CHADEMA amsheni watu kwa kauli za kina Chalamila kwa mjamzito kwamba kama hatoi Shs 50,000 arudi nyumbani mume wake amkate kwa kisu na mkasi ajifungue

📌📌📌Hii dunia sio mahali salama kwa MASIKINI!!!

YAANI HUNA HATA ELFU HAMSINI YA AKIBA ILA UNAPATA WAPI UJASIRI WA KULETA KIUMBA HAPA DUNIANI🧐🧐🧐

WAAFRIKA BADILIKENI UJAUZITO SIO AJALI.CONDOM ISIYOPASULA INAUZWA BUKU.HAKUNA UFAHARI KWENYE UFUKARA!!!

NI DHAMBI KUBWA SANA KUZAA WATOTO USIOWEZA KUJA KUWAHUDUMIA NA KUWAACHIA URITHI. HAO WATOTO WANAISHIA KUWA CHEAP LABOUR HUKO VIWANDANI KWA WAHINDI WANALIPWE BUKU 4 KWA SIKU.


📌KAMA HUNA HELA NI BUSARA UKAPANGA UZAZI!!!
 
Wanataka kuleta watoto wateseke bila sababu
Hamna dada yako, binamu yako au ndugu yako yeyote aliewahi kudungwa mimba bila kupanga? Kumbuka ni wanyama tu wanao mate kwa lengo la kuzaa, sio wanadamu. Huenda hata mimba yako haikupangwa pia.
 
Watu inatakiwa wawajibike kwa watoto wanaowazaa, serikali ijenge barabara, reli, madaraja, ulinzi n.k bado hatujafikia hatua ya serikali kulipia uzazi wa watu.
 
Chadema ndio ina wajawazito? Kule Kenya raia wangeisha lianzisha bila kungoja Chama. Wacha ujinga kuzania kila kitu lazima kianzishwe na chama
 
Point safi sana Mkuu. Hata mie nilivyoelewa ni kwamba uchangiaji kwenye huduma za wajawazito ulikoma, kwa tozo na misaada toka nje kupunguza vifo vya kina mama na watoto. Ndio maana majibu ya huyu mvuta bangi yanatia karaha sana!



Huyo hapo ☝️week iliyopita tu alikuwa anamfanyia mazingaombwe mkurugenzi wa WHO wana huduma nzuri ya uzazi na wamepunguza vifo.

Ndio vitu wanavyochapisha kwenye website yao wapo vizuri. Wakati uhalisia kuna wamama wajawazito na vichanga wanafia mbele ya wauguzi kisa tu kukosa gloves.

Siku chache baadae, mkuu wa mkoa na yeye baada ya bange zake anatoa kejeli kwa raia kama kawaida yao.

Huko serikalini sijui kama kuna hata mmoja ataiona pepo unafiki wa hawa watu sio wa dunia hii.

Mungu anipe nguvu nilisema sitoongelea tena afya huyu mama alipopewa uwaziri maana chaos itakayofuata ni balaa.
 
Watu wenye vichwa mithili ya maboga Huwa wanakera sana.yaani chalamila anapingana na sera ya wizara ya afya ya mama mjamzito kujifungua bure anatuletea ujinga wake.
 
Kama tungekuwa tumezaliwa mazingira hayo tungekuwa tunatia huruma kama wewe na kusubiri kudra za serikali.

Wewe huna elfu 5 ya groves huyo mtoto utamlisha Nini?
 
Mwenye email ya huyu Mkuu wa WHO amtumie hiyo clip ya Chalamila amwambie alivyodanganywa na viongozi wahuni wa Tanzania, hela zote za msaada kwa wajawazito zimenunua mabasi ya CCM!😀
 
Wewe huna elfu 5 ya groves huyo mtoto utamlisha Nini?
KIla mtoto anakuja na baraka yake! Kwanza umesahau tuliambiwa tuzae tu, tufyatue? Si hao hao kina Chalamila walisema tufanye hivyo?
 
Wanataka kuleta watoto wateseke bila sababu
Ni ujinga mkubwa mtu unajijua hohehae na bado unashindwa kutumia CONDOM ukazuia kupata zambi ya kuja kutesa kizazi chako.


Mtu huna mbela wala nyuma ila unang'ang'ana na wewe upate watoto.

📌waafrika waache ujinga kuzaa hovyo sio sifa.Kama mtu hana PESA kabisa ASIZAE!!
 
Ni lugha imetumika vibaya tu, watu wasifurahie tu ngono, wawajibike na kinachofuata baada ya hapo.
 
Namna nzuri ya kufundisha kwa vitendo ni kuwaacha wapambane na hali zao.
 
Ni lugha imetumika vibaya tu, watu wasifurahie tu ngono, wawajibike na kinachofuata baada ya hapo.
Wanadamu sio wanyama kwamba ngono ni tendo la kuzaa tu. Kuna mimba za kutotarajia. Wewe na mimi huenda mimba zetu hazikutarajiwa. Kwani wewe ulishawahi muuliza mama yako kama mimba yako aliipanga akakuhakikishia kuwa ndivyo ilivyokuwa?
 
KIla mtoto anakuja na baraka yake!
Huu msemo ndo maskini wote walimezeshwa😂😂😂


📌Hakuna baraka ya kizembe hivyo.Bali unawaandalia wahindi CHEAP LABOUR wa kwenda kutumikia huko viwandani kwa ujira wa 4,000/= kwa siku.Hivi hamvionei huruma vizazi na damu zenu!!!

Wengine kutokana malezi mabovu yanayoambatana na UMASIKINI wanaishia kuwa wapiga debe,mawinga,madalali,wezi ,majambazi na machangudoa.
 
Namna nzuri ya kufundisha kwa vitendo ni kuwaacha wapambane na hali zao.
Hapana. Huo ni mtazamo wa Ki-CCM wasiojali wananchi. Bado wananchi wa Tanzania zaidi ya 60% ambao hawahusianishi kuzaa na hali za kipato chao. Bado kwa kaya nyingi za Tanzania wana msimamo kuwa kila mtoto anakuja na baraka zake
 
Ameongea vizuri tu.Ni mapokezi na tafsiri ya maneno.Mkiwapa wake wenu ujauzito muwaandalie vifaa na fedha za dharula.Rahisi tu.Dezodezo hakuna.Kipi kigumu kuelewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…