Capital
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 1,508
- 1,104
Hapa umeandika T A K A T A K A boss.. CDM ni jitu kubwa hivi, CCM itatema ndoano mwaka huu.. tuko palee..Hata dhahabu mwanzoni huonekana kama takataka; ila mwisho wake ndio huwa mtamu
Hapa umeandika T A K A T A K A boss.. CDM ni jitu kubwa hivi, CCM itatema ndoano mwaka huu.. tuko palee..Hata dhahabu mwanzoni huonekana kama takataka; ila mwisho wake ndio huwa mtamu
Kwanza mimi sio chadema na wala sishabikii upumbavu unaoitwa chama cha siasa nilicho andika mimi ni ukweli kua adui wa Tanzania ni ccm na watu wake, kila mwenye akili timamu analijua hiloSijakataa huenda ni kweli kabisa 100%; lakini swali langu kwenu CHADEMA ni hili, nyinyi kama Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania chenye umri mkubwa, wadau wengi wa kitaifa na kimataifa, ushawishi, nguvu lakini pia wanachama wengi kuliko chama chochote cha upinzani cha Tanzania; ni lipi (au niseme kipi) mmefanya kwa Tanzania kwenye sekta yoyote ya kijamii kama vile Teknolojia, Elimu, Afya, Uchumi, Chakula, Kilimo, Madini, n.k kwa ajili ya Watanzania? Au nyinyi ndio watazamaji wa vibanzi ndani ya macho ya wenzenu na boriti ndani ya macho yenu wenyewe hamziangalii?
sidhani kama kuna mtu atakaa kusoma hilo gazeti lako, inshort chadema wanapambania ni free and fair election na sio hayo ulioyaandika humo. Kama CCM wataweza kuweka usawa kwenye chaguzi wakashinda basi ni haki watawale mpaka watanzania waseme po!SEHEMU YA PILI
Katika muendelezo wa makala hii sehemu ya pili,
Ninapenda kuanza kwa Kumshukuru MUNGU kwa mara nyingine tena, kisha kundelea na ushauri wa bure wa pili kwa ndugu zangu au ndugu zetu CHADEMA. Tunafahamu kuwa Taifa la Tanzania ni Taifa lenye sheria, kanuni, taratibu na katiba yake lakini sambamba na hivi vitu, Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali yake ni wasikivu na wako tayari kwa maridhiano muda wowote ule.
Ni kweli kuwa jana ilitoka taarifa kuwa CHADEMA haitoshiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025 kwa sababu ya kukataa kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi. Ni imani yangu kuwa kichwa hiki cha habari kinaweza kubadilika muda wowote iwapo CHADEMA mtaamua kulegeza kamba, kujishusha na kukubaliana na mamlaka ili na nyinyi muweze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Nafasi ya Urais inaweza kuwa hapana kwa sasa kwenu, lakini nafasi za Ubunge na Udiwani zinaweza kuleta tija zaidi kwenye chama chenu kwa sasa kwani hata vingi mnavyovilalamikia sasa vinaweza kupata muafaka mkiwa mjengoni, kwenye mabaraza ya kata, majimboni, nk.
Je! Mmewahi kuwaza kuhusu hali za watu mbalimbali wa chama chenu kama kaka Joseph Haule 'Professor Jay' ambaye amepitia changamoto kubwa miaka ya hivi karibuni ambayo imempelekea kuyumba kiuchumi, n.k. Lakini sasa afya yake imeimarika na ninaamini labda (sijathibitisha) kupitia chama chenu anaweza kusimama tena jimboni Mikumi, akagombea na kupita kisha akawatumikia wananchi lakini akajiimarisha yeye mwenyewe upya; kiuchumi, kijamii, n.k.?
Je! Mmewahi kuwaza kuhusu vijana wa chama chenu wenye ndoto ya kufanya kampeni, kugombea na kuongoza kwenye Taifa hili; ni kwa namna gani mnawazima ndoto zao kwa kung'ang'ania mambo msiyojua muafaka wake utapatikana lini? Je! Mtamlaumu nani mkiwapoteza vijana hao wakimbilie kwenye vyama vingine kama CCM ili wakatimize ndoto zao?
Je! Mmewahi kuwaza kuhusu wanachama wenu waliojiandikisha kwa mapenzi ya moyoni na ya dhati kabisa ili siku ya uchaguzi aipigie kura CHADEMA; lakini ni nyinyi wenyewe ndio mmekatisha hili? Mmeshahesabu gharama ya hiki mnachokifanya sasa; kina faida kiasi gani au kina hasara kiasi gani kwa chama chenu wenyewe na wafuasi wake?
MJITATHMINI, MJIFIKIRIE UPYA, PUNGUZENI HASIRA IKIWEZEKANA MZIACHE KABISA; kwani waswahili husema: "Hasira hasara na hasira ya mkizi furaha ya mvuvi."
Wewe ni chawa hii spinning unavyofanya haiwezi kuwatoa kwenye mtazamo wenye akili,mamilioni ya Watanzania wametuelewa na hatugeuki nyuma, tunakupuuza. Wameshindwa wenye bunduki na mabomu utaweza wewe,don't waste your breath we are not buying your product.Si kweli na haiwezi kutokea kwa sababu tunaamini Rais wetu ni mwenye akili timamu, utu, wema, hekima na msikivu hivyo hawezi kufanya jambo la ukatili kama hili. Mtu mwenye adabu na aliyelelewa kwenye maadili hawezi kutamka uchafu huu kuhusu Mhe. Rais haijalishi anatokea chama gani.
Hii ndiyo sababu nimesema vyama vya upinzani vina kazi kubwa ya kufanya; kuanzia kwenye kurekebisha wafuasi wao, wanachama wao, wadau wao na wao wenyewe kabla ya kutafuta mchawi nani.
Ww huset standards za chama Cha upinzani kiweje..Baki na ideologies zako za KiCCM..sio lazima zifatwe na vyama vyote vya siasa.Siku mtakayoukubali ukweli kuhusu nyinyi wenyewe, ili mbadililike nyinyi kwanza vyama vya upinzani hususan CHADEMA; ndiyo siku ambayo magumu mnayopitia sasa hamtayaona tena.
Ndoano lazima itoke na maini.....Hapa umeandika T A K A T A K A boss.. CDM ni jitu kubwa hivi, CCM itatema ndoano mwaka huu.. tuko palee..
Ukubwa unapimwa na nini kwani samahani?Hapa umeandika T A K A T A K A boss.. CDM ni jitu kubwa hivi, CCM itatema ndoano mwaka huu.. tuko palee..
Haijalishi adui wa taifa hili awe ni CCM, CHADEMA au chama chochote kile mimi sijui na sitaki kujua kuhusu hilo, wananchi tunasema hivi, tumechoka na hatuzitaki siasa zenu za maneno tunataka siasa za Vitendo tena VITENDO CHANYA nukta.Kwanza mimi sio chadema na wala sishabikii upumbavu unaoitwa chama cha siasa nilicho andika mimi ni ukweli kua adui wa Tanzania ni ccm na watu wake, kila mwenye akili timamu analijua hilo
Kikubwa ujumbe ufike kata kwa kufanya skimming and scanning.Sid
sidhani kama kuna mtu atakaa kusoma hilo gazeti lako, inshort chadema wanapambania ni free and fair election na sio hayo ulioyaandika humo. Kama CCM wataweza kuweka usawa kwenye chaguzi wakashinda basi ni haki watawale mpaka watanzania waseme po!
Mimi si chawa, sijawahi kuwa chawa na sina mpango wa kuwa chawa. Mimi ni Mtanzania; mwananchi niliyechoshwa na siasa zozote zile zenye maneno mengi, lugha chafu, kashfa, matusi, kuvunjiana heshima na zisizo na tija kwa wananchi. Napenda kuona siasa za kimya kimya zenye VITENDO CHANYA zaidi nchini Tanzania kwa manufaa ya Watanzania.Wewe ni chawa hii spinning unavyofanya haiwezi kuwatoa kwenye mtazamo wenye akili,mamilioni ya Watanzania wametuelewa na hatugeuki nyuma, tunakupuuza. Wameshindwa wenye bunduki na mabomu utaweza wewe,don't waste your breath we are not buying your product.
Una uhakika vyama vya upinzani nchini Tanzania viko 100% perfect?Ww huset standards za chama Cha upinzani kiweje..Baki na ideologies zako za KiCCM..sio lazima zifatwe na vyama vyote vya siasa.
Siasa si ugomvi; sisi sote ni Watanzania.Kelele za nini nyie chawa wa kijani,si tayari tushawapa ushindi?
Hizi nadharia zako akizikia mtu asiyejua ukweli ataamini. Ni mara moja au 2 cdm wametaka kupeleka huduma kwa jamii na wanakaliwa? Ni mara ngapi cdm walitaka kufanya miradi kwenye halmashauri wanakataliwa na wakurugenzi kwa kuwaambia ilani inayotekelezwa ni ya ccm na sio ya cdm. Mfano halisi, mwaka 2011 cdm walitaka kutoa elimu bure kwa shule za msingi katika manispaa ya moshi, mkurugenzi akakataa kwa kusema haiko kwenye ilani ya ccm?Una akili nzuri sana!
Waraka wako umeshiba na umekwenda Shule!
CHADEMA wana viongozi, wanachama na mashabiki wenye upeo mdogo sana!
Wao wanadhani kwa kujenga hasira kwa wananchi basi watapewa mamlaka!!! Too myopic!
Ingia kwenye mioyo ya watu kwa kutatua changamoto zao na siyo kuropokaropoka tu!
Mfano kama CCM wameshindwa kutoa elimu bora basi CHADEMA walikuwa na nafasi hata ya kuwa na Shule zao kadhaa za mfano za kuonyesha Watanzania namna elimu inavyopaswa kutolewa na kuwajengea Wananchi Imani kwamba endapo wakipewa ridhaa na wakawa na mamlaka ya kukusanya Kodi basi wanaweza kuwafanyia Watanzania maajabu!!
Imewachukua zaidi ya miaka 30 kupata ofisi ya Chama ambayo pia bado Haina hadhi kulinganisha na kelele zao na umri wa CHADEMA.
CHADEMA ni chama useless kinachoongozwa na failures kama akina Maria Sarungi!!!
Nashukuru sana ndugu yangu
Naomba niseme kuwa sijafanya utafiti kuthibitisha kama hayo uyasemayo yapo ama la, lakini kama ni kweli yapo Ili kukabiliana nayo; vyama vya upinzani hususan CHADEMA vinapaswa kutumia akili zaidi na vitendo chanya zaidi kwa jamii ili kudhihirisha utu wao wema na ulio chanya zaidi mpaka ifike hatua hata vyombo husika vyenyewe viseme hawa tukiwafanyia tofauti tutakuwa tunawaonea hebu twende nao kwa haki.
Kutumia lugha chafu na uhamasishaji wa vitendo hasi mara kwa mara kiukweli ndiyo sababu ambayo inawa-cost vyama vya upinzani kama Chadema; kwani vyombo kama vyombo vya dola kazi yao ni kulinda usalama; hivyo mtu yeyote anayetishia usalama katu hawezi kuwa rafiki kwao na hii ipo hivi kwa chombo cha usalama cha nchi yoyote ile.
Ile lugha ya Makala kuwa cdm wamepanga kuingiza m-pox ama ebola unaichukuliaje, au kwako busara na lugha mbaya zina macho? Hujafanya utafiti wa tabia za ccm, lakini una bandiko refu la mapungufu ya cdm na nini wanatakiwa wafanye. Hili bandiko lako linaonekana ni la mtu aliye nje ya nchi, na uandishi wako umejikita kwenye nadharia na sio uhalisia. Siku ukirudi hapa nchini uje uangalie uhalisia ndio uandike utafiti wako wenye mahaba ya ccm.Nashukuru sana ndugu yangu
Naomba niseme kuwa sijafanya utafiti kuthibitisha kama hayo uyasemayo yapo ama la, lakini kama ni kweli yapo Ili kukabiliana nayo; vyama vya upinzani hususan CHADEMA vinapaswa kutumia akili zaidi na vitendo chanya zaidi kwa jamii ili kudhihirisha utu wao wema na ulio chanya zaidi mpaka ifike hatua hata vyombo husika vyenyewe viseme hawa tukiwafanyia tofauti tutakuwa tunawaonea hebu twende nao kwa haki.
Kutumia lugha chafu na uhamasishaji wa vitendo hasi mara kwa mara kiukweli ndiyo sababu ambayo inawa-cost vyama vya upinzani kama Chadema; kwani vyombo kama vyombo vya dola kazi yao ni kulinda usalama; hivyo mtu yeyote anayetishia usalama katu hawezi kuwa rafiki kwao na hii ipo hivi kwa chombo cha usalama cha nchi yoyote ile.
Hapa naomba nisaidie; huenda wao CHADEMA walitaka wapeleke huduma kwa jamii kama serikali (hili linaweza kuleta changamoto kweli) lakini kuna alternative ya kupeleka huduma kwa jamii kama taasisi binafsi; na hapa ndiyo maana unaona makanisa na misikiti inamiliki shule, vyuo, hospitali, benki na taasisi nyingine za kijamii pasipo kuingiliana wala migogoro na serikali.Hizi nadharia zako akizikia mtu asiyejua ukweli ataamini. Ni mara moja au 2 cdm wametaka kupeleka huduma kwa jamii na wanakaliwa? Ni mara ngapi cdm walitaka kufanya miradi kwenye halmashauri wanakataliwa na wakurugenzi kwa kuwaambia ilani inayotekelezwa ni ya ccm na sio ya cdm. Mfano halisi, mwaka 2011 cdm walitaka kutoa elimu bure kwa shule za msingi katika manispaa ya moshi, mkurugenzi akakataa kwa kusema haiko kwenye ilani ya ccm?
Baada ya uchaguzi wa 2015, cdm walipata halmashauri nyingi, Magufuli kwa ajili ya wivu wa kisiasa akasema pesa zote zikusanywe na TRA, kisha ziingie hazina na halmashauri ziombe fedha za matumizi huko. Sio mara moja au 2 wakuu wa hospitali ama shule hukwepa kupokea misaada ya wanacdm, na kusema ni maagizo toka juu?
Unajua unachoongea au nibaki kwenye hilo neno lako huenda? Kama hujafanya utafiti ni bora kukaa kimya, ama andika kama mshabiki wa ccm. Taasisi za dini zina madhara gani kwa madaraka ya ccm. Hebu kaa kimya ndugu maana una nadharia zisizo na uhalisia.Hapa naomba nisaidie; huenda wao CHADEMA walitaka wapeleke huduma kwa jamii kama serikali (hili linaweza kuleta changamoto kweli) lakini kuna alternative ya kupeleka huduma kwa jamii kama taasisi binafsi; na hapa ndiyo maana unaona makanisa na misikiti inamiliki shule, vyuo, hospitali, benki na taasisi nyingine za kijamii pasipo kuingiliana wala migogoro na serikali.
Ndugu yangu, mimi nimesema vyama vyote nchini Tanzania tumechoka kusikia vikitukanana, kukashfiana, kusemana vibaya, kunyukana, kuvinjiana heshima, n.k. tunahitaji siasa za VITENDO CHANYA. Kiukweli kabisa hii ni kwa wote; CCM, CHADEMA, ACT na vyama vingine vilivyosalia.Ile lugha ya Makala kuwa cdm wamepanga kuingiza m-pox ama ebola unaichukuliaje, au kwako busara na lugha mbaya zina macho? Hujafanya utafiti wa tabia za ccm, lakini una bandiko refu la mapungufu ya cdm na nini wanatakiwa wafanye. Hili bandiko lako linaonekana ni la mtu aliye nje ya nchi, na uandishi wako umejikita kwenye nadharia na sio uhalisia. Siku ukirudi hapa nchini uje uangalie uhalisia ndio uandike utafiti wako wenye mahaba ya ccm.
Mwandishi yuko sahihi;Hongera kwa uandishi na mawazo mazuri.
Tuna tatizo kubwa la vyombo vya dola kuingilia uchaguzi na kuuwa wagombea na wanachama vipi hayo yatakabiliwa vipi kabla ya kutoa wanachama rahani ya kafara ya uchaguzi.
Pili, tunachangamoto kubwa mamlaka zinazopaswa kusimamia uchaguzi kama tume na wakuu wa serikali kunyang'anya kwa maksudi sauti ya wananchi?
Bandiko lako lilikuwa kuidunisha cdm na sio ccm ama vyama vingine. Au umezidiwa na hoja sasa unarukia chochote? Ni wapi umetaja vyama vinginge zaidi ya cdm against ccm? Nenda kwenye post yako namba moja kama kuna popote umeonyesha kuikanya ccm ama vyama vingine. Kama huna uelewa wa mambo, usijifanye mcha Mungu huku ukifumbia macho ukweli.Ndugu yangu, mimi nimesema vyama vyote nchini Tanzania tumechoka kusikia vikitukanana, kukashfiana, kusemana vibaya, kunyukana, kuvinjiana heshima, n.k. tunahitaji siasa za VITENDO CHANYA. Kiukweli kabisa hii ni kwa wote; CCM, CHADEMA, ACT na vyama vingine vilivyosalia.