa wakitengeneza cement ya jina la rhino..navyosikia sasa wana collaboration katika nchi nne za afrika Tz..Kenya..Rwanda..S africa..hizi nchi zote zina zalisha cement hiyo RHINO ..nadhani watakuwa na ubora unaofanana..thanks
Rhino ya Athi River Mining na Qatar hawana uhusiano!
 
umeuliza swali zuri sana...mimi ni civil engineer na ninajua ubora wa cement mbalimbali...........ukweli ni kwamba watu wengi sana wanauziwa cement zenye ubora mdogo pasipo wao kujua..................kuna cement za barabarani ambazo huwa zinamwaga ili kufanya soil stabilization ambazo mara nyingi ubora wake ni mdogo ambao ni 30.2N hadi 32.5N kwa kiwango cha kiutalaam na watu wamekuwa wakiuziwa hizi cement na kujengea nyumba pasipo wao wenyewe kujua.Cement ambazo unatakiwa ujengee nyumba inatakiwa iwe 40N au 42N.Mimi katika mtaa ninapoishi watu wengi wanachakachuliwa cement pasipo wao kujua.Unakuta mtu anauza cement ambazo amezichanga na zile za barabarani ili apate faida kubwa.ukweli ni kwamba cement za barabarani bei yake ni ndogo kwa hiyo akizichanganya anapata faida kubwa.

NB:JITAHIDI UKIENDA NUNUA CEMENT SOMA MFUKO HADI UONE 40N AU 42N UBORA WA CEMENT.MAFUNDI WENGI HAWAJUI KIINGEREZA NDIO MAANA HAWAWEZI KUJUA LAKINI WANAWEZA ANGALIA HIYO NUMBER 40N AU 42N.

Safi sana kwa kutufumbua macho.
 
Mkuu Swash Bizo ni sahihi ulivyoshauri, majority ya cements zilizopo sokoni ni grade 32.5N ambazo ni recommended kwa stabilisation and masonry works (matofali,mortar ya kuunganishia mawe au matofali) kwa structural works inashauriwa at least grade 40, binafsi nimechunguza hizo Lucky na Rhino naona zimeandikwa grade 43 kwa hiyo kama kweli TBS (assuming weledi ulizingatiwa)wamezikagua na zimefaulu kwa kiwango cha cement grade 43 mimi pia namshauri mkuu Kibela atumie hizo.
 
Last edited by a moderator:
Kama unataka kutumia kiasi kikubwa na una kampuni ya ujenzi wa nyumba za maghorofa manne kwenda juu, basi ni heri uchue hiyo Cement, changanya na kokoto (Concrete) kwa Ratio watakayosema watengenezaji cement na chukua mawe safi, maji safi na mchanga safi na tengeneza Zege lako na utengeneze Cubes na kisha upeleke UDSM kuzi-Crush.

Matokeo utakayopata yasipishane sana na kiasi walichosema wao. Kumbuka kwamba kwenye SITE, utatumia quality mbaya na hutakuwa na muda wa kutosha kufanya kama ilivyo kwenye SAMPLE.

Ila kwa jengo la ghorofa kuanzia nne kushuka chini, msiwe na wasiwasi, hata hiyo ya 35 sijui mnaweza kuitumia ila cha muhimu mhakikishe mnapima vizuri kokoto mnazoweka na msizidishe maji wala kuweka maji kidogo na kuhakikisha mnashindilia vizuri. Jengo litakuwa poa tu.
Kuna maghorofa nilishaona yamejengwa kwa matofali ya kuchoma na yapo imara tu. Ila kuta zake zinazobeba uzito ni nene sana maana kwa jengo la ghorofa nne, ukuta una kama upana wa mita moja hivi.

Tafadhali kila panapowezekana, tumia Matofali ya kuchoma na epukaneni na Cement maana huwa zinatoa Radiations ambazo si nzuri kwa afya zenu. Na kama walivyosema wengi, CEMENT NUNUA iliyoandikwa MADE IN TANZANIA.

Tuisaidie Nchi yetu kwa kununua vitu MADE IN TANZANIA.
 
Back
Top Bottom