CHADEMA badilisheni hiyo kauli mbiu ya "No Reforms, No Elections"

CHADEMA badilisheni hiyo kauli mbiu ya "No Reforms, No Elections"

My two cents from a distance.

Siyo siri kwamba naunga mkono kutokushiriki chaguzi za maigizo zinazoendeshwa na CCM.

Naunga mkono harakati karibu zote za mwenyekiti mpya wa CHADEMA za kuleta mabadiliko ya kweli.

Yote anayofanya ni sahihi kasoro hili la kusema kuwa watazuia uchaguzi kufanyika.

Hiyo kauli si sahihi kwani inaeleweka na kutafsirika kama vile kutakuwepo na harakati za kutumia nguvu kuufanya huo uchaguzi usifanyike.

Hivi CHADEMA haina wataalamu wa mawasiliano ambao kazi yao ni kuzi fine tune hizo kauli mbiu zao?

Kusema mtauzuia uchaguzi kufanyika mnawachanganya watu maana haieleweki mtauzuiaje huo uchaguzi usifanyike.

Ibadilisheni hiyo kauli mbiu.
Huu ushauri wako bila shaka huwajui CCM vizuri. Usije ukashiba magimbi kutoka nanjilinji na kuja kutoa ushauri. No reforms no Election is very perfect. Watazuia vipi kaa utulie wewe omba uhai tu
 
Hata kama ni kwa nguvu powa tu hakuna uhuru unaopiganiwa bila nguvu hasa kwa serikali ambazo zina rushwa kubwa hivi
Ni rahisi kusema hivyo ukiwa zako River Oaks 🤣.
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Hiyo ilani au kaulimbiu ishawatoa pangoni mabalozi wa mabeberu na sasa wanapishana kwenda Chamwino kwa VP, Magogoni kwa PM na Lumumba kwa KM na Tyson
 
My two cents from a distance.

Siyo siri kwamba naunga mkono kutokushiriki chaguzi za maigizo zinazoendeshwa na CCM.

Naunga mkono harakati karibu zote za mwenyekiti mpya wa CHADEMA za kuleta mabadiliko ya kweli.

Yote anayofanya ni sahihi kasoro hili la kusema kuwa watazuia uchaguzi kufanyika.

Hiyo kauli si sahihi kwani inaeleweka na kutafsirika kama vile kutakuwepo na harakati za kutumia nguvu kuufanya huo uchaguzi usifanyike.

Hivi CHADEMA haina wataalamu wa mawasiliano ambao kazi yao ni kuzi fine tune hizo kauli mbiu zao?

Kusema mtauzuia uchaguzi kufanyika mnawachanganya watu maana haieleweki mtauzuiaje huo uchaguzi usifanyike.

Ibadilisheni hiyo kauli mbiu.
Pumbavu
 
Mkuu, ungependekeza pia walau maneno unayoona yangefaa kutumika. Lissu ametolea ufafanuzi mzuri sana hiyo kauli mbiu.

Binafsi naona inafaa maana inaleta attention zaidi hata CCM wanastuka what if kweli uchaguzi usiweze kufanyika na mtu ameshawekeza hela 🤣🤣
 
Kuna mambo yanashangaza sana
unaogopa maandamano et yataleta vurugu
at the same time hutaki mabadiliko yaan maanake umekubali kunyonywa na watawala walioamua kukutawala milele kwa kukukandamiza haki zako za msingi..

Kama kutumia vurugu kudai haki yangu kikatiba ni kosa basi kwangu ni njia sahihi.
 
Hu kinda sana , wenda wajiona ulipo hufikiki ila nakupa onyo kubwa na sio ombi ,unafikika pitia Mungu wangu hapa jf, ukiendelea nitakuonesha kwamba Mungu ni juu sana , mwanalaana mkunwa
🖕🖕🖕
 
Yes.

CHADEMA wahamasishe watu kutokushiriki chaguzi.

Kuzuia uchaguzi usifanyike ni vague plan.

Sasa wanapoamua kuchukua hatua ili kukomesha ujinga ujinga nchini nyie mnakuja na habari za "ahaaa, msifanye hivyo".

Wakibaki na maneno matupu, mnakuja hapa kusema "nyie huwa mnabweka tu hamna lolote".

Miluzi mingi hupoteza mbwa!

By the way, umewahi kuleta hapa mada ya namna ya kufanya Civil disobedience, leo hutaki hizo mbinu zitumike kuzuia uchafuzi?
 
Kuna mambo yanashangaza sana
unaogopa maandamano et yataleta vurugu
at the same time hutaki mabadiliko yaan maanake umekubali kunyonywa na watawala walioamua kukutawala milele kwa kukukandamiza haki zako za msingi..

Kama kutumia vurugu kudai haki yangu kikatiba ni kosa basi kwangu ni njia sahihi.
Mkuu njoo mtaani , kwa afisa elim, Tarafa ,walim wakuu , wote hujifanya ni level flani, njoo kwa vya vyalim ambavyo husimamia mitiani ya darasa la saba, la nne ,utacheka kipumbavu , nchi hii ina watu mijinga sana,

Wanajitutumua hao , bila jua wanatumimiwa kama karatasi wakati mwenye barua wapo ,

Hawa wajinga hufikili kua na no ya mkuu wa mko DAS,RAS Basi umefika palipo,

Wajinga sana hawa
 
No reforms, no elections, ni nzuri, kama wana hiyo popular support, na kama watafanya mambo hayo kwa amani, wamesema watafanya civil disobedience kwa amani, na watazungumza na wafadhili.

Kama wafadhili wata respond, wanatakiwa warespond, kwa namna ambayo haitaumiza wananchi (may be in a peaceful and targeted way).

Lissu yuko sahihi pia kusema kwamba mbunge wa viti maalumu aliekaa bungeni muda mrefu, akagombee jimboni, endapo chadema itashiriki uchaguzi.

Lissu na wafuasi wake ndani ya chadema, wawe free kabisa kuiongoza chadema.

Wabunge 19 wanawake wa chadema, au wabunge wowote wa zamani wa chadema, wanaweza waka angalia upepo unavyoenda, kama wanaona hawana future nzuri ndani ya chadema, wanaweza wakaongea na wapiga kura wao majimboni, kuona kama wagombee kwa tiketi ya ccm.

Nadhani Mbowe aongee na wapiga kura wa jimbo la Hai, kama wanataka agombee ubunge au asigombee ubunge.

Na kama agombee, je ni kupitia chadema au ccm. Kama kupitia chadema ok. Kama kupitia ccm, basi ajiunge na ccm. Na akishinda ubunge, na ccm ikishinda uchaguzi, saa100 anaweza kumteua Mbowe kuwa waziri mkuu wa Tanzania.

Wengine wanaoweza kuwa waziri mkuu wa Tanzania ni Mkenda, Mwigulu, Kabudi, au mbunge mmoja atakae toka eneo la usukumani (kabila lake awe ni msukuma, na sio mtu wa mkoa wa Mara).

Waprotestanti wapewe preference kwenye nafasi ya uwaziri mkuu, kama hakuna mprotestanti anaefaa, basi waziri mkuu awe mkatoliki (kama Mkenda). Waziri mkuu atoke mbali na kusini, as Nchimbi makamu wa rais mtarajiwa anatokea kusini tayari.

Majaliwa anaweza kuendelea kuwa waziri, na sio waziri mkuu. Kimei anaweza kuteuliwa kuwa naibu waziri wa wizara fulani.

Mtu yeyote wa chadema ambaye, anaona kwamba hata fikia potential yake chini ya uongozi mpya wa chadema, anaweza akawa mpole au anaweza akahamia ccm. Ccm isiwatumie watu wanao hamia kutoka chadema, kama nyenzo ya propaganda mbaya, dhidi ya wenzao waliobaki huko chadema.

Vuguvugu la uzalendo limeongezeka, hususan baada ya Tundu Lissu kushinda chadema. Inaelekea kanisa katoliki limeongeza uwekezaji wao huko chadema. Naona pia mkoa wa Mara umeongeza uwekezaji wao huko chadema.

Inabidi Saa100, kama anaweza, a renegotiate mikataba yote mibovu na aifanye iwe na maslahi na ustawi mzuri kwa watanzania.

Abalance vizuri uzalendo, haki za binadamu na demokrasia, huku akiendelea kuwa na mahusiano mazuri na mataifa yenye nguvu duniani. Awe pia na mahusiano mazuri na mikoa yote ya Tanzania. Awe pia na mahusiano mazuri na wachagga.

Saa100 pamoja na bunge, wanaweza wakapitisha sheria ya kuruhusu urais kuwa term tatu, za miaka mitano kila term. Au urais kuwa term mbili, za miaka sita kila term. Wabunge na madiwani wawe na terms za miaka sita, na sio mitano kama ilivyo sasa.

Kwa sasa hii inawezekana, as karibia bunge lote ni ccm. Term za miaka 6, zitapunguza gharama za uchaguzi mkuu.

Miaka saba hapana, ni mingi sana.

TZ diaspora walio acha uraia wa Tanzania, wapewe muhuri wa permanent resident (au permanent leave to remain), kwa urahisi sana, kwenye passport zao mpya za kigeni. Wanaweza pia wakapewa special status, ambayo pia ita include hayo hapo juu.

Umri wa kukana au kuchagua uraia kwa watoto wa kiTZ wenye fursa ya uraia wa zaidi ya nchi moja, uwe ni miaka 30, na sio miaka 18 kama sasa.

Hii itawawezesha watoto hao wa kiTZ kunufaika na elimu nzuri na ya gharama nafuu hadi chuo kikuu, huko ughaibuni.

Umri wa chini wa kuruhusiwa kufanya vitu ambavyo sio vizuri, upandishwe kutoka miaka 18 hadi miaka 21, kama matumizi ya pombe/alcohol, sigara/tobacco/shisha, kamari/sportsbetting/casino/lottery, kwenda disco/nightclub, cinema za miaka 18 huko nje, hapa ziwe ni miaka 21.

Pia shisha au na aina zote za kamari, ziwe regulated au banned, kama vimekuwa out of control.

Umri wa kupiga kura ushushwe na uwe ni miaka 15. Umri wa kufanya kazi nyepesi uwe ni miaka 15. Umri wa kufanya kazi nzito uwe ni miaka 21.

Umri wa kuruhusiwa kujiunga na majeshi uwe ni miaka 21; wakati wa vita, umri huo unaweza kushuka na kuwa miaka 18.

Umri wa kuoa au kuolewa, na wa kuruhusiwa kufanya mapenzi uwe ni miaka 21. Watu wenye umri wa miaka 18, wataweza kuoa au kuolewa kwa ridhaa ya wazazi.

Umri wa kuendesha gari uwe ni miaka 18 (class B na D). Umri wa kuendesha magari makubwchademai miaka 21.

Saa100, inabidi aendelee na concept ya TZ as a developmental state.
 
Sasa wanapoamua kuchukua hatua ili kukomesha ujinga ujinga nchini nyie mnakuja na habari za "ahaaa, msifanye hivyo".

Wakibaki na maneno matupu, mnakuja hapa kusema "nyie huwa mnabweka tu hamna lolote".

Miluzi mingi hupoteza mbwa!

By the way, umewahi kuleta hapa mada ya namna ya kufanya Civil disobedience, leo hutaki hizo mbinu zitumike kuzuia uchafuzi?
Hivi umeelewa ulichokisoma kweli? Kama umeelewa, hebu nieleze tu kwa sentensi hata mbili kuhusu hicho ulichokielewa halafu baada ya hapo tunaweza kuendelea.
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Kuna uandikishaji na uhuishaji wa taarifa za wapiga kura unaendelea baadhi ya mikoa, sioni CHADEMA wakihamasika. Nadhani wameitikia kauli mbiu kuwa hakuna Uchaguzi mwaka huu!
Kilichonivutia kwenye uzi huu, licha ya uzito wa hoja ya Ngabu, ni Paskali ku👍 karibu kila comment
 
Hivi CHADEMA haina wataalamu wa mawasiliano ambao kazi yao ni kuzi fine tune hizo kauli mbiu zao?
Wataalam wa mawasiliano kabisa, au unaota ndoto? Kama mwenyekiti mwenyewe anachanganga hoja/sera na matusi/uropokaji, unategemea hao Wataalam wa mass communication watatoka wapi?
 
Hivi umeelewa ulichokisoma kweli? Kama umeelewa, hebu nieleze tu kwa sentensi hata mbili kuhusu hicho ulichokielewa halafu baada ya hapo tunaweza kuendelea.

Rxt
Uliposema hivi, nanukuu "Hiyo kauli si sahihi kwani inaeleweka na kutafsirika kama vile kutakuwepo na harakati za kutumia nguvu kuufanya huo uchaguzi usifanyike."

Wewe it seems unahofia au hutaki CHADEMA watumie nguvu kuuzuia uchaguzi, Sisi wengine tunasema kuwa JAPO kauli ya No Reforms no election si lazima imaanishe kutumia nguvu, lakini sisi wengine tunasena kuwa kama Chadema wanaweza kuitumia hiyo nguvu kuzuia jinai ya uchaguzi feki (uchafuzi) basi hilo ni jambo zuri sana maana kusaidia kuzuia jinai ni mojawapo ya majukumu ya kila raia.
 
Mimi sijazungumzia kauli ya no reforms no elections.

Ndo maana nikakuambia kwamba hujaelewa nilichokiandika.

Na mods hawajasaidia. Wamenibadilishia kichwa cha mada na sasa watu mnakisoma halafu mnahitimisha kuwa hivyo ndivyo nilivyosema.

Mimi sina tatizo lolote lile na kauli mbiu ya no reforms no elections.

Soma tena kwa utulivu bandiko langu utaona nilicho na tatizo nacho.
 
Back
Top Bottom