CHADEMA anzisheni kituo cha television kabla ya uchaguzi wa 2025

Mim ni bawccha ila nachelea kusema sijui tutakuw na sera ipi mana viongoz wetu wamekua wakidandia sana tunakua hatuelewek.justice formdee
 
NIMEANDIKA SANA KUHUSU HILI HITAJI LA MUHIMU! MBOWE TAKE ACTION.......
 
NI kama Chadema hakiko serious kukiondoa CCM madarakani. Ni kama kimeamua tu kuwa chama Cha upinzani lakini si kutaka kushika dola! Kinawwudhi wapenda mageuzi.

Yapo mambo kadhaa ambayo kiukweli kimefanya vizuri na kufanikiwa na kinastahili pongezi.

Kikiwa hakijilikani sana chini ya Dk. Slaa Chadema kilianzisha programu ya kuwashika wanafunzi wa vyuo vikuu ambao waliporudi majumbani "walimwaga simu" kwa wanavijiji kuhusu demokrasia. Ikumbukwe wasomi huaminika sana vijijini. Sumu hii ilizaa uelewa mkubwa kiasi cha Serikali kupiga marufuku siasa vyuoni. Lakini iliwaongezea Chadema kuzama mioyoni mwa Watanzania wengi hususan vijana.

Chadema kilitumia vibaya tangazo la UKUTA. Hii ilikuwa ni fursa muhimu kukiondoa CCM madarakani hata kama damu ingemwahika. Hakuna ukombozi bila ya damu. Kinachomwagiwa damu Mashariki ya Kati baina ya Israeli na Palestina ni ukombozi.

Programu ya Chadema Msingi imekieneza mno Chadema nchini. Kongole kwa waliobuni jambo hilo. Lakini nchi hii ni kubwa mno ndugu zangu. Hamkufika kila mahali na kwa kila mtu.

Nawashauri kwa sasa tumieni fedha kidogo kuanzisha Kituo Cha Redio. Tafiti nyingi zinaonesha Watanzania 67% hupata taarifa kupitia redio. Msihadaike na social media. Matangazo ya urembo kwenye smartphones ni mbwembwe tu. Ni muhimu lakini msidhani mama yangu kule kijijini anaweza kupangusa simu janja kumuona Mbowe kwenye chopa. Sipingi matumizi ya smartphones kueneza chama lakini mjiulize mnawafikia wangapi?

Redio hata Mzee pale Kijiji akiwa shambani anapalilia lakini pembeni anayo karedio kake anapata somo la Uraia. Hapo ndipo CCM inapopatia wapiga kura.

Acheni mbwembwe nendeni kijijini kupitia redio kuvuna watu mijini tayari wamesharevuka. Sasa muwe na operesheni "Chadema Vijijini". Tokeni town tayari mnajulikana.

Msihadaike na mikutano mikubwa ya kudai Katiba Mpya. Kupitia redio mtatoa elimu juu ya Katiba Mpya saa 24 na mtaeleweka. Mkutano mmoja mkubwa hautoshi. Mliwahi kumiliki gazeti la Tanzania Daima lakini nalo halikutosha maana lilitoa nakala 10000 kwa Watanzania 60m. Nawaambia anzisheni radio station.

Kuna ushindi ambao hata mwizi wa kura anaogopa na hii hutokana na wingi wa kura unaoweza kutokana na uelewa wa mabadiliko. Hivi mnadhani huko kijijini wazee wangu wanamjua Mdude Nyangali? Nendeni vijijini kupitia redio mnakiondoa CCM madarakani asubuhi sana.
 
Ikiwezekana hata tv station
 
Vyombo vikuu vya habari hawatangazi shughuli za Chadema. Siyo haki kwa TBC na hata ITV kufamya kazi kama mali ya CCM.

Ni muhimu Chadema kuanzisha vyombo vyao vya habari. Sina shaka kukiwa na TV Chadema itapata watazamaji wengi sana.

Siyo kazi ndogo kuanzisha TV lakini Chadema siyo chama kidogo. Buy an existing TV company if you can
 
Nimelipigia kelele sana hili...
 
Chama kilikuwa busy kujenga nyumba ya mwenyekiti kwanza kupitia ruzuku ya chama, ili afaidi matunda ya uenyekiti wake wa miaka zaidi ya 20 chamani.

Hilo swala la TV kwa sasa halina tija yoyote kwa chama. Kama unakipenda chama, hata wewe unaweza kuanzisha TV ya chama alaf chama kitakuunga mkono kijana.
 
Tatizo lako ni hilo hilo na la tumehuru. Ukweli ni kwamba vyombo vya habarihavipi kura, ila wajumbe wa tume kila mtu anayo kura moja moja tu. Utashindwa kwa kura si kwa tume. Kuna TV 19 sasa hivi hapa Tanzania, TV ya umma ni TBC pekee, yaani 1 out of 19. Kuna BBC na CNN na DW zote hizi si za CCM. Ni sawa kulalamika hivi ili ujifariji mara pale kura zitakapohesabiwa kuwa Magufuli 83% tundulissu 17%. Too bad.
 
Hili neno!, angalia hili ni bandiko la lini Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ... hivyo alipokuja Mwamba wa Kaskazi nilisema Elections 2015 - Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!

Ushauri huu niliwapa toka 2012!, asante sana kwa kuliona leo 2023!.
Mungu ibariki Chadema iweze!
Mungu ibariki Tanzania

P
 
Wanaamini katika nguvu ya ummma hawana sababu ya kumiliki vyombo vya habari kwani wanao watu wanaoweza ropoko chochote kile kitakacho ,mfano Lema na Lissu ni vyombo vya habari tosha
 
Actually, Tundu Lissu ni GENIOUS. Ila hawezi kufurukuta kwa waliomzunguka.
 
Bwna moshi wewe ni wa kaskazini unaonaje mkaitisha harambee kwa ajili ya kmchangia kamanda mbowe ili cdm ianzishe TV yake?
 
Hivi shida nini inayokwamisha CHADEMA kwa uwingi wa wanachama isione umuhimu WA kuwa na TV STATION NA RADIO. SASA HIVI HATUPATI TAARIFA HALISI. CHADEMA ANZISHENI TV NA RADIO STATION
 
WAZO ZURI SANA

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…