Friends and Our Enemies,
Tulishawaeleza Chadema na wana harakati uchwara ambao walishiriki kwa kiasi kikubwa kuhamasisha fujo na vurugu kabla na baada ya uchaguzi mkuu ya kwamba hawatoboi.
Pamoja na kwamba chadema walipata nguvu kubwa kutoka kwa baadhi ya makanisa na wanaharakati uchwara ndani na nje ya nchi mwisho wa siku wameangukia pua.
Walitaka nchi hii isitawalike eti kisa wao tuh wamegomea kushiriki uchaguzi na kuhamasisha vurugu siku ya upigaji kura kwa kudhani eti nia yao ovu itafanikiwa.
Wamefeli,wakaja na propaganda za kuichafua Tume ya Jaji chande ili ionekane haijafanya kazi kwa weledi na kuhamasisha umma usikubaliane na Tume hiyo.
Wamefeli na hilo pia,kwani ile ilikua ni tume ya Rais na inawajibika kwa Rais ambae wao hawamtambui kwahiyo waache ngenga zao.
Baada ya kuona wamechemka katika hila zao zote sasa wameamua kuja na maigizo yao ya kutekana.
Chadema hakuna mjinga ambae anaweza kuwaamini kwa hayo maigizo yenu.
Nchi iko salama na serikali iko imara.
Soma pia