CHADEMA badilisheni hiyo kauli mbiu ya "No Reforms, No Elections"

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
My two cents from a distance.

Siyo siri kwamba naunga mkono kutokushiriki chaguzi za maigizo zinazoendeshwa na CCM.

Naunga mkono harakati karibu zote za mwenyekiti mpya wa CHADEMA za kuleta mabadiliko ya kweli.

Yote anayofanya ni sahihi kasoro hili la kusema kuwa watazuia uchaguzi kufanyika.

Hiyo kauli si sahihi kwani inaeleweka na kutafsirika kama vile kutakuwepo na harakati za kutumia nguvu kuufanya huo uchaguzi usifanyike.

Hivi CHADEMA haina wataalamu wa mawasiliano ambao kazi yao ni kuzi fine tune hizo kauli mbiu zao?

Kusema mtauzuia uchaguzi kufanyika mnawachanganya watu maana haieleweki mtauzuiaje huo uchaguzi usifanyike.

Ibadilisheni hiyo kauli mbiu.
 
Hata mimi nilitaka tafsiri ya hiyo kauli yake.. Lakini juzi mwandishi wa dk 45 ITV alimhoji swali hilohilo.

Majibu yake yalikuwa atapaza sauti kwa wananchi ikiwemo maandamano na kupiga kampeni wasishiriki chaguzi. Waaiachie ccm yenyewe... Ametumia lugha ya kisheria kwa mbali kumuelewa inabidi uwe na uelewa mpana..
 
Nyani Ngabu tuwaache CHADEMA wafanye kwa sehemu yao. Wamesema kuna njia nyingi za kuzuia uchaguzi.

Tuwaache wafanye kwa sehemu yao. Hakuna ajuaye kesho. Ni Mungu tu.

Hata wa Israel walivofika bahari ya sham hawakuamini kuwa watavuka. Walianza kumhoji Mussa kuwa wanawezaje kuvuka? ila Mungu alifanya muujiza wa kuitenganisha Bahari na wakavuka.

Lissu alisema tufanye kwa sehemu yetu na kuna njia nyingi za kufanikisha hili. Tusipofanikiwa watakuja kufanikiwa watoto wetu. Ila ni kauli imara sana kutoka kwa mpiganaji.

Kikubwa tuwaombee kwa Mungu!
 
Kakosea kwenye kuchagua maneno yake.

Sidhani kama katumia lugha ya kisheria.

Kakosea tu katika kuchagua maneno ya kutumia.

It’s okay. Hata Lisu huwa anakosea.
 
Nyani Ngabu tuwaache CHADEMA wafanye kwa sehemu yao. Wamesema kuna njia nyingi za kuzuia uchaguzi.

Tuwaache wafanye kwa sehemu yao. Hakuna ajuaye kesho. Ni Mungu tu.

Hata wa Israel walivofika bahari ya sham hawakuamini kuwa watavuka. Walianza kumhoji Mussa kuwa wanawezaje kuvuka? ila Mungu alifanya muujiza wa kuitenganisha Bahari na wakavuka.

Lissu alisema tufanye kwa sehemu yetu na kuna njia nyingi za kufanikisha hili. Tusipofanikiwa watakuja kufanikiwa watoto wetu. Ila ni kauli imara sana kutoka kwa mpiganaji.

Kikubwa tuwaombee kwa Mungu!
He is doing the right thing the wrong way?
 
Kwa Mujibu wa katiba Hakunaga Mtu au kikundi cha Watu chenye uwezo wa kuzuia Uchaguzi

Labda watumie njia za Kienyeji za ulozi 🐼
 
My two cents from a distance.

Siyo siri kwamba naunga mkono kutokushiriki chaguzi za maigizo zinazoendeshwa na CCM.

Naunga mkono harakati karibu zote za mwenyekiti mpya wa CHADEMA za kuleta mabadiliko ya kweli.

Yote anayofanya ni sahihi kasoro hili la kusema kuwa watazuia uchaguzi kufanyika.

Hiyo kauli si sahihi kwani inaeleweka na kutafsirika kama vile kutakuwepo na harakati za kutumia nguvu kuufanya huo uchaguzi usifanyike.

Hivi CHADEMA haina wataalamu wa mawasiliano ambao kazi yao ni kuzi fine tune hizo kauli mbiu zao?

Kusema mtauzuia uchaguzi kufanyika mnawachanganya watu maana haieleweki mtauzuiaje huo uchaguzi usifanyike.

Ibadilisheni hiyo kauli mbiu.
Ni Bora kutoshiriki kuliko kuuzuia maana Kwa niijuavyo CCM na vyombo vyake vya dola ni lazima vurugu itatokea hasa kama Lissu ataimiza watu waandamane
 
Hata mimi nilitaka tafsiri ya hiyo kauli yake.. Lakini juzi mwandishi wa dk 45 ITV alimhoji swali hilohilo.

Majibu yake yalikuwa atapaza sauti kwa wananchi ikiwemo maandamano na kupiga kampeni wasishiriki chaguzi. Waaiachie ccm yenyewe... Ametumia lugha ya kisheria kwa mbali kumuelewa inabidi uwe na uelewa mpana..
Mnavyokimbiliaga uelewa mpana sasa,utasema mnao kumbe nyumbu tu
 
Kuna uandikishaji na uhuishaji wa taarifa za wapiga kura unaendelea baadhi ya mikoa, sioni CHADEMA wakihamasika. Nadhani wameitikia kauli mbiu kuwa hakuna Uchaguzi mwaka huu!
 
Back
Top Bottom