Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 13,075
- 11,682
Nimemsikia Slaa akiuliza kwa nini wanachama na wafuasi wa Chadema hawatokezi Mahakamani. Amekumbushia kuwa suala hilo ni tofauti na mikutano ya hadhara kwa vile linahitaji uhamasishaji wa dhati kutoka matawi hadi taifa. Kauliza viongozi wangapi wanajitokeza Mahakamani. Akagusia pia kuwa tofauti zilizomo ndani ya chama zinaweza kuwa zinachangia.Inajulikana kikundi hicho kiko chini ya uongozi wa Awadh; yule polisi aliyewavuruga viongozi wa CHADEMA kule Mbeya mwaka jana. Hicho ni kikundi maalum, kisichokuwa rasmi ndani ya jeshi la polisi. Hawa hawawajibiki kwa viongozi wa polisi moja kwa moja, ndiyo maana Muliro hana lolote la kusema juu yake.
Silaha pekee wanayoweza kujihami nayo CHADEMA katika hali ya namna hii ni kukusanya ushahidi wa matendo haya maovu, kwa kuyarekodi kila inapowezekana na kuwatambua watu wanao husika katika uovu huu.
Mimi nakubaliana nae. Kuwatenga wapambanaji kama Catherine Ruge ni kujipunguzia nguvu maana Ruge na Bawacha wenzake ni wapambanaji wazuri sana. Mtu kama Kigaila ni mhamasishaji mzuri kuliko Naibu KM wao wa sasa hivi. CDM inatakiwa kuachana na mambo ya kijinga ya kuitana Njaa 55, waungane maana wamepewa cause ambayo wote wanaweza kuungana na kuzika tofauti zao.
Mwisho, Mbowe alipoitisha maandamano hakulala kwake ili kukwepa kudhibitiwa. Akaibuka kwenye venue ya maandamano akiwa na binti yake. Nawashangaa hawa wa sasa wanaondoka na convoy kwenda Mahakamani. Na wanalala nyumbani kwao. Wanategemea nini?
Amandla...