Kuna vitu mnachekesha sana, yani uwashauri kufikia hotel za Kariakoo wakati Ramada ni beach front hotel?
Simba ilitakiwa kuwafanyia traffic arrangements tu na hizo huduma zipo zinalipiwa hukai foleni popote.
Hotel watakayofikia Simba Johannesburg umbali wake kwenda uwanja wa FNB Soweto umbali wake haupungui umbali wa kutoka Dar kwenda Mlandizi, sasa kutoka mbezi beach kwenda uwanja wa Mkapa kuna umbali gani? Hazizidi kilometers 35.
Je nyinyi mtakubali mkiambiwa mfikie Soweto au Mayfair au Laanglagte ili muwe karibu na uwanja wa FNB? Na mkiambiwa mfikie Downtown Hillbrow au Holiday in President street mtakubali?
Kwa vyovyote vile Simba ni lazima itafikia uzunguzi Sandton city au Rose bank na ni mbali kwenda uwanjani lakini miundombinu inaruhusu kuna barabara kibao za kutumia siyo kama Dar mnategemea barabara moja tu kutoka Mbezi beach kwenye Mkapa stadium.