CHADEMA acheni kulialia, acheni matamko, fanyeni kwa vitendo

Huyo ni G55, lazima atatee upande alioko.
 
Subiri hapo G55 mtakapochukua uongozi wa chama mkirudishe huko CCM. Bila shaka wakati huu mnasubiri kwa hamu kubwa CCM kuwarudishia hicho chama mkiongoze. Hiyo haitakuwa CHADEMA tena.
 
Huyo ni G55, lazima atatee upande alioko.
Tokea mwanzo kabisa, wakati ule kuelekea kwenye uchaguzi alipokuwa halali kila mara akibandika maandishi marefu sana humu kutetea msimamo wa Mbowe, nilijuwa huyo ni mfaidika wa mipango ya CCM kuinunua CHADEMA.
 
Kama mnategemea kuwa kuna siku polisi watakuwa hawana silaha ndio "mpambane" nao basi mtasubiri sana.
Sasa tazama mawazo ya mtu kama huyu yalivyo! Unahimiza waTanzania wakauliwe ndiyo iwe furaha yako? Tena unahimiza wafanye hivyo, hata bila ya maandalizi ya kina kujuwa kitaendelea kitu gani baada ya kuwatoa mhanga watu? Hii ni akili ya wapi!

Sasa mbona unapinga "kuzuia uchaguzi bila kuwepo na marekebisho kwenye taratibu za uchaguzi", huoni kuwa huko ndiko kwenye mapambano zaidi ya hayo unayolilia ya kuwatoa tambiko kwa CCM wanachama na wapenzi wa CCM ili nyinyi mpate nafasi za kuingilia mlango wa nyuma?

Nyinyi sasa mmejipambanua waziwazi kabisa kuwa ni maadui wakubwa wa mabadiliko. Nyinyi ni zaidi hata ya CCM; kwa sababu inaonekana mnayo njaa kubwa zaidi kiasi kwamba hata subira hamna. Hamtumii tena akili kufikiri matokeo ya mnayohimiza yafanyike, huku nyinyi mkiwa pembeni mkishangilia.

Nimeanza kukudharau.
 
Subiri hapo G55 mtakapochukua uongozi wa chama mkirudishe huko CCM. Bila shaka wakati huu mnasubiri kwa hamu kubwa CCM kuwarudishia hicho chama mkiongoze. Hiyo haitakuwa CHADEMA tena.
Hapo ndipo mnapokosea. Hao G55 ndio waliokifikisha chama chao hapo kilipo mpaka mkakitamani. Mimi naanza kuamini kuwa mmetumwa kukimaliza kabisa.
Amandla...
 
Hapo ndipo mnapokosea. Hao G55 ndio waliokifikisha chama chao hapo kilipo mpaka mkakitamani. Mimi naanza kuamini kuwa mmetumwa kukimaliza kabisa.
Amandla...
Mbona upo sahihi kabisa. Hao G55 ndio hakika waliokiuza chama kwa Samia. Hawa hawakuwa na mchango wowote wa maana wakati CHADEMA ikivuma, kama enzi zile za Dr Slaa akiwa Katibu Mkuu.

CHADEMA ambayo ilikuwa chini ya Mbowe aliyesambaratishwa na Samia ingepata mwanya wa kuwa serikalini, hawa G55 wangekuwa ni wabovu zaidi hata kuliko CCM ilivyo sasa hivi.
 
Mkuu watu kama ninyi ndio vikwazo vikubwa katika haya mapambano

Yaani wewe unaona kuna upande mmoja unauonea upande mwingine badala ya kukaani na kuunga mkono juhudi za kitafuta haki unaanza kuwalaumu watafuta haki utadhani huu ni mchezo halali kama unavyo ilaumu Azam kwanini haifanyi vizuri

Mkuu kama juhudi zote zilizo fanyika na CDM na bado huoni kama wanapambana kwa kadiri ya uwezo wao basi utakua na matatizo makubwa sana

Imetangazwa tu NRNE Mwenyekiti kapewa uhaini, kwenda mahakamani tu watu wanavunjwa miguu
Before that watu wamefungwa wametweka na kuuwawa na madhila yote mabaya unayoyajua lakini unaona bado tu...... unataka wafe na kufungwa CDM wote ndio utaridhika imepembana vyema?

Hakuna tawala dhalimu itadumu milele mkuu hata CCM itaanguka tu kwa namna yoyote ile, ni swala la muda tu
Juhudi hizi hizi unazo ziona za kiwaki na zina wa cost watu uhai wao, uhuru wao na mateso ipo siku zitakuja kulipa...... kikubwa ni ku keep fighting
 
Sasa tazama mawazo ya mtu kama huyu yalivyo! Unahimiza waTanzania wakauliwe ndiyo iwe furaha yako? Tena unahimiza wafanye hivyo, hata bila ya maandalizi ya kina kujuwa kitaendelea kitu gani baada ya kuwatoa mhanga watu? Hii ni akili ya wapi!
Ndio zenu hizo. Ku twist mambo anayosema mtu. Wapi nimehimiza watu wakauliwe. Nilichokuambia ni kuwa Tanpol siku zote watakuwa na silaha kwa hiyo kungojea mpaka watakapokuwa hawana silaha ni kujidanganya. Hayo maandalizi unayotaka kufanya ni yapi?
Napinga kwa sababu uwezo wa kuzuia uchaguzi hamna. Na mpaka sasa hivi hamjaweka wazi namna mtakavyohakikisha hamna uchaguzi. Njia zilizopo ni mbili tu:
1. Kuomba Mahakama iuzuie
2. Kuingia barabarani na kuhakikisha kuwa haufanyiki.
Ya kwanza ni ndoto na ya pili haitafanikiwa kama mnaogopa kuumizwa. Mnaotaka kuwatoa kafara ni nyie ambao mnatumia maneno magumu bila kuwa na njia ya kuwalinda wasiumie.
Msio na subira ni nyie. Hivi kweli mlitegemea CCM itakubali mabadiliko ya katiba miezi 7 kabla ya uchaguzi. Wenye njaa ni nyie ambao mko tayari kuwalaghai raia wa nchi hii ili tu mlambe pesa za tone tone ( ambazo pamoja na ahadi yenu ya transparency mnawaficha wanachama wenu kuhusu mapato na matumizi yake). Bado unaniwekea maneno mdomoni. Wapi nilipo himiza fujo?
Nimeanza kukudharau.
Mbona umechelewa? Maana wanaonidharau ni wengi sana.

Amandla...
 
Unajichanganya na haujui ulisemalo. Chadema ilivuma sana baada ya Slaa kuondoka. Ilikuwa inakisumbua chama tawala ndani na nje ya Bunge. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Amandla...
 
Mbona umechelewa? Maana wanaonidharau ni wengi sana.
Na wanafanya hivyo kwa haki kabisa. Kwa bahati mbaya nilichelewa kutambua hilo. Nilidhani kuwa pengine una hata chembe ndogo tu ya 'objectivity' ndani ya akili yako, kumbe hakuna kitu!

Na sasa kumbe unajitambulisha kuwa "Fundi Utumbo"! Hongera kwa ukweli huu.
 
Na wanaofanya hivyo hata hawajanibadilisha hata kidogo. Wengi wao huishia kunitukana kama unavyojaribu kufanya. Hata hivyo sidhani kama unajua maana ya objectivity. Unadhani objectivity ni kukubaliana na wewe hata kama ni wazi haujui usemacho.

Amandla...
 
I'm done with you.
There is no value in engaging you any further.
 
Hivi siku ya kupiga kura, polisi watakuja kuwatoa watu majumbani wakapige kura? mana wamefanikiwa kutumia nguvu kushurutisha raia kufuata matakwa ya watawala
Mimi na familia yangu tutaenda kupiga kura kwa iyari na tunaomba polisi na jwtz watuwekee usalama wa kutosha.
 
Mimi na familia yangu tutaenda kupiga kura kwa iyari na tunaomba polisi na jwtz watuwekee usalama wa kutosha.
kampigie baba arudi bungeni, koo za wanufaika na mfumo waende, bebeni na wajukuu mliowaandikisha nchi huru hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…