PreGE2025 CHADEMA; baada ya tamko la kutoshiriki Uchaguzi Mkuu, fanyeni haya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ccm na watu wake ndio adui mkuu wa Tanzania
umaskini wa akili na fedha, ujinga na maradhi wanavionea tuu kwa sababu vinaletwa na ccm tangu zamani hata sasa
 
Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako. CCM yako ni laana kwa Taifa hili,na wote wanaoiunga mkono wamelaaniwa.
 
Nilikuwa nadhani una mawazo yenye maana kumbe unawaza CCM kuionea huruma Chadema.

Niliona umeandika kwa busara nikasema nisikilize hoja zako ili walau tuombe chadema wazitumie hizo, lakini nikiri huna maana

kwanza unadai huna hakika ya madai ya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi, wewe uko Tanzania au ughaibuni? Kwamba hujui mambo yaliyotokea uchaguzi wa 2019,2020 na ule wa 2024.

Pili, unaona kama chadema ndio yenye changamoto ilihali Serikali na Chama tawala ndio wenye matatizo.
Waangalizi wa uchaguzi tangu mwaka 1995 na tume mbalimbali zimedai mabadiliko yanayohitajiwa na chadema

Yote hayo muhimu hujasoma unaona ubaya wa njia zinazotumika kutafuta haki.

Kwa hali ya nchi yetu ilivyo nitawaunga mkono chadema kwa mipango na mbinu yeyote wanayoileta kwetu wananchi maana busara kwa CCM ni kusukuma ukuta
 
Nashukuru sana ndugu yangu japo sijapenda kumtukana yeyote kwenye ukurasa huu akiwemo Madame Maria Sarungi kwani mimi nawaheshimu watu wote; wakiwemo CCM, CHADEMA, ACT, n.k

Kuhusu kutumia maneno yenye lugha chafu na yenye kuhamasisha vitendo hasi badala ya kuenenda kwa utaratibu, hekima, lugha ya ulimi laini wenye kuvunja mfupa na kufanya vitendo chanya ndiyo gharama kubwa inayowagharimu upinzani; lakini mbaya zaidi ni kwamba hawataki kuukubali ukweli.

Zipo fursa nyingi sana kwa jamii ambazo upinzani wakizichangamkia hawatokaukwa mate tena kushindana na CCM, hawatoumiza kichwa wala kutumia nguvu kubwa kushindana na CCM, watajikuta tu automatically wamefika wanapopataka.

Tatizo moja tu linalowakabili upinzani hususan CHADEMA; ni kwamba hawataki kusikia ukweli mchungu utakaowaponya na kuwavusha salama ila wanataka kusikia uongo mtamu utakaowaangamiza milele.
 
Sijawahi kwenda shule peku namshukuru MUNGU, lakini pia hii ndiyo imenifanya niwape challenge wapinzani kwamba washindane na CCM kwa vitendo chanya ili Tanzania ipate maendeleo makubwa zaidi kuliko wanavyoshindana kwa maneno dhaifu na kuhamasisha vitendo hasi huku wimbi kubwa la Watanzania wakilalia mlo mmoja au kula chakula kisichofaa.

Lengo la waraka huu mimi kama mtanzania nisiye CCM wala CHADEMA ni kwamba tumechoka kusikia maneno yenu wanasiasa kila siku mkilumbana nyinyi kwa nyinyi huku vitendo chanya vikibaki kwa chama tawala pekee ambao nao bado tunawahitaji waweke nguvu kubwa kwenye siasa za kiutendaji zaidi kuliko maneno sisi hatutaki maneno na hatutaki kila siku mgombane nyinyi kwa nyinyi siasa za namna hii tumezichoka tunataka za vitendo chanya.

Kuhusu Nyerere alifanya nini ni lazima tukumbuke kwa sababu pamoja na udhaifu wake wote asiyetambua mchango wa yule mzee kwenye taifa hili basi hastahili kuitwa mzalendo.
 
Ninyi ndio mnaotuletea maigizo; kwa sababu mnafahamu dhahiri kuwa kupikwa, kuiva, kupakuliwa na kuliwa kwa sheria yoyote ili Tanzania basi jikoni kwake ni Bungeni. Too bad! Ni nyinyi haohao tena mnaotaka sheria zirekebishwe mnaokataa kushiriki Uchaguzi Mkuu kama njia ya kuwapeleka huko jikoni mkapike huko, mkaivishe, mkapakue wananchi wale halafu mnakuja kuniandikia mwananchi wa Tanzania kama mimi eti 'NO REFORMD NO ELECTION' mimi ni bunge?

Kama hamtatafuta njia na namna ya kwenda bungeni ili mwende mkaisemee huko hii 'NO REFORMS NO ELECTION' yenu msije mkawaza kwamba mtapata suluhu kupitia mitaani, vijiweni au kwenye mitandao ya kijamii.

Huku wapo wananchi wa kawaida kabisa na hawana cha kuwasaidia hebu kubalini ukweli basi.
 
Kwako wewe mambo kama haya ikiwa ndiyo hekima basi una tatizo kubwa kwenye ubongo wako. Chadema wanachopigania ni kuwa uchaguzi ulio huru na haki na wenye kuaminika na wala hawahitaji fadhila wa huruma yoyote katika uchaguzi na hili siyo kwa faida ya Chadema tu bali ni kwa vyama vyote na wapiga kura wote. Kwa kilichotokea 2019, 2020 na 2024 inahitaji akili ya mwenda wazimu kwenda kusimama foleni na kupiga kura ambayo unajua kuwa haina thamani. Na pia ni utaahira mkubwa sana kushiriki uchaguzi ambao unajua kwa 100% kuwa hata ukishinda hutatangazwa kuwa umeshinda. Na pia ni upumbavu hata kwa serikali kutumia zaidi ya nusu trillion ya kodi zetu kuandaa na kuendesha igizo linaloitwa uchaguzi mkuu. Ni bora waendelee tu waliopo Rais ,wabunge na madiwani wa CCM na hizo fedha zikaelekezwa kwenye hudumua za kijamii kama Afya na Elimu.
 

Attachments

  • downloadfile-24.jpg
    38.4 KB · Views: 22
  • downloadfile-35.jpg
    44.8 KB · Views: 20
  • 6021056-bf15b8f6f927c72fa16d6bb328a5e41f.mp4
    14.1 MB
  • 5723085-f2958354fb3d5c7668951cd04505632.mp4
    16 MB
Asipoelewa na maelezo yote haya pamoja na picha basi haitaji kuielewa chadema.

Chadema haina vichaa kwamba ianze tu kuwa na hasira. Kuna mahali unafikishwa hata kama ni mpole kiasi gani lugha inayobaki ni kupambana tu
 
Yaani CCM mnatakiwa kunyongwa mpaka kufa nyote bila aibuu unamtaja Mungu kwenye ujinga wewe akili huna kabisa wewe ni kipofu na mwizi.
Si kosa lako; tatizo macho ya nyama hudanganya sana na ndiyo hayo yalimtamanisha Hawa mpaka akala tunda ambalo MUNGU Aliwakataza wasile. Ni maombi yangu macho yako moyoni yatiwe nuru siku moja uone na ung'amue upumbavu uliouandika hapa, hata ujiulize hivi huyu aliyecomment hapa alikuwa ni mimi?
 
Siku mtakayoukubali ukweli kuhusu nyinyi wenyewe, ili mbadililike nyinyi kwanza vyama vya upinzani hususan CHADEMA; ndiyo siku ambayo magumu mnayopitia sasa hamtayaona tena.
 
Ccm na watu wake ndio adui mkuu wa Tanzania
umaskini wa akili na fedha, ujinga na maradhi wanavionea tuu kwa sababu vinaletwa na ccm tangu zamani hata sasa
Sijakataa huenda ni kweli kabisa 100%; lakini swali langu kwenu CHADEMA ni hili, nyinyi kama Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania chenye umri mkubwa, wadau wengi wa kitaifa na kimataifa, ushawishi, nguvu lakini pia wanachama wengi kuliko chama chochote cha upinzani cha Tanzania; ni lipi (au niseme kipi) mmefanya kwa Tanzania kwenye sekta yoyote ya kijamii kama vile Teknolojia, Elimu, Afya, Uchumi, Chakula, Kilimo, Madini, n.k kwa ajili ya Watanzania? Au nyinyi ndio watazamaji wa vibanzi ndani ya macho ya wenzenu na boriti ndani ya macho yenu wenyewe hamziangalii?
 
Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako. CCM yako ni laana kwa Taifa hili,na wote wanaoiunga mkono wamelaaniwa.
Usihukumu usije ukahukumiwa, kwa maana kipimo hiki unachowapimia CCM ndicho ambacho huenda MUNGU Anakitumia kuwapimia CHADEMA. Kubalini ukweli kuwa wenzenu legacy yao ni kubwa na msingi wenye mizizi mirefu; mtaishia kuwalaumu wanawaibia kura bure na wakati ukweli ni kwamba nyinyi kuna maeneo hamjulikani kabisa na hata kama wanawafahamu hamjawahi kuwafanyia chochote kugusa mioyo yao.
 
Lengo si CCM kuionea huruma CHADEMA; lengo ni kama hayo madai yaliyodaiwa yapo kweli kwa vyombo vya dola; nimeshauri kuwa basi CHADEMA waanze wao kufuata utaratibu, kuwa wema zaidi na kuenenda kwa upole na utulivu ili wasivipe sababu vyombo vya dola.

Siwezi kuthibitisha jambo ambalo ni nadharia sikulifanyia utafiti, lakini pia siwezi kuamini matokeo ya tafiti na kutoka kwa watu ambao ni wa nje wa taifa hili; kwani haya ni mambo ya ndani wa nje anaweza kusema chochote ili tu familia igombane hivyo naomba nirudie kwa herufi kubwa SIJATHIBITISHA.
 
Legacy ya wizi wa kura na kuifisadi nchi kwa kuingia mikataba ya kimangungo,utakuwa chawa wewe.
 
Wewe unajifanya kichaa somo ripoti ya Prof. Mkandala
Alikuwa mkuu wa chuo cha Dar es Salaam


Au Naye anataka tuvurugikiwe?

CCM ni kama shetani Yohana 10:10
Ataiba rasilimali za nchi, ataiba Kura, atavuruga utaratibu wa demokrasia na ukifanya unahoji utapotezwa, utauwawa au kufunguliwa kesi ya ugaidi au uhaini.

wewe kama haoni mambo yaliyofanyika bandari kupewa DPWorld, rasilimali zote kupewa wahindi,waarabu, na macartel ya ulaya na marekani.
 
Nimegundua sasa kuwa mnayo changamoto nyingine ya kutokujiamini, hofu na woga. Changamoto haikimbiwi; Changamoto inakabiliwa KIUME WAMBA! Samson alikutana na simba, hakukimbia bali alipigana naye akamrarua vipande akaenda zake alikokuwa anaenda, wakati wa kurudi hakusema ile njia siipiti tena kwani ina simba; Alijivika ujasiri wa kiume alipita njia ileile tena kwa kujiamini.

Good news ni kwamba, safari hii hakukutana na simba (changamoto) ila aliukuta mzoga wa yule simba aliyemuua mwanzoni ndani yake una asali. Akaichukua, akaila mwanaume. Haya hebu jiulize, angehofia kupita njia hii kisa mwanzoni alikutana na simba, asali angeipata?

Sasa kwa kuukimbia uchaguzi huu wa 2025 tafsiri yake ni kuwa nyinyi hata mkipata madaraka changamoto ndogo inaweza kuwafanya mkalikimbia taifa. Tiba si kuukimbia uchaguzi au kuleta vikwazo na visingizio kwenye uchaguzi, tiba ni kuingia na kutokoma kuingia kwenye uchaguzi mpaka kieleweke, mpaka mpate asali yenu na nyinyi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…