PreGE2025 CHADEMA; baada ya tamko la kutoshiriki Uchaguzi Mkuu, fanyeni haya

PreGE2025 CHADEMA; baada ya tamko la kutoshiriki Uchaguzi Mkuu, fanyeni haya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mwandishi yuko sahihi;

Hilo tatizo la uchaguzi ni dogo sana; mfano upinzani unaweza ukasimamisha watu mahiri majimboni ambao wanauzika bila hata kuhitaji msaada wa chama? CCM wamefanikiwa hapo, kwanza wana chama imara lakini wana watu wanaouzika kwenye jamii. Mfano pale Kahama unadhani ni rahisi sana kumshinda Kishimba??? Ni kama ilivyokuwa ile moshi ya Ndesamburo (ukiacha xhama chake lakini Ndesa alikuwa system imara sana na alifanya mambo mengi kwa watu wote CCM na CDM kiasi kwamba kumshinda ilikuwa next to impossible ) Bado safari ni ndefu sana aisee, wanakwenda spidi mno. Mfano baada ya halima kununuliwa pale Kawe kuna mwanachadema yupi mwenye nguvu angalau nusu ya halima? Ukifikiria kwa mapana unaona mwandishi yuko sahihi sana.
Ndio maana tunataka ushindani wa haki, utaona watu ambao hujawahi kuwaona. Wengi hawana ujasiri wa kujitokeza kwenye chaguzi za kihuni. Kutokujua watu waliopo haimaanishi hawapo.
 
Nashukuru sana ndugu yangu

Naomba niseme kuwa sijafanya utafiti kuthibitisha kama hayo uyasemayo yapo ama la, lakini kama ni kweli yapo Ili kukabiliana nayo; vyama vya upinzani hususan CHADEMA vinapaswa kutumia akili zaidi na vitendo chanya zaidi kwa jamii ili kudhihirisha utu wao wema na ulio chanya zaidi mpaka ifike hatua hata vyombo husika vyenyewe viseme hawa tukiwafanyia tofauti tutakuwa tunawaonea hebu twende nao kwa haki.

Kutumia lugha chafu na uhamasishaji wa vitendo hasi mara kwa mara kiukweli ndiyo sababu ambayo inawa-cost vyama vya upinzani kama Chadema; kwani vyombo kama vyombo vya dola kazi yao ni kulinda usalama; hivyo mtu yeyote anayetishia usalama katu hawezi kuwa rafiki kwao na hii ipo hivi kwa chombo cha usalama cha nchi yoyote ile.
Uko sahihi sana Mkuu;

Mfano angalia mkoa wa Geita CDM wanaweza kupata majimbo mangapi tena wakiweka watu sahihi sana? Mkoa wa Singida je? Mkoa wa Tabora je? Mkoa wa Tanga je? mkoa wa Dodoma je? Mkoa wa Simiyu je? Mkoa wa Morogoro je? Mkoa wa Pwani Je? Mkoa wa Katavi Je? lindi?? Shinyanga je? Mtwara? Kigoma ni pro ACT kwa majimbo matatu hivi. Hata kule kwenye ngome zao, mfano Arusha wana majimbi mawili tu (strong red) Kilimanjaro (nako wana majimbo mawili tu strong red) Manyara (wana majimbo mawili tu strong red) Mbeya ni ngome lakini sio full red (wanagawana) halikadhalika Songwe... mara wana majimbo 3 strong red wanakwenda speed bure, kuna kazi kubwa inatakiwa kufanyika kuliko maneno. Ya sasa
 
Ndio maana tunataka ushindani wa haki, utaona watu ambao hujawahi kuwaona. Wengi hawana ujasiri wa kujitokeza kwenye chaguzi za kihuni. Kutokujua watu waliopo haimaanishi hawapo.
Ukiwa na watu kweli hata mzani ukiwaje utashinda tu (too big ti rig) refer kina Ndesa nk shida ni kwamba watanzania tuna hulka za kudeka. Ndicho CDM wanafanya. Kama EL alikuwa very strong lakini aliambulia wabunge 40+ tu katika kipindi ambacho CCM ilikuwa na migawanyiko mikubwa sana sembuse sasa mkuu? Kazi kubwa inatakiwa kufanyika. Kuna wagombea hata hawajulikani, mfano pale Nyamagana pambalu ana nguvu ya kumshinda mgombea strong wa CCM?
 
Unajua unachoongea au nibaki kwenye hilo neno lako huenda? Kama hujafanya utafiti ni bora kukaa kimya, ama andika kama mshabiki wa ccm.
Najua ninachokiongea, na hili swali niliuliza kwenu kuwa ni kipi mmewafanyia watanzania?

Umenijibu sawa, lakini huko walikoenda kwenye halmashauri mimi na wewe hatukuwepo a reason to why nikasema huenda kwa sababu mimi sijafanya utafiti na wewe kwa unavyoongea ni dhahiri kuwa ni maungo aidha ya habari au rumours ambazo na wewe umezisikia tu. Kama ni kweli, tafsiri yake ndicho ninachokipigania mimi; kwamba tumechoka siasa za mivutano, migogoro, kunyukana, kutukanana, n.k. kwani zinarudisha taifa nyuma.

Kingine kwa mfano kufungua 'company ya kuongeza thamani madini' kweli halmashauri nayo inazuia? Haya, ujasiriamali au business entities nayo halmashauri wanazuia? Tuache hayo, na kufungua migahawa ya chakula na ya kitalii nako halmashauri wanazuia? Kuwekeza kwenye utalii na kwenyewe halmashauri wanazuia? Mbona fursa za kijamii ni nyingi sana?
 
Uko sahihi sana Mkuu;

Mfano angalia mkoa wa Geita CDM wanaweza kupata majimbo mangapi tena wakiweka watu sahihi sana? Mkoa wa Singida je? Mkoa wa Tabora je? Mkoa wa Tanga je? mkoa wa Dodoma je? Mkoa wa Simiyu je? Mkoa wa Morogoro je? Mkoa wa Pwani Je? Mkoa wa Katavi Je? lindi?? Shinyanga je? Mtwara? Kigoma ni pro ACT kwa majimbo matatu hivi. Hata kule kwenye ngome zao, mfano Arusha wana majimbi mawili tu (strong red) Kilimanjaro (nako wana majimbo mawili tu strong red) Manyara (wana majimbo mawili tu strong red) Mbeya ni ngome lakini sio full red (wanagawana) halikadhalika Songwe... mara wana majimbo 3 strong red wanakwenda speed bure, kuna kazi kubwa inatakiwa kufanyika kuliko maneno. Ya sasa
Asante nashukuru sana ndugu yangu kwa uchambuzi na kuelewa. High five!
 
Ukiwa na watu kweli hata mzani ukiwaje utashinda tu (too big ti rig) refer kina Ndesa nk shida ni kwamba watanzania tuna hulka za kudeka. Ndicho CDM wanafanya. Kama EL alikuwa very strong lakini aliambulia wabunge 40+ tu katika kipindi ambacho CCM ilikuwa na migawanyiko mikubwa sana sembuse sasa mkuu? Kazi kubwa inatakiwa kufanyika. Kuna wagombea hata hawajulikani, mfano pale Nyamagana pambalu ana nguvu ya kumshinda mgombea strong wa CCM?
Mkuu hakuna mwenye tatizo la kushindwa ama kushinda, tunataka uwanja sawa wa ushindani kisha ulete mrejesho hapa.
 
Najua ninachokiongea, na hili swali niliuliza kwenu kuwa ni kipi mmewafanyia watanzania?

Umenijibu sawa, lakini huko walikoenda kwenye halmashauri mimi na wewe hatukuwepo a reason to why nikasema huenda kwa sababu mimi sijafanya utafiti na wewe kwa unavyoongea ni dhahiri kuwa ni maungo aidha ya habari au rumours ambazo na wewe umezisikia tu. Kama ni kweli, tafsiri yake ndicho ninachokipigania mimi; kwamba tumechoka siasa za mivutano, migogoro, kunyukana, kutukanana, n.k. kwani zinarudisha taifa nyuma.

Kingine kwa mfano kufungua 'company ya kuongeza thamani madini' kweli halmashauri nayo inazuia? Haya, ujasiriamali au business entities nayo halmashauri wanazuia? Tuache hayo, na kufungua migahawa ya chakula na ya kitalii nako halmashauri wanazuia? Kuwekeza kwenye utalii na kwenyewe halmashauri wanazuia? Mbona fursa za kijamii ni nyingi sana?
Hebu ukipata muda fanya utafiti, mimi ninaongea ambacho nina ushahidi nacho. Ww una nadharia za darasani.
 
Hebu ukipata muda fanya utafiti, mimi ninaongea ambacho nina ushahidi nacho. Ww una nadharia za darasani.
Jibu kwanza hili swali ndugu; kufungua bank ya kijamii (community bank) halmashauri nayo inazuia?
 
Nani wafungue community bank, cdm au nani?
Natolea tu mfano wa namna ambavyo huduma za kijamii ni nyingi; na bila shaka CHADEMA wangetaka pia wangeweza kufungua kwani hawasikii malalamiko ya watanzania kuhusu wanavyosumbuka na kuteseka na mikopo ya kausha damu kila siku?
 
Mkuu hakuna mwenye tatizo la kushindwa ama kushinda, tunataka uwanja sawa wa ushindani kisha ulete mrejesho hapa.
It doesn't work like that mkuu;

Upinzani unahitaji agenda setting ambayo haijielekezi kwenye election tu.

Unakumbuka miaka ya 2006 hadi 2012 hivi. Vijana wengi tulivutiwa na CDM kwa sababu ya agenda setting iliyokuwepo; ufisadi nk. Mimi binafsi nimepigwa mabomu mara 3 Arusha mwaja 2009 nadhani; tulioigwa kiwanjani jukwaani akiwepo SG na Chair na baadaye tulitaka tukamchukue mwanachama central. CDM ile ilikuwa na watu wa makundi mengi na wenye kujenga hoja vizuri bila papara; unamkumbuka JJM wa miaka hiyo? ZZK na uchumi wake? Kafulila nk? Leo watu hao wako wapi; kumekuwa na CDM mpya ya waropokaji na watukanaji na washambuliaji...

Imagine kina mdude siku hizi wanapewa mike, kina Sativa wanatukana matusi ya nguoni, kina pambalu wanaishia kupayuka tu hakuna utulivu.... too sad kwa sisi ambao CDM ilituvutia sana; wako wapi wazee wenye busara kama kina baregu, kina Prof Safari nk... kabla ya NRNE CDM inahitaji strategy mpya hii ya sasa ni useless... too sad lakini ndiyo ukweli

Na bahati mbaya vijana wa sasa wa CDM KILA uzi against wao humu majukwaani kazi yao ni kumshambulia mtoa hoja. CDM inazidi kujitenga na watanzania....
 
SEHEMU YA KWANZA

Salaam na heshima nyingi kwenu; Uongozi, Wanachama, Wapenzi na Wadau wote wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Waswahili husema; haraka haraka haina baraka, simba mwendapole ndiye mla nyama, polepole ndio mwendo lakini pia haba na haba hujaza kibaba...

Kwanza, napenda kumshukuru sana MUNGU kwa siku hii ya leo; Jumapili tulivu yenye hali njema ya hewa na kuvutia.

Pili, naomba niende moja kwa moja kwenye lengo nililolikusudia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA). Ninajua na ninafahamu kuwa mioyo yenu inaugua sana kwa sababu ni kwa muda mrefu sasa mmekuwa hamlipati lile ambalo mna shauku nalo na mnalitarajia sana; la kuwa chama tawala ama kwa lugha nyepesi kushika madaraka.

Neno la MUNGU Linasema: "Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana ni mti wa UZIMA." (Mithali (Proverbs) 13:12)

Ni kweli mioyo yenu CHADEMA na Wana-CHADEMA inaugua; lakini hii si sababu ya kutaka kuyaambukiza maumivu hayo kwa kila Mtanzania kupitia kuwalisha sumu kwamba CCM hawafai! CCM ni wakatili! CCM ni wabaya! CCM ni wanyama! Halafu CHADEMA ndiyo chama pekee bora na kinachotakiwa kuwa madarakani! La hasha, huu si Uongozi! Si Utanzania na wala si Utu na Uzalendo hata kidogo; hii ni roho ya kichawi, ubinafsi na umimi, ambayo haijawahi kumfanikisha yeyote yule.

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) ambacho mmekuwa mkikivimbishia na kukitunishia misuli huku mkishindana nacho, kukitukana, kuwatukana wanachama na viongozi wake; wala si mchawi wenu, mchawi ni nyinyi wenyewe mnaotaka kulazimisha kushika madaraka wakati muda na wakati wenu bado; huku mkitaka kujenga UKUTA juu ya mchanga kwani msingi hamjauchimba bado.

CCM si CCM kama mnavyodhani; CCM ni Mwalimu Nyerere ambaye alisimama kuwaunganisha watanzania kwanza na si kuwagawa kama mnavyofanya, lakini pia alianzia kwenye ngazi ya jamii kwanza kama mwalimu na mdau wa elimu aliyejitolea kuipigania elimu ya Tanzania na Watanzania; hivyo alisimama kama mtoa Huduma za Kijamii kwa Watanzania na Tanzania kwanza; ndipo baada ya hapo akajiingiza kwenye masuala ya Kisiasa na kuunda Chama cha TANU ambayo baadaye ndiyo ikawa CCM.

Hii ndiyo sababu CCM inawaumiza kichwa CHADEMA, wana-CHADEMA na wapinzani wengine kutoka ndani na nje ya Tanzania; kwani CCM haikulala na kuamka ikajikuta imekuwa Chama Tawala hapana BIG NO! CCM si CCM kama nilivyotangulia kusema hapo awali, bali CCM ni Mwalimu Nyerere na CCM ni Legacy ya Mwalimu Nyerere; ambaye yeye aliujenga msingi wa CCM kwa kuanzia kwenye ngazi ya chini kabisa kwa jamii (akiwa kama Mwalimu); hivyo mtu (au chama chochote) anayetaka kuwa kama CCM inampasa kuwa na vitu vifuatavyo kwanza kabla ya yote ndipo siku moja awaze kupokea kijiti cha madaraka kutoka kwa CCM na wala si kuwapora wala kuwanyang'anya kwa nguvu.

  • Hekima ya Kiungu

  • Afanye kama yale ambayo Mwalimu Nyerere alifanya na zaidi ya Mwalimu Nyerere aliyoyafanya ikiwemo kuanzia chini kabisa kwenye ngazi ya jamii; na hii si kupitia kushika nafasi za Uongozi wa Serikali za Mitaa wala kushika Nafasi za Uongozi wa Kata; bali kupitia mtu au Chama cha Kisiasa kufanya kazi kama Shirika la Kijamii lenye Kubuni na Kutekeleza Miradi midogo midogo na ya kati ya Kijamii yenye kunufaisha na kugusa mioyo ya jamii na mtu mmojammoja moja kwa moja.

  • Utulivu

  • Heshima na Nidhamu kwa Chama Tawala; kwani mzazi ni mzazi siku zote atabaki kuwa mzazi haijalishi mapungufu aliyonayo, hivyo huwezi kumtukana Mama au Baba yako kisha kumpoka madaraka ya Umama au Ubaba wake kwa nguvu kisa kuna mahali amekosea; La hasha! Lazima atatumia Ubaba au Umama wake kukudhibiti kama mtoto wake na hayo madaraka hutayapata. Hii ndiyo sababu Neno la MUNGU Linasema: "Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa MUNGU; na ile iliyopo umeamriwa na MUNGU." (Warumi (Romans) 13:1)

    Tafsiri yake ni kuwa; kuitukana mamlaka, kuipinga mamlaka pasipo kutumia hekima, kuiongelea vibaya mamlaka, kutaka kuipanda kichwani mamlaka na kufanya chochote kinachofanana na hayo ni kuenenda kinyume na NENO LA MUNGU; hivyo mamlaka ina uwezo wa kukufanya lolote na NENO LA MUNGU Limekwishasema kuhusu hili: "Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; kwa kuwa yeye ni mtumishi wa MUNGU kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni Mtumishi wa MUNGU, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu." (Warumi (Romans) 13:3-4)

  • Uvumilivu au Subira kwa sababu mchakato utakachukua muda kidogo

Kuanzisha msingi imara kuanzia chini kabisa kwenye ngazi ya jamii ndiyo sababu cheo maarufu cha Hayati Julius Kambarage Nyerere si Rais (ambacho ni cheo cha juu au ukuta uliojengwa na msingi aliouweka); bali ni Mwalimu (ambacho ni cheo cha msingi na ndio msingi wenyewe alioujenga)

Na hii pia ndiyo sababu hata ukienda kwenye vijiji vingi leo hii visivyo na mawasiliano ya simu, barabara na vyombo vya habari; lakini bado wanamjua Nyerere na bado wanaijua CCM.

Wazo lenu CHADEMA na chama chochote cha siasa cha upinzanzi kutaka na kupenda kushika madaraka si wazo baya ni wazo zuri sana; lakini naomba niwaulize maswali yafuatayo:-

  1. Je! Mpaka leo hii kwa kutumia ukubwa wa jina la chama chenu, ukubwa wa majina ya baadhi ya viongozi wenu, wadau wanaowaunga mkono kutoka ndani na nje ya tanzania lakini pia umri mlio nao; ni jambo lipi kubwa mmeshawahi kulifanya kwa manufaa na maslahi ya Tanzania na Watanzania?
  2. Je! Mpaka leo hii kwa kutumia ukubwa wa jina la chama chenu, ukubwa wa majina ya baadhi ya viongozi wenu, wadau wanaowaunga mkono kutoka ndani na nje ya tanzania lakini pia umri mlio nao; ni miradi mingapi ya elimu, kilimo, madini, ujasiriamali, uchumi au afya hata ile midogo na ya chini kabisa mmewahi kuibuni na kuitekeleza kwa Tanzania na Watanzania?
  3. Je! Mpaka leo hii kwa kutumia ukubwa wa jina la chama chenu, ukubwa wa majina ya baadhi ya viongozi wenu, wadau wanaowaunga mkono kutoka ndani na nje ya tanzania lakini pia umri mlio nao; ni mara ngapi mmekwishatatua changamoto za Watanzania ambazo CCM wameshindwa kuzitatua (mfano kwenye sekta ya Teknolojia, Kilimo, Elimu, Afya, na nyinginezo ambazo ni za Kijamii na si za Kisiasa)?
  4. Kama jibu ni hakuna; Je! Mnasubiri mpaka muingie madarakani ndipo muanze kujihusisha na Masuala ya Kijamii?
  5. Mfano mzuri ni wadau wa maendeleo wa kimataifa au wahisani (wafadhili) wa mashirika ya kijamii ambao wengi wao hutoa ufadhili kwa wingi kwa mashirika (organizations) ambazo zimeshafanya vitu tayari na yameshapiga hatua kufikia kati au mbali, huku baadhi ya wahisani hawa wakiwapa kisogo wale wenye mashirika yenye hatua za awali, changa na ambao bado hawajafanya chochote ila tu wana wazo zuri (good idea) ya kuanzisha shirika. Je! Unadhani ni kwa nini?

BWANA YESU KRISTO Amesema: "Mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu hata kile alichonacho atanyang'anywa" (Mathayo (Mathew) 25:29) (Luka (Luke) 19:26)

Kwa waraka huu, baada ya jana kutangazwa ya kuwa CHADEMA hamtashiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025 kwa sababu ya nyinyi wenyewe kukataa kwa makusudi kutosaini kanuni za maadili ya uchaguzi; ni vyema sasa mkajipanga kurudi kwa jamii mkaihudumie jamii kwa huduma za kijamii ili mkawa-challenge CCM huko kwa vitendo na wala si kwa maneno kama mfanyavyo na ambavyo mmekuwa mkifanya siku zote.

Nendeni mkatumie ukubwa wa jina la chama chenu, ukubwa wa majina ya baadhi ya viongozi wenu, wadau wanaowaunga mkono kutoka ndani na nje ya Tanzania lakini pia umri mlio nao; mkawe Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mkahudumie jamii na kujenga msingi kwa jamii kwanza kabla hamjataka kuitawala jamii kisiasa... Itaendelea
Mleta mada ishia hapo kabla sijawatuma malaika wangu wakuchalaze viboko,

Ccm ni vibuli, ccm wajiona ni nchi , ccm,ccm naita mara mbili wanaharibu nchi .ccm wanabambikia kesi ya huaini ,ccm haina jema , ccm imekwisha kabisa kabisa alisema dr Remmy( R.IP )

Ccm ,ccm mtavuna ambacho hamkupanda period
 
Natolea tu mfano wa namna ambavyo huduma za kijamii ni nyingi; na bila shaka CHADEMA wangetaka pia wangeweza kufungua kwani hawasikii malalamiko ya watanzania kuhusu wanavyosumbuka na kuteseka na mikopo ya kausha damu kila siku?
Kwanza cdm ni chama cha kisiasa na sio taasisi ya kifedha. Ccm pamoja na ukongwe wao wana bank? Kama kila taasisi itafanya unavyosema, basi team za mpira za yanga na simba zingekuwa na mabenk, mahoteli, viwanja vya mpira nk, ama wao hawaoni hizo fursa? Je team za simba na yanga kukosa hiyo miradi zimepunguza ushawishi wake kwa umma?
 
It doesn't work like that mkuu;

Upinzani unahitaji agenda setting ambayo haijielekezi kwenye election tu.

Unakumbuka miaka ya 2006 hadi 2012 hivi. Vijana wengi tulivutiwa na CDM kwa sababu ya agenda setting iliyokuwepo; ufisadi nk. Mimi binafsi nimepigwa mabomu mara 3 Arusha mwaja 2009 nadhani; tulioigwa kiwanjani jukwaani akiwepo SG na Chair na baadaye tulitaka tukamchukue mwanachama central. CDM ile ilikuwa na watu wa makundi mengi na wenye kujenga hoja vizuri bila papara; unamkumbuka JJM wa miaka hiyo? ZZK na uchumi wake? Kafulila nk? Leo watu hao wako wapi; kumekuwa na CDM mpya ya waropokaji na watukanaji na washambuliaji...

Imagine kina mdude siku hizi wanapewa mike, kina Sativa wanatukana matusi ya nguoni, kina pambalu wanaishia kupayuka tu hakuna utulivu.... too sad kwa sisi ambao CDM ilituvutia sana; wako wapi wazee wenye busara kama kina baregu, kina Prof Safari nk... kabla ya NRNE CDM inahitaji strategy mpya hii ya sasa ni useless... too sad lakini ndiyo ukweli

Na bahati mbaya vijana wa sasa wa CDM KILA uzi against wao humu majukwaani kazi yao ni kumshambulia mtoa hoja. CDM inazidi kujitenga na watanzania....
Unataka kuona cdm ya 2009 na sijui mwaka gani huko, lakini huangalii mazingira ya sasa. Unaongelea mazingira ambayo mpinzani alikuwa anaweza kwenda kwenye chombo cha habari na kufanya mdahalo, wakati sasa hivi ni tofauti. Unaongelea miaka ambayo bunge lilikuwa na spika anayeangalia hoja na sio chama anachotoka. Unaongelea wakati demokrasia ikiwa inaridhisha, unafananisha na sasa.

Sasa hivi polisi anajivunia kuwa mwanaccm hadharani, wakati katiba imetenga kabisa siasa na vyombo vya dola. Naona kama unataka uone vumbi likiwa linatimka juu ya bahari. Tazama uhalisia wa sasa, na sio hizo hadithi za hapo zamani za kale.
 
It doesn't work like that mkuu;

Upinzani unahitaji agenda setting ambayo haijielekezi kwenye election tu.

Unakumbuka miaka ya 2006 hadi 2012 hivi. Vijana wengi tulivutiwa na CDM kwa sababu ya agenda setting iliyokuwepo; ufisadi nk. Mimi binafsi nimepigwa mabomu mara 3 Arusha mwaja 2009 nadhani; tulioigwa kiwanjani jukwaani akiwepo SG na Chair na baadaye tulitaka tukamchukue mwanachama central. CDM ile ilikuwa na watu wa makundi mengi na wenye kujenga hoja vizuri bila papara; unamkumbuka JJM wa miaka hiyo? ZZK na uchumi wake? Kafulila nk? Leo watu hao wako wapi; kumekuwa na CDM mpya ya waropokaji na watukanaji na washambuliaji...

Imagine kina mdude siku hizi wanapewa mike, kina Sativa wanatukana matusi ya nguoni, kina pambalu wanaishia kupayuka tu hakuna utulivu.... too sad kwa sisi ambao CDM ilituvutia sana; wako wapi wazee wenye busara kama kina baregu, kina Prof Safari nk... kabla ya NRNE CDM inahitaji strategy mpya hii ya sasa ni useless... too sad lakini ndiyo ukweli

Na bahati mbaya vijana wa sasa wa CDM KILA uzi against wao humu majukwaani kazi yao ni kumshambulia mtoa hoja. CDM inazidi kujitenga na watanzania....
Aisee! Hii ni zaidi ya comment ndugu yangu. Kongole nyingi kwako
 
Mleta mada ishia hapo kabla sijawatuma malaika wangu wakuchalaze viboko,

Ccm ni vibuli, ccm wajiona ni nchi , ccm,ccm naita mara mbili wanaharibu nchi .ccm wanabambikia kesi ya huaini ,ccm haina jema , ccm imekwisha kabisa kabisa alisema dr Remmy( R.IP )

Ccm ,ccm mtavuna ambacho hamkupanda period
Haa! Malaika gani hao? Jeshi la Malaika lililo upande wangu ni kubwa kuliko jeshi lolote lingine. Sina hofu wala mashaka, kwa sababu ninaye BWANA wa majeshi. Kazi inaendelea!
 
Back
Top Bottom